Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Viongozi kuhusu Afya ya Mama na Mtoto uliofanyika jijini New York, Marekani.
Mkutano huo uliandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) na kufanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81).
Mkutano huo uliwakutanisha viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na viongozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wadau wa maendeleo, kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu afya ya mama na mtoto.
Miongoni mwa waliohudhuria ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC, Dkt. Jean Kaseya, pamoja na Mwenza wa Rais wa Benin, Bi. Nathalie Vilette Wadagni.
Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa taasisi na mashirika ya maendeleo, wakiwemo Gates Foundation, Global Fund, Gavi, UNFPA, UNICEF, Susan Thompson Buffett Foundation, Beginning Fund, pamoja na viongozi kutoka Umoja wa Afrika (AU).
Mkutano huo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na wa Afrika katika kuboresha afya ya mama na mtoto, hususan katika kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wanawake na watoto.


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)



.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...