Na Victor Masangu, Kibaha
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwalimu Mwajuma Nyamka, amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa na mabalozi kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa za El-Nino zinazotarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini.
Mwalimu Nyamka amewataka viongozi hao kuhakikisha wananchi wanaacha tabia ya kutupa taka hovyo na badala yake kushiriki katika usafi wa mazingira, ikiwemo kusafisha mifereji na kuzibua mitaro ili kuepusha maji kukwama na kusababisha mafuriko.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maandalizi ya mvua hizo, Mwenyekiti Nyamka amesema CCM Wilaya ya Kibaha Mjini imekutana na viongozi mbalimbali, wakiwemo wenyeviti wa serikali za mitaa na mabalozi, kwa lengo la kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
“Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) hivi karibuni ilitoa taarifa kuhusu mvua hizi kubwa za El-Nino. Sisi kama chama tukaona ni vema tukutane na viongozi wetu kuanzia ngazi za chini ili kupeana maelekezo na majukumu yanayopaswa kufanyika katika kipindi hiki,” amesema.
Amesema viongozi hao wamehimizwa kuwasisitiza wananchi kutotupa taka hovyo, kuzibua mitaro na kusafisha mifereji ili kuhakikisha maji ya mvua yanapita kwa urahisi na kupunguza uwezekano wa kutokea kwa mafuriko.
Mwenyekiti Nyamka amesema taarifa iliyotolewa na TMA imepokelewa kwa tahadhari kubwa na kwamba CCM pamoja na Halmashauri ya Mji wa Kibaha wamezingatia maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika ili kuhakikisha wananchi wanajiandaa mapema na kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
Aidha, amewataka wananchi kuacha tabia ya kutupa taka hovyo na kusisitiza kuwa watakaobainika kukiuka taratibu za usafi wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ili kuwa fundisho kwa wengine.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti Nyamka amezitaka mamlaka zinazohusika, ikiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kuhakikisha zinachukua hatua za mapema kukarabati madaraja na makalavati yaliyo katika hali hatarishi.
Amesema hatua hiyo ni muhimu hasa katika maeneo yanayokumbwa na changamoto wakati wa mvua, ikiwemo Kata za Muheza, Mwanalugali na maeneo mengine yenye changamoto ya miundombinu.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini, hali ambayo inawataka wananchi na mamlaka husika kuchukua hatua za mapema ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza, ikiwemo mafuriko.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...