Home
Unlabelled
ujiji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
balozi huyu kaninyima viza
ReplyDeletePicha hii imenipeleka pande kadhaa.
ReplyDeleteKwa upande mmoja:
Inanionyesha jamaa waliotumwa kwenda kutafiti ughaibuni ili kuleta mali nyumbani kwa faida ya taifa zima. Kazi yao waliitimiza na matokeo yake yanaonekana mpaka leo, kesho, mtondogoo, na milele. Basi na siye Watanganyika tungekuwa tunakuja huku ughaibuni kwa kutumwa na serikali zetu kuja kuhemea kwa faida ya nyumbani kama walivyofanya hawa jamaa tungekuwa mbali sana kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiteknolojia na kisayansi. Lakini cha ajabu kuna baadhi ya mabalozi wa tanzania nchi za nje hata kukutana na wananchi wao inakuwa sudi,hofu, mashaka, au bahati na nasibu.
Upande mwingine:
Ningelikuwa anthropologist ningetunga hypothesis juu ya utiifu, amani na utulivu waliokuwa nao Watanganyika kwa kusawiri jinsi wale majibaba waliombeba Dr Livingstone toka Mpwapwa hadi Bagamoyo akiwa amekufa. Jamani! safari ya hawa jamaa haikuwa fupi na yenye raha. Ukizingatia kwamba walikuwa hawana viatu, wala mashati au suruali kwa hiyo miba, joto, baridi, vumbi na kila kitu kilikuwa kinawapiga kisawasawa. Zaidi ya hiyo, mzigo wa maiti. Fikiria unatembea umebeba maiti siku tatu, nne, wiki, au zaidi siyo jambo la mchezo. Na pengine maiti mwenyewe kishaanza kutoa harufu. Lakini Watanganyika wale kwa sababu ya utiifu, amani na utulivu wao wakamfikisha mpaka Bagamoyo misheni wakamkabidhi kwa wazungu wenziye. Cha ajabu wale jamaa majina yao wala hayajulikani wala hawakuitwa na Malkia kwenda kutunukiwa Usir!
Jambo jingine:
Inanikumbusha habari za watu kama kina Sidi "Bombay" Mubarak, Mtanganyika ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi na mtafsiri katika misafara ya Richard Burton na John Speke. Hapa ninachanganyikiwa kidogo: Sidi Bombay alikuwa amejifunza wapi na kuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ngapi zaidi ya Kiswahili, Kiingereza, Kihindi, Kipeshia, na lugha zingine kadhaa za makabila ya Kitanganyika na Kiafrika? Sijui kama Tanzania yetu ya leo tuna wanalugha wa kariba ya Sidi Bombay. Pia ninajiuliza kuhusu kutapakaa kwa lugha ya Kiswahili kwa wakati ule tokea mwambao wa pwani hadi bara.
Zaidi ya hayo:
Kutamakani nyumbani na kuzurura ughaibuni kote kuna fadia zake. Hebu angalia faida walizopata Waingereza kutokana na kuzurura ughaibuni kulikofanywa na hawa mabwana!
F MtiMkubwa Tungaraza.