walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi wakiingia kwenye karandinga kufuatia salaam kwa igp mwema zilizotolewa leo na jamaa waliovamia standard chatered bank na kuingia kizani na 300m/- za kampuni ya shivacom kabla hawajakabidhi benki. walinzi 12 wamechukuliwa kuhojiwa na inasemekana jamaa watano, mmoja demu, walihusika na tukio hilo lililokuja masaa 48 tu tangia igp mwema aapishwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. You wait. Atawaonyesha 'wema' wake soon.

    ReplyDelete
  2. kweli sasa Tanzania usalama hakuna! maana wezi wenye uwezo wa kuiba bank, wanaweza kuiba nyumbani kwa mtu yeyote yule,,,, "danger zone" jj

    ReplyDelete
  3. wezi wa bank wako kila nchi, wiki iliyopita majambazi huku UK walipora bank pound 23 million. Kwa hiyo mimi sishangai chochote kile sasa hivi.

    ReplyDelete
  4. polisi watakula sahani moja na walinzi wa kampuni binafsi wakati wezi wenyewe hawapatikani

    ReplyDelete
  5. Sasa inabidi waachane na walinzi waanze kuwashughulikia wakuu wa makampuni wanaopeleka fedha zao benki bila ulinzi imara.

    ReplyDelete
  6. kweli wezi wako kila pahali, ila jamani bongo wamezidi, kaa mchezo kila wiki. sasa itabidi wakaombe ushauri kwa mbwana mrema"awape siku saba wezi wote"jj

    ReplyDelete
  7. Kwanza kabisa naomba nimlekebishe jamaa hapo juu ni kwamba Tarehe 22nd February 2006 majambazi yalipora pounds Million 53 ktk ghara la kampuni binafsi (Securitas depot) inayo ifazi pesa za makampuni mengine.

    Lakini kutokana na wenzetu walivyo endelea Kent Police wameweza kukamata watu na baadhi za pesa zilizoibiwa.Soma hapa

    Tatizo la nchi yetu Tanzania ni kutokuwa na Good Intelligence report ktk kila kona ya nchi yetu.
    Kama tungekuwa macho ktk kila mitaha, majeshi yetu, na mipaka ya nchi kusingekuwapo na haya mambo.

    Mfano: Baadhi ya asilimia kubwa na Silaha zinazotumika ktk ujambazi huu zinatoka nje ya nchi, Je huu ni uzembe wa nani? Immigration officers ktk mipaka yetu? Au Rushwa inayo fanya watu waingie nchini kama watakavyo na kununua passports zetu kama njugu? Au Police na Intelligence officers kutokuwa macho?

    Leo hii nenda ktk guest houses na ma-hotel kibao utawakuta wageni kibao wanaoishi kinyume na sheria hapa nchini.Huu ni uzembe mwingine.

    Mimi nina uhakika kabisa kuna uzembe ktk kila vyombo vyetu vya ulinzi ambapo baadhi wa maofisa wetu wanajitafutia utajiri kwa kushirikiana na haya majambazi.
    Fikiria ni mamilioni mangapi yameibiwa, je unadhani huu uzembe aufanyi uchumi wa nchi yetu kuzolota?

    Na police wetu hawaoneshi progress yoyote ile kuyakamata haya majambazi na pesa zilizo ibiwa.Yaani inatia huruma na Hasira.

    Ingekuwa vyema kwa maboss wote wa police na maofisa wengine wa vyombo vyetu vya ulinzi kufanyiwa uchunguzi.Kuna maofisa kibao tunajua mishahara yao lakini cha kushangaza utawakuta na utajiri wa kutisha je wameupata wapi? Je ni rushwa ama Kushirikiana na haya majambazi? Maana hiyo mishahara ata ukiizidisha mara miaka mitano uwezi kupata huo utajiri wao.

    Mwisho, Ingawa tuna baadhi ya maofisa walio wema na wachapakazi lakini kuna wengi ni wala rushwa na wezi.Kuna kazi kubwa ya kufanya.

    Wakamateni hawa watu na pesa walizo iba, Sasa hivi Taifa letu lina matatizo kibao (Njaa,Umeme, Umasikini, Magonjwa, n.k.) hivyo tunaitaji hizi pesa zinazoibwa kuendeleza uchumi wetu.

    Wazembe wafukuzwe kazi.

    Nadhani sitokuwa nimewaudhi baadhi ya wasomaji wengine, Kama mtakuwa mmeudhika kwa yote nawaomba mniwie radhi.Ukweli utabaki ukweli.

    Nashukuru.

    ReplyDelete
  8. Kent, hii kiwanja ndio bunge lenyewe, japo hakuna mashangingi na marupurupu! ndio kuelimishana humu humu. haya mambo tungeyajua wapi sasa kama usingewakilisha!!

    pia blogu imeonekana ni njia nzuri ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru! watu wanaoweza kupingana bila kuwa maadui! - kitu tunachokikosa sana katia siasa za bara letu! blogu pia ni mtambo wa kurekebisa tabia - watch tower!

    cha mwisho lakini ninakusifu, ni hii teke linalokujia lililokuwezesha kuweka viungo maridhawa kama kule tunapochapisha hizi mambo! tunaomba utupe shule wengi wetu hatujui kuweka viungo kwenye maoni!

    kazi nzuri, laiti Mahita angekuwa bado IGP apwewe huu ujumbe, lakini si haba hata Kamanda Mwema ameupata!

    ReplyDelete
  9. Mark sijakupata vizuri kuhusu viungo kwenye maoni lakini kama nimekuelewa sawa, basi nina hii website inahusu javascript. Click hapa

    Hiyo website ina mambo mengi mazuri ambayo ni bure, wewe ni kufuata maelekezo na utaona website yako au page yako inapendeza zaidi.

    Ukitaka mengi zaidi kuhusu javascripts nenda Google au Ask Jeeves alafu search neno java scripts na utapata mengi zaidi.

    Note: baada ya kupata (ku-copy)hizo code kutoka ktk website hiyo juu niliyokupa, kama website yako ni blog nenda chini kabisa (mwisho) ktk Template na u-paste alafu click ktk save template changes na mwisho republish your blog.

    Na kama una website nyingine siyo blog unabidi ufuate maelekezo kama utakavyoelezwa au nenda chini (mwisho)ktk sehemu unayo ifazi code ya website yako na u-paste na ku-save.

    Kwa ujumla wewe fuata maelekezo.

    Kama ndivyo ulikuwa unamaanisha basi nitakuwa nimekujibu maombi yako kama si hivyo naomba unieleweshe zaidi.

    Nashukuru.

    ©2006 MK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...