JUMLA ya wazee 246 wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wamepatiwa vitambulisho vya msamaha wa matibabu hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee bila vikwazo vinavyotokana na ukosefu wa vitambulisho hivyo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la wazee cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Sumbawanga Herry Sanga amesema wamefanikiwa kutoa vitambulisho vya msamaha wa matibabu ikiwa wanawake 138, wanaume 108 huku wazee 29 ambao hawakuwa na vitambulisho vya msamaha wa matibabu wamepewa msamaha wa muda wa matibabu.

Kwa upande wake katibu wa Baraza la wazee Manispaa ya Sumbawanga Moris Massanja amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wazee kuhusu haki zao pamoja na huduma zinazopatikana kwa ajili yao.

Utoaji wa vitambulisho vya msamaha wa matibabu kwa wazee unalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na kuhakikisha wazee wanapata huduma za matibabu kwa wakati na bila vikwazo vinavyotokana na ukosefu wa vitambulisho.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...