ALGIERS: Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Viwanda vya Dawa wa Algeria, Dkt. Wassim Kouidri, katika ofisi za Wizara hiyo jijini Algiers, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo katika sekta ya viwanda vya dawa na vifaa tiba.
Mazungumzo hayo yamejikita katika namna ya kukuza ushirikiano wa kitaalamu na uwekezaji katika sekta hiyo, ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipa kipaumbele katika jitihada za kuongeza uzalishaji wa dawa nchini na kukidhi mahitaji ya soko la ndani pamoja na masoko ya ukanda wa Afrika.
Akizungumza katika mazungumzo hayo, Balozi Matinyi alimweleza Waziri Kouidri kuwa Serikali ya Tanzania imeweka vivutio maalum kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya viwanda vya dawa, huku viwanda vitano vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi na vingine zaidi vikitarajiwa kujengwa.
“Serikali imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha viwanda vya dawa na vifaa tiba katika ukanda wa nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika wenye watu takribani milioni 350,” alisema Balozi Matinyi.
Kwa upande wake, Waziri Kouidri aliahidi ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria kwa Tanzania, hususan katika eneo la utaalamu na teknolojia za kisasa za utengenezaji wa dawa na vifaa tiba.
“Ni kweli, Tanzania ipo kwenye eneo zuri la kimkakati la ukanda mkubwa wa Afrika na Algeria iko tayari kushirikiana nayo kitaalamu ili kuhakikisha inafikia malengo yake,” alisema Waziri Kouidri.
Aidha, Balozi Matinyi aliikaribisha nchini Algeria kupitia Mamlaka ya Taifa ya Bidhaa za Dawa (ANPP), ambayo inatarajiwa kuwasili Tanzania mwezi Oktoba mwaka huu kwa mwaliko wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA).
Ziara hiyo inatarajiwa kutoa fursa kwa mamlaka hizo kujadili na kuweka mikakati ya namna bora ya kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kitaalamu, ikiwemo udhibiti na uzalishaji wa dawa na vifaa tiba.
Tanzania inaheshimika barani Afrika katika eneo la udhibiti wa dawa, ikiwa ni nchi ya kwanza barani Afrika kufikia kiwango cha ML3 mwaka 2018 chini ya mfumo wa tathmini ya viwango vya udhibiti wa dawa (GBT) wa Shirika la Afya Duniani (WHO), unaopima ubora na ufanisi wa mifumo ya udhibiti wa dawa katika nchi.
Tangu mwaka 2020, nchi nyingine tisa za Afrika zimefikia kiwango hicho cha ML3, huku hakuna nchi barani Afrika ambayo imefikia kiwango cha juu zaidi cha ML4.
Nchi hizo ni Afrika Kusini, Ethiopia, Ghana, Misri, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Senegal na Zimbabwe.
Kwa upande mwingine, Algeria ni miongoni mwa nchi zinazoongoza barani Afrika katika sekta ya viwanda vya dawa na vifaa tiba, ikiwa na jumla ya viwanda 230, sawa na takribani theluthi moja ya viwanda 690 vya aina hiyo vilivyopo barani Afrika.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...