Na Mwandishi Wetu

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mariam Abdallah Ibrahim ambaye pia ni Mbunge wa Mkoa wa Pwani ametoa Sh.milioni moja kwa ajili ya Kusaidia kukamilisha Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa Jumuiya hiyo wilayani Gairo mkoani Pwani.


Mbunge Mariam amekabidhi fedha hizo akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na vikundi vya wajasiriamali hasa walioko kwenye Jumuiya ya UWT .

Akiwa katika ziara hiyo alipata nafasi ya kukagua pia nyumba ya mtumishi wa Jumuiya ya UWT Wilaya ya Gairo ambapo amekabidhi mchango wake wq fedha Sh. milioni moja ili kusaidia kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mtumishi huyo.

Akizungumza na wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewashukuru wakazi wa Mkoa wa Morogoro kwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu kwa kumpatia kura nyingi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwachagua wabunge na madiwani wa chama hicho.

Mbunge Mariam pia amewahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ndani ya CCM, akieleza kuwa ushiriki wao katika nafasi za maamuzi ni muhimu katika kuimarisha maendeleo na kuendelea kutetea maslahi ya wanawake na jamii kwa ujumla.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za UWT Taifa za kufuatilia utekelezaji wa shughuli za jumuiya hiyo, kuhamasisha maendeleo ya wanawake, na kuimarisha ushiriki wao katika shughuli za kisiasa, kijamii na kiuchumi.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...