Na Janeth Raphael - MichuziTv
Serikali imetangaza kuwa inatarajia kupeleka bungeni muswada wa kufuta sheria ya utaifishaji wa mifugo katika kikao kijacho cha Bunge, hatua inayolenga kuondoa changamoto zinazowakabili wafugaji na kuweka mazingira bora ya maendeleo ya sekta ya mifugo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati akifungua Maonesho ya Wakulima ya Nanenane 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya John Samwel Malecela jijini Dodoma.
Dkt. Mwigulu amesema uamuzi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha wafugaji wanafanya shughuli zao katika mazingira yenye uhakika wa kisheria, huku ikipunguza migogoro inayohusisha wafugaji, wakulima, wawekezaji na wananchi.
"Katika kikao kijacho cha Bunge, Serikali inakusudia kufuta sheria ya utaifishaji wa mifugo. Hatua hii itaenda sambamba na ushirikiano wa wizara zote zinazohusika ili kuhakikisha rasilimali na vifaa vilivyopo vinatumika kutatua changamoto zilizopo na kuimarisha uzalishaji," alisema.
Dkt. Mwigulu amezitaja WIZARA zinazopaswa kushirikiana kuwa ni Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Maji pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, akisisitiza kuwa ushirikiano huo utasaidia kupunguza migogoro ya matumizi ya ardhi na kuongeza tija katika sekta za uzalishaji.
Amesema mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi yameifanya Tanzania kuendelea kujijengea nafasi ya kuwa ghala la chakula kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Afrika Mashariki.
Amebainisha kuwa kwa sasa Tanzania imefikia kiwango cha kujitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 130, huku mauzo ya mazao nje ya nchi yakiongezeka kwa asilimia 77, jambo linaloonyesha ukuaji wa sekta hiyo na mchango wake katika uchumi wa taifa.
Akizungumzia kaulimbiu ya Maonesho ya Nanenane ya mwaka huu ya "Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050", Dkt. Mwigulu alisema ni wakati wa wakulima, wafugaji na wavuvi kuachana na uzalishaji wa mazoea na kuelekea kwenye kilimo na ufugaji wa kisasa unaozingatia ubora na mahitaji ya soko.
Amesisitiza kuwa kuongeza uzalishaji pekee haitoshi, bali bidhaa zinazozalishwa lazima zikidhi viwango vinavyohitajika ili kuongeza ushindani katika masoko ya ndani na kimataifa.
Aidha, amesema Serikali itaendelea kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo kupitia ongezeko la bajeti, kuboresha huduma za ugani na kuhakikisha maafisa ugani wanafika moja kwa moja kwa wakulima na wafugaji ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Kuhusu migogoro ya ardhi, Dkt. Mwigulu alisema suluhisho la kudumu ni kuongeza uzalishaji wa malisho ya mifugo badala ya kuendelea kutegemea maeneo machache ya malisho.
Amesema Serikali tayari imezalisha zaidi ya tani 200 za malisho na inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya maji, ikiwemo uchimbaji wa visima, ili kuhakikisha mifugo inapata maji ya kutosha na kuzuia vifo vinavyotokana na ukame.
Pia ametangaza kuwa Serikali imezindua mkakati wa miaka 10 wa maendeleo ya sekta ya kuku, unaolenga kuongeza uzalishaji, thamani ya bidhaa za kuku na fursa za kiuchumi, hususan katika Kanda ya Kati.
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, alisema Maonesho ya Nanenane yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwakutanisha wadau wa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na kuwapa wananchi elimu kuhusu teknolojia mpya na fursa za masoko.
Amesema maonesho ya mwaka huu yamewakutanisha waoneshaji zaidi ya 200 wa kimataifa kutoka nchi 24, jambo linalofungua milango ya ushirikiano, uwekezaji na upatikanaji wa masoko mapya.
Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Bashiru Kakuru, alisema Serikali imeendelea kuweka kipaumbele katika sekta za uzalishaji, huku akisisitiza kuwa mafanikio ya mageuzi yanayoendelea yanahitaji ushirikiano wa Serikali na wadau wote.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege, alisema benki hiyo imeongeza uwezo wa utoaji wa mikopo kwa sekta ya kilimo kutoka Sh bilioni 60 hadi Sh bilioni 450.
Ameongeza kuwa TADB tayari imetoa mikopo yenye thamani ya Sh trilioni 1.55, ambapo asilimia 84 ya fedha hizo zimetolewa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa ajili ya kuwawezesha wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wa mazao kuongeza uzalishaji na kukuza biashara zao.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...