Zaidi ya Shilingi milioni 700 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kashishi iliyopo Kata ya Nyakamwaga Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Shule hiyo inatarajiwa kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndugu Wazo Michael Mwang’onda, ndiye aliyeweka jiwe la msingi katika ujenzi wa shule hiyo wakati Mwenge ulipofika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi, Mwang’onda amesema ameridhishwa na mradi huo ambao mpaka sasa umefikia asilimia 75 ya utekelezaji. Amesema ni shule ya kwanza ya Serikali yenye muonekano wa gorofa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Ameeleza kuwa shule hiyo ilianzishwa kwa nguvu za wananchi na baadaye kuungwa mkono na mdau wa maendeleo, Mhe. Evarist Gervas, ambaye ametumia zaidi ya Shilingi milioni 300 kukamilisha miundombinu.
Mwang’onda amesema mradi huo utakuwa na madarasa zaidi ya 8, matundu 12 ya vyoo pamoja na ofisi mbalimbali. Pia ametoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano wa Mhe. Gervas kwa kuunga mkono juhudi za wananchi katika kukuza maendeleo ya elimu Kata ya Nyakamwaga.
Kwa upande wao wananchi wa Kijiji cha Kashishi wamesema walianzisha ujenzi wa shule hiyo ili kupunguza umbali wa watoto kwenda kusoma. Wamesema hapo awali wanafunzi walikuwa wakitembea umbali mrefu hadi Shule ya Sekondari Nyakamwaga na wengi waliishia kukatisha masomo.


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...