kumbe wanablogu nanyi mmo!
kwenye maktaba yangu nimekuta picha hii ya kihistoria. kutoka kushoto ni Abdallah Ezza (mpwawe Gema aliyekuwa mpiga gitaa wa Afrosa), katikati ni Hayati Patrick Pama Balisidya, na mwisho ni F MtiMkubwa Tungaraza. Picha ilipigwa mjini Helsinki wakati Marehemu alipoenda kushiriki katika tamasha la Etnosoi mwaka 1993.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Bila blogu hizi picha tungeziona wapi? Safi kama Michuzi.

    ReplyDelete
  2. Brother Michuzi tunashukuru sana kwa kutuletea burudani hizi. Hii ni changamoto kwa wapigapicha wetu wa Kibongo, kuwa habari zinatengezwa na wasomaji sio wanakazania picha za viongozi wakila kuku kwa mikono kwenye mahoteli makubwa au wakiingia kwenye state dinner na designer suit.
    TAMASHA JEMA,
    Dennis- Denmark

    ReplyDelete
  3. Unaona Bwana, siku zote mii nasikia tu Mtimkubwa Mtimkubwa!! kumbe ni huyu swahiba wangu wa zamani sana. Siku hizo tulikuwa tunamwita "Sujaroro" huyu Bwana alikuwa burudani ya pekee na ni furaha kwamba yumo humu.
    Fadhil

    ReplyDelete
  4. Abdallah Ezza yuko wapi sasa?

    ReplyDelete
  5. ezza yuko helsinki, yeye ni alwatan wa jiji pia ni rizevu wa Bongo FC. ni vigumu kwa mtanzania yoyote anayepita helsinki kutomuona ezza, kwa bahati mbaya naona hamkukutana.

    ReplyDelete
  6. Asante Mti kwa taarifa. Nikija tena lazima nikutane naye.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...