Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii nchini kwa kuendelea kuwekeza katika suluhisho za kifedha na kiteknolojia, ubia wa kimkakati pamoja na mipango ya uwajibikaji kwa jamii inayolenga kuunga mkono maendeleo ya sekta hiyo.

Dhamira hiyo ilisisitizwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NBC, Elvis Ndunguru, wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka kampuni na taasisi mbalimbali jijini Arusha.

Hafla hiyo, iliyowakutanisha viongozi na maofisa wa NBC pamoja na wawakilishi wa kampuni na taasisi mbalimbali, ililenga kuimarisha uhusiano kati ya benki na wateja wake, kubadilishana mawazo kuhusu fursa za biashara, kutambulisha huduma na suluhisho mpya za kifedha, pamoja na kupata mrejesho kuhusu namna NBC inavyoweza kuendelea kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji ya wateja.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara ya benki hiyo (CIB), Ndunguru alisema matukio kama hayo ni sehemu ya mkakati wa benki wa kuwa karibu na wateja wake, kuwaeleza maendeleo katika huduma za kifedha na kidigitali, pamoja na kuunda mazingira yanayowezesha wateja kubadilishana taarifa na fursa za biashara.

“Tukiwa kama mhimili muhimu wa utoaji wa huduma za kifedha nchini, NBC tunatambua umuhimu wa kutoa huduma bora na kujenga ushirikiano wa karibu na wateja wetu. Mabadiliko ya kiteknolojia na ubunifu yanaendelea kubadili mahitaji ya wateja, hivyo tunahitaji kuendelea kubuni na kuboresha huduma zetu ili ziendane na mazingira hayo,” alisema Ndunguru.

Alitaja baadhi ya maeneo ambayo NBC imeendelea kuboresha kupitia teknolojia kuwa ni mifumo ya ukusanyaji wa mapato na malipo ya serikali, ikiwemo GePG na MUSE, pamoja na suluhisho za ukusanyaji wa malipo kwa taasisi mbalimbali, zikiwemo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Ndunguru alisema Arusha ni mkoa wa kimkakati kwa NBC, kutokana na nafasi yake katika uchumi wa utalii nchini, huku akieleza kuwa benki hiyo itaendelea kutafuta fursa za kuunga mkono uwekezaji katika utalii pamoja na sekta nyingine muhimu za uchumi kama kilimo na ufugaji.

“Arusha ni mkoa wa kimkakati katika utekelezaji wa agenda yetu ya kuhudumia sekta ya utalii. Tutaendelea kuboresha na kuwekeza katika fursa mbalimbali, hususan katika maeneo ya utalii, sambamba na sekta nyingine zenye mchango mkubwa katika uchumi kama kilimo na ufugaji,” alisema.

Aidha, Ndunguru alisema NBC inaendelea kutumia matukio kama hayo kujenga mitandao ya kibiashara miongoni mwa wateja wake, huku huduma za kidigitali kama NBC Connect zikitumika kama sehemu ya suluhisho zinazolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa kampuni, mashirika na taasisi za serikali.

“Tunaamini kuwa msingi wa huduma za kipekee ni kuelewa mahitaji na matarajio ya wateja wetu. Matukio kama haya yanatupatia mitazamo na mrejesho unaotusaidia kuwa wabunifu zaidi na kuendelea kuboresha uzoefu wa wateja wetu katika huduma za kibenki,” aliongeza Ndunguru.

Kwa upande wake, Meneja wa NBC Tawi la Arusha, Mukiza Aggrey Mboneko, alisema NBC inaendelea kutoa huduma mbalimbali zinazolenga kukidhi mahitaji ya wawekezaji na wafanyabiashara katika sekta ya utalii.

Alisema huduma hizo zinajumuisha mikopo kwa ajili ya ununuzi wa magari ya kubebea watalii, ujenzi na uendelezaji wa kambi za utalii (camps), lodges na hoteli, pamoja na mitaji ya biashara kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao ndani ya mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii.

“Pia tuna mifumo ya malipo iliyounganishwa na TANAPA na Ngorongoro, inayowawezesha wadau kufanya malipo mbalimbali, ikiwemo ada za hifadhi (park fees), kwa urahisi zaidi,” alisema Mboneko.

Aliwaalika wafanyabiashara na taasisi mbalimbali jijini Arusha kutumia fursa zilizopo kushirikiana na NBC, akisema benki hiyo itaendelea kutoa suluhisho na zana za kifedha zinazolenga kusaidia biashara kukua na kuimarisha ufanisi wa shughuli zao.

Baadhi ya wateja wa NBC waliohudhuria hafla hiyo walisema majadiliano hayo yamekuja wakati muhimu, wakati Arusha ikiendelea kushuhudia shughuli kubwa za kiuchumi zinazochochewa na ukuaji wa sekta ya utalii pamoja na biashara, kilimo na viwanda.

Miongoni mwao ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Ernest Mjingo, ambaye alisema huduma za kisasa za kifedha, hususan mifumo ya kidigitali, zimeendelea kuwa muhimu kwa taasisi na wafanyabiashara katika kurahisisha miamala na ukusanyaji wa mapato.

“Kwa sasa Arusha iko katika kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi yanayochagizwa na ukuaji wa utalii, biashara, kilimo na viwanda. Ni jambo zuri kuona NBC, ambayo inahudumia wadau wengi katika sekta hizi, ikiendelea kuwaunga mkono kupitia huduma za kisasa, ikiwemo huduma za kidigitali ambazo zimekuwa msaada mkubwa katika kurahisisha miamala ya kifedha na ukusanyaji wa mapato ya serikali,” alisema Dkt. Mjingo.

Mbali na huduma zinazolenga taasisi na biashara, Dkt. Mjingo pia alieleza kuvutiwa na huduma zinazotolewa na NBC kwa wastaafu, akisema huduma hizo zinampa matumaini ya kuendelea kuwa na uhusiano mzuri na taasisi za kifedha hata baada ya kustaafu

Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (pichani) akizungumza na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.






Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru (wa tatu kushoto - waliosimama) akisalimiana na baadhi ya wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Baadhi ya wateja wa benki ya NBC jijini Arusha wakifuatilia hafla hiyo



Hafla hiyo, iliyowakutanisha viongozi na maofisa wa NBC pamoja na wawakilishi wa kampuni na taasisi mbalimbali, ililenga kuimarisha uhusiano kati ya benki na wateja wake, kubadilishana mawazo kuhusu fursa za biashara, kutambulisha huduma na suluhisho mpya za kifedha, pamoja na kupata mrejesho kuhusu namna NBC inavyoweza kuendelea kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji ya wateja.

Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw, Elvis Ndunguru sambamba na maofisa wengie wa benki hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki hiyo jijini Arusha wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kutoka makampuni, wateja binafsi na taasisi mbali mbali (Corporates) ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Hafla hiyo iliyoandaliwa kupitia timu ya Biashara na Uwekezaji (CIB) ya benki hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...