Na Belinda Joseph – Tanga
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimesema matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu yamewezesha wanafunzi kusoma, kufanya mawasilisho na kupata huduma za kitaaluma bila kulazimika kusafiri hadi chuoni, hatua inayopanua fursa ya elimu kwa watu waliopo ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumza Agosti 23, 2026 katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea Tanga, Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi wa OUT, Dkt. Rwejuna Zacharia, amesema chuo hicho kinatumia mifumo ya kidijitali kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia, mihadhara, mitihani, matokeo na mawasiliano kati ya wanafunzi na wahadhiri.
Amesema teknolojia hiyo imewasaidia pia wanafunzi waliopo nje ya Tanzania kushiriki katika mawasilisho ya kitaaluma kupitia Zoom pamoja na wahadhiri na wataalamu waliopo katika maeneo mbalimbali, bila kutumia gharama za kusafiri kwa ajili ya shughuli hizo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Ubunifu wa OUT na mwakilishi wa Mkuu wa Chuo, Dkt. Straton Ruhinda, amesema matumizi ya teknolojia ni sehemu ya mabadiliko makubwa katika namna elimu inavyotolewa, akisisitiza kuwa ubunifu haupaswi kuangaliwa kama matumizi ya teknolojia pekee, bali pia namna ya kurahisisha elimu na kuifanya iendane na mazingira ya mwanafunzi.
Amesema OUT inaendelea kuboresha baadhi ya mitaala na programu zake, huku ikitoa elimu kuanzia ngazi ya cheti na diploma hadi shahada za kwanza, uzamili na uzamivu (PhD), kwa kutumia mifumo inayompa mwanafunzi unafuu katika namna ya kufuatilia masomo.
Dkt. Ruhinda amesema mfumo huo umekuwa muhimu kwa wanafunzi wenye majukumu mengine, kwa kuwa unaweza kuwawezesha kufuatilia masomo kwa njia inayolingana na mazingira yao badala ya kulazimika kufika darasani kila siku.
Aidha, amesema OUT imeendelea kutumia teknolojia katika mawasiliano kati ya wanafunzi na wasimamizi wa masomo, ambapo mwanafunzi anaweza kutuma kazi yake kwa njia ya mtandao, kupata mrejesho wa mhadhiri na kuendelea na hatua zinazofuata bila kusafiri.
Dkt. Ruhinda amewakaribisha wananchi wenye nia ya kujiendeleza kielimu kutumia fursa zinazotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), akisema chuo hicho kinatoa programu mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti, hadi uzamivu (PhD), huku mfumo wake wa elimu kwa njia ya masafa ukimwezesha mwanafunzi kusoma akiwa katika eneo alilopo na kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Ushiriki wa Chuo kikuu huria cha Tanzania katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayofanyika Tanga kuanzia Agosti 15 hadi 24, 2026, unalenga kuwafahamisha wananchi kuhusu programu na fursa mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho pamoja na namna elimu kwa njia ya masafa inavyoweza kumfikia mwanafunzi akiwa katika eneo alilopo.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...