Na MWANDISHI WETU
UONGOZI mpya wa Taasisi ya Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA) leo umekabidhiwa rasmi ofisi na uongozi uliopita baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Julai 11 mwaka huu.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Anatouglou, jijini Dar es Salaam, yalipo makao makuu ya UKUTA, Mwenyekiti wa taasisi hiyo taifa, Hussein Ally Jimbika, amesema , wamejipanga kusimamia kikamilifu usanifu wa lugha ya Kiswahili na ushairi nchini.
Amesema, UKUTA itaendelea kuenzi jitihada za kubwa za viongozi na waasisi wa taasisi hiyo hususan Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye ndiyo mtu wa kwanza kuunda chombo hiki kabla ya uhuru kwa kushirikiana na hayati Abeid Aman Karume na Sheikh Amri Abeid Karuta.
Ameeleza UKUTA ilitoa mchango mkubwa katika kufanikisha taifa kupata uhuru na kwamba uongozi wa taasisi hiyo utaendelea kufuata nyendo zao kuhakikisha safari ya kuenzi Kiswahili inafanikiwa.
“Wazee hawa walikuwa na makusudio makubwa ya Kiswahili kuwa ni nyenzo muhimu ya kupata uhuru na ustawi wa taifa.
Hivyo Uongozi mpya tutashirikiana na wenzetu kuhakikisha lengo la waasisi hawa linaendelewa na kufikiwa katika kukuza Kiswahili,”amesema Jimbika.
Jimbika alisema lengo lingine ni kuongeza usajili wa wanachama kwani mpaka sasa UKUTA inawachama 2050 tu.
Katibu Mkuu wa UKUTA, Abubakyr Kiaibamba, amewarika wanachama wa katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo zilizopo katika jengo la Anatouglou kwa uratibu wa shughuli zote za taasisi na kujisajili .
“Malengo yangu ni kuhakikisha tunakifanya Kiswahili kuwa bidhaa. Hii ndiyo kazi anayoifanya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Tutahakikisha vitabu vinaandikwa, mashairi yanatungwa na tunawakomboa washairi kuchumi kupitia kazi zao,”amesema Kiaibamba.
Akikabidhi nyaraka za ofisi Katibu Mkuu mstaafu Hassan Ligile, ameupongeza uongozi huo mpya kushinda katika uchaguzi wa kidermokrasia uliofanyika na kwamba wataendelea kutoa ushirikiano kuhakikisha UKUTA inasonga mbele huku akijivunia mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...