
haka ndo kachumba ka habari ka deliniuzi nnakosotea waya mie. nimekaweka makusudi kwani naomba mnisaidie mawazo. hivi sasa kazi ya ajira bomba na mshiko si mbaya. tatizo biashara nayo imechanganya na ili iendelee kumea yahitaji muda wangu wote. niko njia panda. nijimwaye kwenye sekta binfasi ama niendelee na jobu la ajira? naomba msaada jamani. niko njia panda
Ukiondoa vile viti viwili vya baa, delinuzi ni pazuri
ReplyDeleteHii inashiria nini wanablog wenzangu!!!!
ReplyDeleteKwangu mimi naona kama wafanyakazi wa hapo ni wavivu sana,yaani hata mtu mmoja ofisini wa kuzuga hakuna!!!!!Au unataka kutuambia uliipiga wakati gani bwana michuzi????
Jee huko ndo kuupiga umaskini vita kwa ari mpya,kasi mpya na nguvu mpya??????
habari yakhe yatafutwa mtaani na hizo meza tupu ni za waandishi sio ma-mangi meza. nilipiga saa tano asubui jumapili ilopita
ReplyDeleteTumekuzoea kwa kujitetea!!!!!
ReplyDeleteIna maana wote mnaenda field????
nasema hivi, hiyo ni seksheni ya waandishi. wahariri ni kwingine, na waendao fildi ni waandishi. maswaaaali?
ReplyDeleteMichuzi hivi hivi ulitutishaga kuacha Blogu sasa unakimbilia kwenye maswali ya kazi. Wewe acha hiyo kazi uone wanao watakavyoandamana kwa JK? Mimi simo naomba kikombe chako kiniepuke lakini kama wataka sana kuwekwa chini na JK na kuanzwa kuhojiwa kutumiwa na wapinzani acha hiyo kazi hapo bila baraka za hao wafalme wa Tanzania!
ReplyDeletembona kompyuta zimezima? au ndio mgao mkali wa umeme umefika hapo? jj
ReplyDeleteBwana Michuzi mimi ninakushauri ya kwamba uendelee kufanya kazi hapo ulipo tu kama unapata yale malengo yako.
ReplyDeleteNasema hivyo kutokana ya kwamba watu wanabakiaga kufanya kazi sehemu moja kama wanatimiziwa matakwa (needs) yao na mwajili husika.
Hii ni kujumuisha Mishahara mizuri pamoja na malupulupu mengine, Jinsi ya mwajili anavyo mchukulia mwajiliwa (company policies,rules), Jinsi ya vyeo vinavyotolewa maana wengine hawawezi kukaa sehemu moja miaka mitano bila ya kupandishwa vyeo, au wamechoshwa na kazi (Job Dissatisfaction).
Kama unaona kazi ni nzuri kutokana na needs zako zinatimiziwa bora uendelee kufanya kazi.Kama unaona umeichoka tafuta ile itakayo timiza mahitaji yako.
Kingine husiache kazi kabla ujapata kazi maana kuna vijana wengi ambao wapo mitahani hawana kazi na wameitimu elimu zao(yaani kuna ukilitimba ktk kupata kazi).
Nakutakia maamuzi mema yenye busara.
Nashukuru.
Michuzi,
ReplyDeleteKwanza ahsante sana kwa maoni uliyoweka kwenye blogu yangu.Nayafanyia kazi.
Kuhusu swali lako.Mimi nakushauri usiache kazi bali pia uendelee kufanya shughuli zako binafsi.Nadhani hata mwajiri wako hatokuwa na tatizo na hilo kwani ulimwengu wa sasa unaenda kwa mwendo huu.Kisha ukiona biashara binafsi imekomaa au muda wa kutekeleza vyote unakuwa haba basi unaweza kuachana na ajira ya serikalini na kusimamia zaidi ya kwako.Kwa uzoefu wako na ufanisi wako nina uhakika hata serikali itaendelea kuwa mmoja wa wateja wako.Uhuru wa kujiajiri ndio mwanzo wa mafanikio.Naomba email yako Michuzi,kuna jambo nataka tutete.
naiomba email address yako bw Michuzi. Ahsante
ReplyDeletesumz81
Mwandishi anatakiwa akatafute kazi mtaani (kuitaviuu watu, presi rilizi nk).
ReplyDeleteHao wanaotaka waandishi wawepo ndani ndio wale waliozoea habari za kudownload mtandaoni. Na siku hizi magazeti mengi ndio dili zao hizi. Hatuyasemi tunaogopa-ga mkong'oto.
Daily Noise mnatuonyesha ni jinsi gani mnang'anga'nia maadili ya uandishi wa habari. Heko.
nimehemewa kwa majibu yote. nikianza na reginald, viti vile ni vya wageni na ni masalia ya samani za zamani. asante kwa sifa. anony nashukuru kwa onyo nisiacha kazi kama sitaki laana ya jk & kampani. we anony mwingine ni kwamba kompyuta zimezimwa kwa kuwa hakuna mtu anayetumia. nadhani huna mtindio wa macho. bw mk nawe asante kwa ushauri, ingawa nasisitiza kuwa niko njia panda, kwani pande zote zanifaa, na kila moja yajitegemea kwa hilo. yaani sipati kazi za nje kwa kuwa paparazi, zinakuja kwa kuwa mimi ni mimi, tofauti na nilipoanza uandishi, na upande wa pili kadhalika. hakika jeff kaka umenikuna, kwani naona wewe umesema kama mtu asiye na woga wa kuoga maji baridi. email yangu ni issamichuzi@gmail.com. nasubiri waraka kwa hamu toka kwako pia kaka/dada sumz8i. jmwipopo pia asante kwa heko na kwa kunitembelea-ga mara kwa mara. ila nina kiu kupata mawazo ya ndesanjo, damija, markmsaki, baragumu, mtimkubwa na washakji wengine.
ReplyDeleteMichuzi, ninaungana na kaka Jeff kwa asilimia 100 %. najua sera ya kazi haikuzuii kuwa na shughuli nyengine pembeni.
ReplyDeletemara nyingi kuna mtingishiko unaweza kuupata unapocross line. mtingishiko huu unapaswa kutafakariwa kwa makini kwanza. kwani hautakuhusu wewe tu, bali hala wale malaika uliotuwekea picha zao juzi! wachilia mbali wale shemeji zako unaowalipia ada. hivyo huhitaji maamuzi makini. mara nyingi utaona ukifika hapa washauri hukaa kimya. inabidi utafiti vitu vifuatavyo!
1. Shughuli zako za binafsi pengine unaona zinakuingizia kwa sababu ya network uliyonayo sasa hivi (kuwepo daili nuzi). inawezekana mtandao wako bado haujakomaa kufikia kiwango cha kusimama mwenyewe na kukidhi kila chako!
2. mara nyingi nimeshuhudia shughuli binafsi za watu wengi waliokuwa mwanzo kama wewe huwa hazijiendeshi kibiashara (hubebwa na ofisi uliyoajiriwa)..yaani mfano utawalipa vijana kutokana na mshahara wako. ukiacha kazi unakuwa umeumbuka!
3. kuchukua risk pia kumesemwa kuwa ni siri ya waliofanikiwa. hata hivyo ni vizuri kujitahidi kupunguza uwezekano wa risk hiyo kutokea na ukubwa wake hata ikitokea (mfano, je nini kitanihakikishia nauli? je nina uhakika wa chakula? bili ya nyumba?). mara nyingi ndio maana watu huweka mitego huku na kule na kuwa na vitega uchumi kadhaa vya kukufanya usiumbuke!
4. Kwa kuwa basi umeamua kuwa mtu wa kisasa, ili kukabiliana na risk hiyo kuna mambo kadhaa ya kufanya (kuwa mtu wa kisasa ni gharama sana na ndio maana mie huwaga ninasemaga kujua sana kunatufanya tuishi maisha mafupi - maana ukijua sana unataka sana)
a. Ifanyie utafiti biashara yako, ulipoanza, na inavyokuwa, mapato faida na hasara! inavyoyumba labda kwa kipindi cha mwaka mzima...(biashara nyengine hufanya kazi miezi mitatu tu ya mwaka na kulipa kwa ajili ya mwaka mzima).
b.kwa hali ya bongo, ni vyema pia ukawa na (vengine vidogo dogo vya kuingiza za kula na pango - kujishikiza), usidharau hata vioski vya magazeti! Sio lazima ufanye ile proffesion peke yake.
c. Ajiri mtu / watu kutokana na mahitaji ya biashara. (hapa ndio pagumu)lakini panahitaji usimamizi. inabidi uwe na nidhamu kama wahindi kukagua vitabu vyako mara kwa mara. kama kuna upungufu utauona hata baada ya wiki.....unapohitajika na wewe nadhani hakuna atayekuzuia.... Bibie kama yuko fresha anaweza akakusaidia kwenye hiki kitengo!!
hivyo kama biashara inakuwa, basi ujue umeishakuwa mmoja wa "Proudly Tanzanian" kwani teyari utakuwa unaendelea kukuza soko la ajira!! mahusiano mazuri kati yako na waajiriwa wako ni jambo la msingi sana sana na ukifanikiwa hili eneo tu basi umeula wa Ipinda!! unanukiaaaaa!!!!!!!! kuna sayansi yake, wajue kuwa mafanikio yako ni ya kwao, na iwe hivyo, uwajali...mwenyewe utashangaa!!
huko kwenye mradi wako, usitupe hela zote mara moja hata kama unazo, zipeleke kidogo kidogo ili uzidi kukua wenyewe taratibu badala ya kukufrustrate!
kama shughuli inalipa fikiria kuwa na patnership ya wakurugenzi na watu wengine ambao wanaweza kuwa na mchango kwa namna au nyengine (wanawekeza halafu mnakula dividends baadaye au mnazizungusha faida zenu - ni nyie wenyewe)
nakushauri kuwa huna haja ya kukimbilia kuacha kazi!! nimeona watu wengi tu tena hapo dar na wana biashara tena kubwa tu (na ni wafanyakazi wa serekali) wanazikurugenzi na kukutana labda mara 1 kwa wiki kujadiliana. kila mtu huwa anapewa jambo lake la kusimamia, wakikutana wanapeana taarifa na kushauriana pa kuelekea! sijui umenipata? inakuwa sasa ni wewe mwenyewe wakati wa kunch unafuatilia, au jioni baada ya kazi, au weekend!! siku hizi kuna simu, na mtandao ndio mambo ya ajira binafsi na madhali umeamua kuwa mtu wa kisasa!! wasikudanganye mtu kuwa eti ukianza kusakanya mwenyewe mtaa hadi mtaa ndio biashara itakwenda...sana sana wataanza kukupa appointment na kudisappear!!watacheza na muda wako...
ni hayo tu kwa leo! karibu sana msaki.mark@gmail.com
Nafikiri tulishaongelea hili swala mida ya nyuma kidogo. Nafikiri kutokana na ulichoniambia kwa kweli umefika muda wa ku-sink or swim. Mzee inabidi upige mbizi kama maji kweli yamekuwa shwari. All good things come to an end. Delinyuzi nayo inabidi ufunge chapter na ufungue chapter nyingine. Kumbuka mwanafalsafa Machiavelli alisema bahati inawajia wenye ujasiri. Mzee labda muda wa kujitosa umefika.
ReplyDeleteMichuzi baragumu jo jujo Mwaipopo.
ReplyDeletendaga nkamu mwaipopo. ngamenyeko... ukiwisa ndili kukaja? mma, kuli kununu linga uli na mahala. lwako, une ndi na ndalama nyingi naloli, linga uli mu sukulu, po mmma. utugalege kokuko. linga umalisye, isaga kukaja. mambo manunu...
ReplyDelete(samahani wengine kwa kwenda idhaa ingine. ni ujumbe muhimu kwa mwaipopo)
Michuzi kwani unafikiria biashara gani?naomba tuwasiliane kwa email ambayo ni tale562@hotmail.com
ReplyDeleteMichuzi, umenifurahisha sana hapo ulipokwenda idhaa nyingine. Idhaa nyingine hizo nazo ni muhimu sana. Nimeamka leo kupitia blogu kwa nguvu.
ReplyDeleteKuhusu swali lako. Wako wanaosema kuwa unapokuwa njia panda, hujui ufanye hili au lile, jibu lake ni kufanya yote.
Kwani huwezi fanya yote? Nadhani kote kuna faida zake na sekta zote zinahitaji watu wenye ujuzi na mawazo kama yako.
michuzi acha kazi tu, wengine nao wajaribu bahati zao. unapendelea sana, hata hapa inaonyesha unavyompendelea mwaipopo kwa sababu huwa yeye anacheka tu.
ReplyDeleteJitokeze basi ili nawe upendelewe.
ReplyDeleteGawe.
Anonimasi umekosea ungeandika-ga "anacheka-ga"
ReplyDeleteMaendeleo basi! Nakumbuka enzi zile za kugombania TYPEWRITER!
ReplyDeleteMgeni anakuja Newsroom anakuta waandishi wanashikana masharti kisa kila mtu anataka kutumia typerwiter!
Hey Michuzi, Jimwaye kwenye sekta binafsi.!...Italipa.
ReplyDeleteMichuzi kupanga ni kuchagua,watu wote waliofika waliko wengi wao wametumia nafasi walizo nazo kuwafikisha hapo.Kwa mtazamo wangu binafsi nafikiri bado unaouwezo wakufanya mambo haya mazuri na bado ukawa hapo daily news.Kumbuka
ReplyDeleteinawezekana baadhi ya mafaniko au upenyo unaoupata sehemu mbalimbali ni kwa hiyo nafasi uliyo nayo daily news.Kunaubaya gani wa kupiga ndege wawili kwa jiwe moja?
hivyo basi,kama siyo kwamba kazi inakuwea nzito katika hiyo sekta binafsi nakushauri piga ndege wawili kwa jiwe moja.La sivyo kama daily news inakufanya ushindwe kutimiza malengo yako basi chako ni chako.Huo ndo ushauri wangu ndugu yangu Muhidini.
Hi,
ReplyDeleteI found your blog on accident. I was looking online for the word "kachumba" to find out what it means.
My father sometimes calls me Kachumba, so I tried to find out if it means anything anywhere or whether he just made up the name.
Then I found your blog. It looks interesting from the pictures. I would like to read it, but don't even know what language it is!
I am from San Francisco, California, in the United States.
I am a singer and composer.
Nice to meet you! Hope you can read this!
:) michelle