Piga ua bila hawa, pamoja na mapungufu yao (ya kibinaadamu), wengine msingekuwa mnatanua huko ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Michuzi umetoka mbali kwelikweli yaani hata hii picha uliipiga wewe! Kweli wewe kiboko.

    Pili katika picha hii naweza ku-guess kumuona Haile Selasie, Milton Obote, Julius na Kenyatta. Sijui nimepatia au nimenoa. Otherwise Michuzi hebu wabandike majina tupate kuwafehemu.

    ReplyDelete
  2. Duh!Lakini katikati nyuma(Center back) mbona naona kuna mtu kafanana na michuzi mwenyewe!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. kaka michuzi,

    kuna kitu kimoja inabidi tukiweke wazi hapa. ni kweli kuwa hao ndio waliwekwa kichwa katika kuwakilisha mawazo na maoni ya watanganyika wenzao katika kudai uhuru! hapa ninasisitiza kuwa SIO KWELI KUWA KAMA SIO NYERERE NA KAWAWA TUSINGEKUWA HURU NA TAIFA KAMA TULIVYO LEO! walikuwapo kina kambona walikuwapo kina mtei, walikuwapo weeeeeeeeeeeeeennnngiiiiiiiii tuuuuuuuuuuu!! walikuwapo baba na mama yangu!!!dhana hii iliendelea kuwepo hadi leo watu walidhani bila msekwa bunge lisingeenda, walidhani bila nyerere uraisi ndio basi tena.......bila CCM amani itatoweka na haitatawalika sio kweli! ni dhamana tu ambayo mtu anapewa na umma! mbona baba yake mheshimiwa Mbowe hayuko hapo kwenye picha lakini alimfadhili mwalimu kwenye pita pita zake? mbona wale wazee wa Tabora hawapo? mbona chifu Kingalu WA waluguru hayupo? hiyo kamera ingeweza kuchukua watu milino kadhaa??au watu milioni kadhaa wakasaini uhuru??? mbona??? mbona???mbona???? NINACHOSISITIZA HAPA NI KUWA TANZANIA NI YETU WOTE NA HAKUNA MTU ATADAI ANA COPYRIGHT YA KUTAWALA !

    aksante kwa picha zinazozua mijadala!!

    ReplyDelete
  4. Hawa wote walikipata chamoto ughaibuni - ikimuondoa Bw. Joseph Mobutu na Mzee Selasie. Kenyata na Nkrumah ndio walikipata haswa. kutanua ughaibuni... sijui! Labda matanuzi ya rejareja. Mtu kwao michuzi!

    ReplyDelete
  5. Ughaibuni hakuna kutanua jamani.Nani kasema huku tunatanua?Kumbeee....ndio maana.

    ReplyDelete
  6. waambie kaka jeff! nilogopa kuzua mjadala!

    cheers

    ReplyDelete
  7. Hao jamaa walikuwa na personal identity kama bakora, vitambaa, kofia, aina ya uchanaji wa nywele ....... lakini hawa wa siku hizi identity zao ni aina ya mikufu na mapete makuuubwa wanayovaa....... tubandkie majina ndugu yangu.

    ReplyDelete
  8. kaka michuzi mapungufu yao ni ya kibinadamu...na jitihada zao ni za ki nini?

    ReplyDelete
  9. mark msaki..nadhani ungezaliwa mwaka 22 ungeweza pia kuongoza nchi...nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.hizi dhana kuwa bila nyerere ooh bila nyerere kusingekuwa hivi kusingekuwa vile kunafanya vizazi vya sasa vijisikie havithaminiki.msaki anaelezea vizuri na lazima ielewe kuwa bila mkapa basi angekuwepo rais mwingine na bila nyerere basi may be mtemvu au fundikira wangesimamia nchi.kumbuka kuwa nyerere alichukuliwa pugu na wazee waliokuwa wanaendeleza haraki za uhuru,wakamvua kamptula wakamvalisha suruali,na wale ndio waliomuweka jukwaani.asingekuwepo yeye hiyo kazi ingefanywa na mtu mwingine.au michuzi unataka kutuambia kuwa bila wewe tusingeona picha za matukio bongo???????????????????
    cheers kaka!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 16, 2006

    Nyie akina Mark acheni hizo, wapeni sifa zao hao wanaostahili. Nyerere, Samora, Kenyatta, Kaunda, Kawawa walikuwa na vipaji na courage ambavyo wengi wetu hata leo bado hatuna. Unafikiri ni rahisi watu kujitolea maisha yao kwa ajili ya wananchi wenzao? sina maana hawakuwepo watu waliokuwa wakiwasiadia akina Nyerere.

    Ukianza kuleta mambo ya walikuwepo akina Kambona, sijui akina Mtei je nini kiliwazuia wao kuwa ma Rais? lazima mkubaliane kwamba kuna roles ambazo watu wanatakiwa kuplay akina mtei wliplay role zao na akina Nyerere wao walikuwa marais na wakizeshepu nchi zao jinsi zilivyo leo. It is as simple as that!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...