WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili jijini Roma, Italia, leo Septemba 20, 2026, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health).

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Septemba 21 hadi 23, 2026, katika Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), jijini Roma.

Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Leonardo da Vinci (Fiumicino), Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amepokelewa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.

Mkutano huo unalenga kujadili masuala ya afya ya binadamu, wanyama na mazingira, pamoja na uhusiano wake na mifumo ya chakula na kilimo duniani.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...