Wajawazito wanaohudumiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi, wanatarajiwa kunufaika na vifaa vya uchunguzi na kujifungulia vilivyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Yas Tanzania kupitia Kampeni yake ya ‘Tumaini’.
Msaada huo unajumuisha kitanda cha uchunguzi kwa wajawazito, kiti mwendo, mashuka, trei za kujifungulia (delivery tray) na khanga. Vifaa hivyo ni sehemu ya nyenzo muhimu zinazotumiwa na madaktari na wauguzi katika kutoa huduma kwa akina mama wajawazito hususan wakati wa kujifungua.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Dkt. Hadija Said Kitiku, alisema mahitaji ya vifaa vya uzazi ni miongoni mwa vifaa muhimu vinavyohitajika katika hospitali hiyo, na kwamba msaada uliotolewa utawasaidia wahudumu wa afya kuboresha huduma kwa wajawazito.
“Tunapokuwa na vifaa vya kutosha, madaktari na wauguzi wanakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya uchunguzi na kuwahudumia kwa ufanisi akina mama wakati wa kujifungua. Kitanda cha uchunguzi, kiti mwendo na trei tulizopokea ni vifaa muhimu sana ambavyo tunavihitaji katika kazi zetu za kila siku. Tunaishukuru Yas na wafanyakazi wake kwa kuja na wazo hili la kibunifu ili kuleta manufaa kwa jamii,” alisema Dkt. Kitiku.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Yas Kanda ya Pwani Kusini, Bw. Erick Munaku alisema Kampeni ya Tumaini ilitokana na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuguswa na changamoto zinazowakabili baadhi ya akina mama wakati wa ujauzito na kujifungua.
“Tumaini ilianza na sisi wafanyakazi kujiuliza tunaweza kufanya nini kusaidia mama anayekwenda kujifungua. Tukaona ni vyema kuchangia vifaa vinavyomgusa mama mjamzito kwa kutambua changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo hususan wakati wa kujifungua. Leo tumefika Liwale kutekeleza wazo hilo, tukiamini kuwa mchango wetu unaweza kumsaidia mama na mhudumu anayemhudumia,” alisema Munaku
Munaku aliongeza kuwa kupitia kampeni hiyo, wafanyakazi wa Yas wanashirikiana na taasisi za afya katika maeneo mbalimbali ya nchi kubaini mahitaji na kuchangia vifaa hivyo kwa ajili ya kusaidia suala la uzazi.
Aliwashukuru madaktari, wauguzi na watoa huduma wengine wa hospitali hiyo kwa kazi wanayofanya, akisema msaada huo unaunga mkono juhudi licha ya kumgusa mama na mtoto.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...