Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima nchini kutonunua mbegu yoyote ambayo haina lebo ya utambuzi ya TOSCI, ikieleza kuwa lebo hiyo ndiyo uthibitisho kuwa mbegu imekaguliwa na kuthibitishwa ubora wake.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Nyasebwa E. Chimagu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika jijini Dodoma Agosti 1, 2026.
Chimagu alisema matumizi ya mbegu bora ni msingi wa kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao na kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, amesema kuwa wakulima wanapaswa kuhakikisha mbegu wanazonunua zimefungashwa katika vifungashio rasmi vyenye lebo ya TOSCI.
Alieleza kuwa wakulima wanaweza kuhakiki uhalali wa lebo hiyo kwa kutumia simu za mkononi ili kubaini kama mbegu ni halisi au la, hatua ambayo itawasaidia kuepuka kununua mbegu bandia zinazoweza kusababisha hasara.
Aidha, alisema TOSCI inaendelea kutoa elimu kupitia mabanda yake katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu zilizothibitishwa, pamoja na kutoa mafunzo kwa wazalishaji na wafanyabiashara wa mbegu kuhusu taratibu za uzalishaji, usafirishaji na biashara ya mbegu.
Chimagu alibainisha kuwa matumizi ya mbegu bora, sambamba na kuzingatia kanuni bora za kilimo, yanaweza kumwezesha mkulima kuvuna kati ya tani tano hadi kumi kwa hekta.
Aliwahimiza wakulima kutumia Maonesho ya Kilimo ya Nanenane kama fursa ya kupata elimu kuhusu mbegu bora na teknolojia mbalimbali za kilimo zitakazowaongezea tija katika msimu wa kilimo wa mwaka 2026/2027.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...