NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, amewapongeza viongozi wa Jimbo la Donge kwa juhudi za kutafuta wadau na wahisani wanaosaidia utekelezaji wa miradi ya elimu na malezi ya watoto.
Ndugu Abdi ameyasema hayo baada ya kutembelea na kukagua miradi ya skuli pamoja na kituo cha kulelea watoto yatima katika Jimbo la Donge, ambapo amesema jitihada hizo zina mchango mkubwa katika kuboresha huduma za elimu na malezi.
Amesema kituo hicho ni miongoni mwa njia muhimu za kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, elimu na mazingira salama yatakayowasaidia kukua katika misingi ya maadili na kuwa vijana wema wenye elimu na ujuzi wa kukabiliana na changamoto za maisha.
“Ndugu Abdi amesema CCM inapongeza jitihada zinazofanywa na viongozi wa Jimbo la Donge katika kuibua na kuendeleza miradi inayolenga kuchochea maendeleo ya elimu pamoja na kuboresha mazingira ya malezi ya watoto nchini.”
Aidha, amesema ushirikiano kati ya viongozi na wadau mbalimbali ni muhimu katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika na kutoa huduma zinazokusudiwa kwa jamii.
Miradi hiyo inajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Al-Attah Charitable Organization, ambapo inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha watoto wanapata malezi bora, elimu na mazingira salama kwa maendeleo yao.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...