Rais mpya wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa nchi mbalimbali na marais wastaafu wa Tanzania na Kenya Ikulu leo 21/12/05

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Jicho langu limetua kwa Kiboko yake Blair.

    ReplyDelete
  2. Hivi hao marais wengine vinganganizi wa madaraka hawaoni aibu kupozi kwenye picha hii!?

    ReplyDelete
  3. Na huyo aliyevaa suti nyeupe ambayo haijamkaa sawasawa ni Moi?

    ReplyDelete
  4. Ni Mzee Moi umepatia baba/mama, 'profesa wa siasa' kule Kenya. Kuna haja ya kundi la kina Museveni kuwaigizia akina Mkapa, Mwinyi na Moi (ingawaje naye 'alikaako' madarakani sana).

    Michuzi unaona tupicha twako tunavyoleta mjadala wa heri?

    NB:'alikaako' ni Kiswahili kilichojeruhiwa na Kinyakyusa kidogo. Muulizeni Michuzi.

    ReplyDelete
  5. mkapa na mwinyi kumbe kimo chao sawa! Moi mrefu kupita wote.
    Ningefurahi wangetafuta mshonaji mwingine, kama wa mandela, suti haziwafai, wawe original

    ReplyDelete
  6. Mugabe kidume, mwone alivyosimama, hatishiki Mbeki anasoma hali ya hewa, habadiliki kwa alichoona. museveni anafikiria kama Mkapa anamawazo gani kukubali kuondoka......

    ReplyDelete
  7. it would be nice if we named everyone in the photo (from L to R)... I now live in Canada and have left Tanzania 11 years ago (although, I still go there every 4 years to see amazing developments there).

    I know the frontliners (our 3 presidents and kenya and Uganda), and also know Mbeki... but the rest at the back are not known as much...

    thanks michuzi... bring as many pics as you can... infact create a portfolio online at http://www.portfoliocity.com/

    ReplyDelete
  8. Mloy hujamaliza bwana, endelea kututolea ufafanuzi maana kweli ukiwaangalia hawa viongozi kuna mengi yanayojieleza nyusoni mwao, ...Labda nikusaidie mmoja, Kibaki limemshuka amesimama tu ila hana jinsi....haya mpira ni wako bwana Mloy endelea na safu ya nyuma.

    ReplyDelete
  9. katika hao waheshimiwa kuna wawili ambao hawakustahili kuwepo. ni mugabe na museveni! nimesoma pale nadhani ni kwenye the nations jinsi museveni alivyomwaga mabilioni ya us dollars kulipa wahamasishaji wa kama ilivyokuwa nyumbani mabalozi kufuatilia wapiga kura kwa kuangalia kadi zao na misimamo yao. nina wasiwasi hii itafanya majina ya wengi yasitokee kwenye orodha ya wapiga kura. naona hilo alijifunza kwetu. huyu kidume mugabe naye nilisoma hotuba yake kwa kiasi kikubwa ilikuwa inamsihi kikwete aendeleze ukanda wa kumsapoti kifedha na kihotuba kama kaka yake ben - kwa taarifa ni ben peke yake ndie kiongozi aliyekuwa anamuunga mkono mugabe hadharani akiacha wengi wakimshangaa. ushauri wa bure kwa kikwete, huyo mugabe achana naye. fedah ukimpa ni za kula mwenyewe wakati amewafanya wazimbabwe wengi sana wateseke na mamilioni kuwa wakimbizi. pia atakuchafulia reputation yake mbele ya uso wa kimataifa. wewe jenga uchumi wa Tz, hizp zambi zake acha zimuhukumu mwenyewe!

    ReplyDelete
  10. Nini lakini Mark? mbona hivi?..hapana tena nasema hapana...TAFADHALI ANDIKA VIZURI.

    ReplyDelete
  11. Maximum respect to you brother MARK!Nami nafikiri fursa kama hiyo michuzi angepaswa kwa ujasiri kudodosa siri ya hao waheshimiwa wawili museveni na mugabe kutaka kuendelea kubaki kitini.

    Michuzi hili una nafasi ya kulikemea kwani mbegu za aina hiyo zimeanzwa kupandwa Tanzania.Si unaona mambo anayotaka kuleta bau yetu msekwa?

    ALUTA CONTINUE.

    ReplyDelete
  12. The Presidents with their countries are from left front row Kibaki (kenya), Mugabe (Zimbabwe), Moi (retired Kenya) Mkapa (retired Tanzania), Kikwete (Tanzania, incumbent), Mwinyi (Tanzania, retired), Museveni (Uganda). Back row Bingu wa Mutharika (Malawi) Pierre Nkurunzinza (Burundi), Festus Moghae (Botswana), Armando Guebuza (Mozambique), lEVY Mwanawasa (Zambia), Zinawe (Ethiopia), Thabo Mbeki (SA), Kagame (Rwanda), Umar Hassan Ahmad al-BAshir (Sudan), Joseph Kabila (DRC)and King Letsie III (Lesotho)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...