hapa ndo pangu jamani, vyumba sita na wapangaji idadi hio hio. hiyo meza na viti vya kulia chakula (?) ni vya baba mwenye nyumba, anaeishi uani na familia yake ya watu nane na watumishi watano (watatu wanauza kahawa, mmoja anaipika mwingine kazi za nyumbani) na choo na bafu ni moja. mie chumba changu, niishicho na mai waifu wangu na watoto watatu, ni hicho cha kwanza kulia... maswaaali?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Michuzi kabla sijaenda mbali, tafadhali fafanua vizuri... ina maana huyo baba mwenye nyumba wenu anawapatia pia na mapazia? au ndio milango yenyewe? Manake naona hiyo nyumba yenu mapazia yote saresare!

    ReplyDelete
  2. Nyumba za namna hii kazi ipo asubuhi kwenye foleni za kwenda chooni na bafuni. Tatizo lingine ni jinsi ya kushea bili ya umeme, zamu za kusafisha choo. Si ajabu ukakuta familia ya baba mwenye nyumba haihusiki kwenye usafi wa nyumba wala bili ya umeme. Mlango wa nje ni mmoja hivyo ukichelewa kurudi jiandae kulala nje

    ReplyDelete
  3. Duuh!! Ama kweli Bongo haina huruma! Pole sana Michuzi. Walahi sikutegemea kabisaa kama ungekuwa unaishi kwenye mazingira ya kifukara kama hivi. Usinielewe vibaya mzee, nasikitika tu kuona jinsi mwandishi wa habari mchapakazi. tena afsa mzima anavyo zawadiwa kwa utumishi wake wa miaka na miaka serikalini.

    ReplyDelete
  4. Michuzi.. Umesahau kutuambia kuhusu choo ni cha aina gani? passport size au???

    ReplyDelete
  5. heri yako michuzi unaraha sana, mwinzio nakaa vyumba vya uwani, mende kibao.

    ReplyDelete
  6. Michuzi,
    Mswalie mtume.....Maisha haya najua ulishayakimbia kitambo kirefu. Si vibaya kutupa ushuhuda wako wapi ulitokea. Inawaongezea nguvu vijana kuona kwamba kwenye nia ipo njia.
    Londo

    ReplyDelete
  7. awe michuzi au mtu mwingine yeyote awate, haya ni maisha ya taabu. Naamini hapa si kwa Michuzi, ila nataka kujua, Michuzi ulienda kufanya nini kwenye nyumba hii?

    ReplyDelete
  8. Kaka, hilo jicho lako. Picha safi kweli kweli.

    ReplyDelete
  9. Michuzi hii nyumba inavyoonekana ni ya loong time,ukiangalia dari yake ya kifusi siku hizi watu wanatumia hardboard,softboard or whatever na milango yake pia ni ya kizamaani na inavyoonekana watu wa nyumba hii bado hawajaanza kutumia LUKU naona kuna mita ya TANESCO karibu na mlango wa mbele.Ningependa kujua hii nyumba iko maeneo gani Dar,pwani au ZNZ?

    ReplyDelete
  10. Mimi anacho niuzi bwana michuzi ajibu maoni yetu ina maana hasomi blogi yake. Bwana shemeji soma ata siku moja moja ili uweze kujibu maoni yetu.Tutafurahi ukisikiliza hiki kilio.

    ReplyDelete
  11. Acha fiksi wee michuzi . . .

    ReplyDelete
  12. Michuzi acha utani hapa siyo kwako bwanaaa. Hapa bila shaka ni Zanzibar, nyumba hii ni ya enzi zile ama kweli umepatia maisha ya wabongo wengi. Hivi hiyo rangi ya mafuta ikifika saa saba hivi wanakuwa na hali gani watu wanaoishi humo?

    ReplyDelete
  13. nasoma sana blogu, usijekosea, hata yale mazito dhidi ya janguo nimeyaona, nadhani tokeo umeona. hapa jamani ni kwangu, sehemu za kariakoo (mtaa sitaji, msijentembelea) kwani sina sebule. sita kwa sita yangu imetanda chumba kizima, helafu feni ya shingo na tv ya aiwa inchi 17 kwa juu ya kabati la vyombo. nguo na nini uvunguni. choo, kumjibu jamaa alieuliza, ni cha pasipoti, na shurti uwe na shabaha na bingwa wa kukwepa; kwani ni tundu la sindano na kinajaa haraka.rangi ya mafuta tumeweka sababu wajukuu wa baba mwenye nyumba si wastaarabu kama alivyo babu yao. tuliweka ya chokaa wakaiandika yote. angalau hii wanaishia kukwangua tu na visoda. halafu hapo hashindi mtu, kama mai waifu wangu kupika anapikia uani. labda inyeshe. maji ni ya kununua na umeme wa tanesko sababu umo kodini. wote tumepinga luku, zogo la ulipaji mwalijua...

    ReplyDelete
  14. nasoma sana blogu, usijekosea, hata yale mazito dhidi ya janguo nimeyaona, nadhani tokeo umeona. hapa jamani ni kwangu, sehemu za kariakoo (mtaa sitaji, msijentembelea) kwani sina sebule. sita kwa sita yangu imetanda chumba kizima, helafu feni ya shingo na tv ya aiwa inchi 17 kwa juu ya kabati la vyombo. nguo na nini uvunguni. choo, kumjibu jamaa alieuliza, ni cha pasipoti, na shurti uwe na shabaha na bingwa wa kukwepa; kwani ni tundu la sindano na kinajaa haraka.rangi ya mafuta tumeweka sababu wajukuu wa baba mwenye nyumba si wastaarabu kama alivyo babu yao. tuliweka ya chokaa wakaiandika yote. angalau hii wanaishia kukwangua tu na visoda. halafu hapo hashindi mtu, kama mai waifu wangu kupika anapikia uani. labda inyeshe. maji ni ya kununua na umeme wa tanesko sababu umo kodini. wote tumepinga luku, zogo la ulipaji mwalijua...

    ReplyDelete
  15. naona mitambaa panya kwa juu hapo.jamjuah

    ReplyDelete
  16. Michuzi isi ujobile hapo pamwanya sya naloli pamo kulonda kutwala inongwa itolo? Nikujoba isi papo muno kuboneka na muno gwasimbile kumyangu ukuti ikisu kya Bongo kumyako mma kinunu, pakafu ukuti niitikege. Linga momumo mma bakupepo akajumba kamo ku-bupanga (Upanga).

    ReplyDelete
  17. joni, pakali pomumo. ndi kubhaketa bajanga bikujobha nki. une kumyangu kununu itolo. linga ukwisa angukupimba upabone.

    hahaah! joni aliniuliza kama hapo ni pangu ama magirini. nimemjibu ipaswasyo, kuwa ndipo

    ReplyDelete
  18. Ahha brother mbona unatupiga fiksi mchana kweupe!!!! siye ndugu zako wa karibu twajua kwamba Tabata unakokaa hakuna kijumba cha aina hiyo achilia mbali Tukuyu.

    Sya fiki utusyoboge tu abandu abakusi? kumyako tupamenye. Tubabenye abakamugo bosa. Leka ubutungulu Michuzi.

    ReplyDelete
  19. asee! gwe absalomu fyo fiki?

    ReplyDelete
  20. haaa michuzi sikujua kama wewe mnyakyusa?

    ReplyDelete
  21. Usimuonee michuzi kwamba hajibu maswali ya watu anajibu kila swali ktk kila hoja
    linalojibiwa bwana mzee hapo juu ni swali si oni,maoni yanapokelewa au kutolewa nje na mhusika hivyo bwana michuzi nadhani tuko pamoja na tunaelendelea kukufagilia kwa heshima na nidhamu kubwa uliyokuwa nayo.

    ReplyDelete
  22. ngimba uli nnyakyusa michuzi tukameenyee. uswe twe bha dada bhako tuli mu london fyo fiki fififyo kubasyoba abajanga ba bhandu!!!?? Jubha!!

    ReplyDelete
  23. Mnabakia kuendekeza ukabila tu wakati mwalimu alishakataza. Mkitaka fungueni blogu nyingine kwa ajili ya wanyakusya

    ReplyDelete
  24. kweli kabisa hawa ndio watakao kuwa wa kwanza kuanzisha vita na kujitenga.acheni ukabila jio watu.mshasahau ya nyerere?

    ReplyDelete
  25. nyie watu acheni ukabira.

    ReplyDelete
  26. na wewe mbona unauendeleza wa musoma ni ukabila si UKABIRA wewe anony vipi?

    ReplyDelete
  27. kaka michuzi acha utani...maisha magumu jijini kuna watu wanaishi katika mazingira kama hayo...shukuru maulana unaishi pema kuliko hapo unapopafanyia mashala
    !!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...