Wahadhiri wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wametwaa tuzo ya machapisho bora ya utafiti yenye hadhi ya juu zaidi Duniani iliyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, baada ya kufanya tafiti kuhusu nishati safi ya kupikia kupelekea kutambuliwa miongoni mwa machapisho bora.

Akizungumza katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea mkoani Tanga, Mhadhiri wa Chuo cha Mipango, Dkt. Aniseth Rwezaula, amesema tuzo hiyo inaonesha namna wahadhiri wa Chuo hicho kufanya tafiti katika zinazolenga kutatua changamoto za jamii.

Dkt. Rwezaula amesema Chuo hicho kina majukumu makuu matatu ambayo ni kufundisha, kufanya tafiti na kutoa huduma elekezi, huku tafiti zikitumika kuzalisha maarifa yanayoweza kusaidia kupata suluhisho la changamoto mbalimbali za wananchi.

Amesema katika kuimarisha eneo hilo, chuo hicho kilitenga shilingi milioni 500 mwaka wa fedha uliopita kwa ajili ya kuwawezesha wahadhiri kufanya tafiti, huku mwaka huu kikiongeza kiasi hicho hadi shilingi milioni 600.

Amesema tuzo hiyo imetolewa kwa machapisho yenye hadhi ya juu yaliyochapishwa katika majarida makubwa  duniani, ambapo washindi wamepewa vyeti pamoja na zawadi za fedha.

Kwa upande wake, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Mipango Kampasi ya Mwanza,  Dkt. Mwaya Biarwa, amesema chapisho lililotunukiwa tuzo lilihusu teknolojia ya nishati safi ya kupikia na mchango wake katika utunzaji wa mazingira.

Amesema utafiti huo ulifanyika katika nchi 28 za Afrika,  na Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zilizoshiriki, huku utafiti huo ukilenga kuonesha umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika kupunguza uzalishaji wa hewa ya kaboni.

Dkt. Biarwa amesema chapisho hilo liliingia  katika kundi la Natural Science na Mathematics, likishika nafasi ya nane kati ya machapisho 12 yaliyoshindanishwa na hatimaye kuwezesha  Chuo cha Mipango kutwaa tuzo hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...