Wakulima zaidi ya 1,500 mkoani Morogoro wamenufaika na huduma za kifedha kidijitali zinazotolewa na Mixx by Yas, kupitia malipo ya stakabadhi za ghala pamoja na mikopo nafuu inayopatikana kupitia jukwaa hilo.
Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika mkoa wa Morogoro, Meneja wa Biashara wa Mixx by Yas Kanda ya Pwani Kaskazini, Bw. Anwar Kisesa, alisema huduma hiyo imewanufaisha wakulima wa mazao mbalimbali yakiwemo ufuta, korosho, mbaazi na kakao, na kuwawezesha kupokea malipo yao kwa njia salama, ya haraka na rahisi.
Alisema kampuni hiyo inaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya kilimo ili kuhakikisha wakulima wengi zaidi wanapata huduma za kifedha zitakazorahisisha shughuli zao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa vijijini.
Aidha, Bw. Kisesa aliwahamasisha wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane kwa mkoa wa Morogoro kutumia huduma ya Mixx Super App kununua tiketi za kuingia viwanjani pamoja na tiketi za maegesho ya magari, akibainisha kuwa huduma hiyo inasaidia kuepuka foleni na kurahisisha kuingia katika viwanja vya maonesho.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...