jk akimpa pole mmoja wa mapolisi waliopambana na majambazi waliopora pesa za mnb karibuni. kesho (alhamisi) jk anatembelea magereza ya keko, ukonga na segerea kujionea hali ilivyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2006

    Jamaa wa magereza wiki hii utakuta wamekuwa busy mno kusafisha uchafu ulioko huko...Na mimi lile suala la kubeba wafungwa kama mbuzi kwenye yale magari mimi naona ni against na human rights kabisa. Mahabusu wale hawakutakiwa kuwa wanajazana vile kwenye lile lori vile kwani haiwezekani kununua scania au jiefang lingine waweke na viti hili wawe wanakaa, sidhani kama wanashindwa hili kwasababu magari ya serikali hayalipiwi kodi. Na pia tatizo la lishe na hygiene yale wafungwa ndo maana magonjwa ya milipuko hayaishi kwenye magereza yetu. Na pia kuna hule mtindo unasikia eti leo gari bovu,wafungwa hawawezi kuletwa mahakamani. Hule jamani ni uzembe na unyanyasaji wa watu...Na watu wanaosimamia hayo magereza wanatakiwa wawe wanajiuzilu uzembe kama huo ukitokea, huwezi kusema gari bovu ndo maana wafungwa hawajaja mahakamani, hukiwa kiongozi unatakiwa huwe na alternative za kufanya sio kuwaacha watu wake tu kule.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2006

    jamani huyu ndio rais wetu au namchanganya? anajimix sana naye bwana sikatai kujishusha kama watu wa chini lakini atafanya kwa wangapi? anasahau protocol ee ngoja wamshughulikie.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2006

    casual wear jamani ha ha ha ha ha

    pole sana polisi wa wetu, ila michuzi unadhani hiyo picha kumtoa mwenzako na tumbo hivyo anafurahi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2006

    Our Military Police needs people who are physically fit.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2006

    nimeshindwa kuelewa risasi umekosaje hilo tumbo,mpaka mzee mwenyewe naona mzee anacheka!
    yaani msalie mtume kidogo angetumbuliwa baba wa watu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2006

    aise anaenda kutoa misamaha au ni kutembelea tuu?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2006

    hutu raisi poa sana amesema atawasomesha watoto wa marehemu. huyu kweli ni the people's president

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2006

    Michuzi kwa hii habari ya ubungo umekuwa mchoyo mno kutuhabarisha vilivyo wa ughaibuni,kwa nini lakini?AU kwa kuwa upo kwenye sistimu?Tutafutie picha ya koplo solomon akitinga ndani ya cheo kipya!

    ReplyDelete
  9. poa anony. sajini solomon, ambaye ni mshkaji wangu, tena kwa taarifa yako ni askari trafiki wa pikipiki, namsaka kwa udi na uvumba. inshaalah ombi lako litatimizwa

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2006

    HIYO PICHA NAISUBIRI KWA HAMU!MPE HONGERA SANA ,AMENIKONGA KWELIKWELI.NI MTU WA MKOA GANI?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2006

    Mimi nashauri huyu Solomon waanze kumpa ulinzi maana hayo majambazi yaliyotoroka yatakuwa na hasira naye sana, wanaweza kummaliza.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2006

    Michuzi,
    Huyu askari aliyetembelewa na mh. Rais ni trafiki polisi au? manake naona tumbo lake halina uhusiano na askari wengine.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2006

    huyu police achunguzwa akipona, hiko kitambi mie na mashaka nacho kama ni cha halali au ndio walewale!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 05, 2006

    Jamani, huyu afande ameridhika na maisha yake ya shida.

    Huko kunawiri kwake sio kwasababu ni mbadhirifu au mla rushwa, bali ameridhika na maisha yake ya kiwango cha chini.

    Anaishi vyema na mke wake na familia yake. Anafuraha moyoni pamoja na kuwa na kipato cha chini.

    Kuna watu wangapi wanamabilioni lakini afya zao wala haziakisi utajiri wao? Hiyo inatokana na kuishi kwa mashaka. Pesa za wizi! Hapo hata kwa dawa huwezi kunawiri.

    Mwache afande wa watu na afya yake.

    Pole sana mkuu, tunakumbea upate nafuu mapema.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 25, 2006

    Aise JK kaenda kishikaji kweli na baada ya picha hiyo akawafungulia mashitaka ya uuaji majambazi wa Ubungo hapo hapo hospitali kwa hiyo hakwenda tu kuwaona wagonjwa bali kutoa tamko la serikali. Angalia watu wameshitakiwa kwa mauaji si uporaji au ujambazi. JK huyo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...