Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Shughuli za serikali (Chief of Staff) wa Ghana Dkt Julius Debras ametoa wito kwa nchi za Afrika kuangalia kwa namna gani rasilimali zilizopo zinaweza kujitosheleza kama bara hususani katika sekta ya nishati.

Dkt Debras ametoa wito huo katika wiki ya mafuta Afrika inayoendelea Accra Ghana wakati wa hotuba yake akimwakilisha Rais wa nchi hiyo John Dramani Mahama.

Amesema kuwa endapo bara la Afrika litakuwa na nishati ya uhakika itasaidia kuinua uchumi lakini swala la ajira pia halitakuwa wimbo kwani kutakuwa na maendeleo ya uhakika ya viwanda.

Ameweka bayana kuwa kwa upande wa Mkondo wa Juu wa Petroli wa Ghana, serikali imeweka mikakati mathubuti kuhakikisha kupitia sekta hiyo wanapata wawekezaji wenye uhakika.

Amesema ni lazima kama bara la Afrika kuangalia aina ya wawekezaji wanaokuja kuwekeza katika nishati ni lazima wawe na nguvu ya kiuchumi ili kuweza kuleta manufaa ya uhakika na haraka katika sekta hiyo.

Kwa upande wake Kamishna wa Miundombinu na Nishati kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika Lerato Mataboge amesema vijana wa Afrika wapo tayari katika mabadiliko ya nishati yanayoendelea barani Afrika.

Amesema kinachotakiwa hivi sasa ni mshikamano wa Afrika kuweka njia madhubuti katika kuhakikisha kuwa katika kuelekea maendeleo hayo kuwe na mabadiliko makubwa katika matumizi ya teknolojia kwa kutoa vipaumbele katika bunifu zote zinazofanywa na vijana wa Afrika.

Ameweka bayana kuwa Umoja wa Afrika umeweka utengamano wa viwanda ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na ushirikiano wa kikanda katika sekta ya nishati ambao baadaye utaleta tafsiri sahihi ya kuwa na nishati ya uhakika katika bara zima.

Wiki ya Mafuta barani Afrika imeanza Septemba 01 hadi 03 ambapo Tanzania imewakilishwa na wajumbe kutoka Wizara ya Nishati, wajumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), na wajumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Petroli Zanzibar (ZPRA).





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...