Mwimbaji Muumini Mwinjuma amezindua upya bendi yake ya Double M baada ya kufa kwa Double Extra aloianzisha na Ali Choki ambaye yuko Mchinga Sound band. Hapo Muumini (wa mbele) akiwa na bendi yake aloizindua upya mkesha wa mwaka mpya. hapo ni msasani club, kuelekea msasani kwa mwalimu, dar (kwa mlioondoka bongo looooong time)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. sawa sasa kazi na ianze, ukipata muda owasogelee kwa karibu uwapige picha na hao mademu wa shoka. nadhani da mija atawapenda sana!

    ReplyDelete
  2. Umesema kweli Mark. Lakini nafikiri na wewe ulitamani uwaone kwa ukaribu zaidi...unasemaje?

    ReplyDelete
  3. Michuzi,
    Mimi bado nina tatizo moja na hizi bendi za kwetu.Ni kuhusu mavazi yao tu!Hivi ni kwanini wasitinge viwalo vya kiafrika wakautangaza utamaduni wetu wa mavazi?Kuna haja gani ya hao kina dada kuvaa viatu vya majira ya baridi kali wakati Bongo nasikia joto limezidi vibaya sana?Nina tatizo sana na hali hii.

    ReplyDelete
  4. Jeff: viatu vya majira ya baridi ndani ya bongo sio? Umemsoma Chemi? Anaongelea wanawake wa Kiafrika wanavyotumia vipodozi vilivyotengenezwa kwa ajili ya ngozi nyeupe.

    Lakini kali ni Mark...Da Mija nakubaliana nawe. Mark alitaka kupiga jicho kwa karibu. Unataka anuani?????

    ReplyDelete
  5. aha no ndesanjo, nilikuwa nataka niangalie lebo ya viwalo walivyotinga. ila nilikuwa namfagilia de mija kimtindo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...