hapa ni nakivubo, kampala, mwaka 1993 klabu bingwa afrika mashariki na ya kati. wenye ubavu tupeni majina tafadhali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2006

    Umenikumbusha Bongo Michuzi, But nawakumbuka wachache kutoka kulia
    1.Keneth Mkapa
    2.Stephen kazimir Nemes
    3.Mohamed Husseim Mmachinga
    6.Issa Athuman Mgaya
    7.Zamoyoni Mogella Golden boy
    8.Edibily Lunyamila
    14.Said mwamba kizota
    15.Rifaat Said Mpemba.
    Nadhani baada ya machinga huyo mwenye mpira ni Abubakar Salum.Wengine nimewasahau.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2006

    aaaahhhhh Michuzi mbona umenikumbusha mbali hiyo timu hapo simba walikuwa wanalia kila leo maana kila wakitia mguu ni bao kwa kwenda mbele nawakumbuka wachache wengine siwaoni vizuri, kenneth mkapa, steven names,mwanamtwa kiwelu issa athumani,lunyamila,riffat said etc.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2006

    Dah hii si mchezo Issa Muhidini wa Michuzi! umenikumbusha Good old DaYs! hawa ndio Kuala Lumpur Ndugu yangu! Kuanzia Kulia Dar Young Africans:-

    Keneth Pius Mkapa;
    Stephen Casmir Nemes "Masajage";
    Mohammed Hussein "Mmachinga"
    Abubakar Salum "Sure Boy"
    Mwanamtwa Kihwelo "Garincha"
    Issa Athumani Mgaya
    Zamoyoni Mogella "DHL"
    Edibily Lunyamila
    Steven Mussa
    Hamisi Thobias Gaga
    Method Mogella "Engineer"
    Mikidadi Jumanne "Bubu"
    Saidi Nassoro Mwamba "Kizota" &
    Riffat Said

    Michuzi acha tu! acha tu! Simba na Friends of Simba yao walikuwa wanakoma na sisi we acha tu! Mungu Mkubwa! atatujaalia tena tuache ubabaishaji katika soka!

    Hamidu A. Mashaka
    mhamidu@mof.go.tz
    shark_ham@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2006

    Enzi hizo watoto wanatinga Boby Soap. Watoto waliku wametulia. Enzihizo hata litokee Gogoro kubwa kivipi klabuni watoto walikuwa Wanatinga kwenye Sharuksi wanaenda kumpiga mtu bao chini ya Uongozi wa Kapten Kocha Mchezaji Marehemu Issa Athumani Mgaya.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2006

    It has been 16 years since this pictures had been taken in Nakivubo stadium.But we still remember these guys. Can somebody tell me Why? And do you think we gonna' be able to mention atleast recently Yanga and Simba player in 13 years later??

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2006

    kuna mtu kawapatia wote vizuri mpaka STEVEN MUSSA lakini baada ya hapo namuona MP, David Mwakalebela, Sanifu Lazaro( tingisha) Willy Mtendawema, na kuna mtu kama sikosei ni marehemu Method Mogella(Fundi) mungu amlaze mahali pema alitupa raha sana pale neshno!!of kozi na Riffat Said
    enzi watoto walikuwa wanakwenda kama umoja wa mataifa ilikuwa raha tupu pale jukwaa la ushindi, main stand upande wa YANGA DUME!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 31, 2006

    Michuzi, Tafadhali tubandikie picha ya Katibu mkuu wa Tiefuefu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 31, 2006

    Sasa hapo viungo nani alikuwa anaanza kati ya Gaga,Method Mogella au Issa Athumani? Na je listi nzima ilikuwaje maanake huko mbele kuna kizota, machinga na Zamoyoni.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 31, 2006

    wakati mwingine tunatamani mno nyakati hizi zijirudie, lakini aaaah ndio hivyo tena, neva kam bak ageini

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 31, 2006

    Chama lilikuwa hivi: 1. Steven Nemes 2. Minziro/ Mkati 3.Keneth Mkapa 4. Method Mogella 5. Wille Mtendawema 6. Issa Athuman 7. Abou Sure Boy 8. Hamis Thobis Gaga 9. Kizota 10. Daima Mmachinga 11. Lunyamila. Lakini kumbuka enzi hizo Yanga ilikuwa ndio timu pekee yenye uwezo wa kutuma nusu Timu mkoani wakati timunyingine inacheza Dar. Ilikuwa balaa babu!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 31, 2006

    Aloonimekosea number 2. alikuwa David wa Mwakalebela na sio minziro

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 31, 2006

    Anony at 7:14; Viungo ilikuwa inakuwa hivi; Method anasimama nne, Issa anakamata sita, Gaga anafunika nane akisaidiana na Steven Musa. Yani timu ilikuwa safi hata akianza nani huoni tofauti. Ila hao ndio walikuwa waanzaji most of the time.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 31, 2006

    Check this; Yanga Vs RTC Kagera; ( Kaitaba Stadium) 1. Rifat Said. 2. David Mwakalebela 3. Keneth Mkapa 4. Method Mogella 5. Mtendawema 6. Issa athuman 7. Sanifu Razaro 8.Hamis Thobias Gaga 9. Said Mwamba Kizota 10. Mohamed Hussein mmachinga 11. Lunyamila. Next two days watoto wanatakiwa wakipige Dar.(Ngoma ilikuwahivi) 1. Steven Nemes 2. Seleman Mkati 3.Minziro 4. Said Zimbwe 5. Mwanamtwa Kiwelu. Mikidadi jumanne 7. Sure Boy 8. Steven Mussa 9. Zamoyoni Mogella 10.Mohamed Hussein 11. John Alex. Sim mchezo!!!

    ReplyDelete
  14. hii kanitumia ndugu yangu mmoja kwa email leo:



    Kutoka kulia kwenda kushoto: Kenneth Pius Mkapa, Steven Nemes Masajage, Mohammed Hussein “mmachinga”, Abubakar Salum “Sure Boy” Mwanamtwa Kihwelo, Isaa Athumani Mgaya (Marehemu), Zamoyoni Mogella “DHL”, Edibily Lunyamila, Steven Mussa, Hamisi Thobias “Gaga” (Marehemu), Method Mogella (Marehemu), Sekilojo Johnson Chambua, Mikidadi Jumanne, Saidi Mwamba “Kizota” na Rifat Said (Marehemu). Muhidini Issa wa Michuzi! Hapo alikuwa hachomoki mtu chama hilo! Acha bwana siyo siku hizi kila mtu anataka kucheza mpia! Soccer ina wenyewe bwana! Jogo Bonito! (The sound of Football)!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 31, 2006

    Michuzi! Hapo Chambua hajakanyaga mguu Jangwani. Ki punk hicho ni cha Mtendawema. Yule number tano alikuwa katulia sana pale kati, mipira ya juu ndio usiseme. Punk likuchanganye Michuzi!!Najua Chambua ana punk pia lakini hapo alikuwa bado hajatua Jangwani!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 01, 2006

    Kuna jamaa alikuwa anaitwa Salum Kabunda "Ninja" unaweza kutuwekea picha yake Michuzi??

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 01, 2006

    MMESAHAU WAKATI HUO MAMBO YOTE YALIKUWA UNAYAPATA KUPITIA REDIO TANZANIA DAR ES SALAAM.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 02, 2006

    sawa sawa mwana yanga, yule baada ya Steven Mussa ni Marehemu BABA TOBI, Gaga, kuna mchezaji mmoja alikuwa anachezea AC Milan, miaka ya 90 hivi, Zvonimir Boban, kiuchezaji alikuwa hana tofauti yoyote na Gaga, mpaka wanavyokimbia, sema ndio tatizo la kuzaliwa kwetu, huonekani.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 03, 2006

    Kama mnakumbuka kule Kampala Kocha alimrudisha Issa Athumani akawa mkoba, namba tano, mwisho wa michuano hiyo akawa beki tano bora!
    kama vile ambavyo alimrudisha Mtwa Kiwelu kutoka katikati(miedfield) hadi beki mbili ambaye pia aling'ara sana, Kocha alikuwa yule mrundi, Nzoyisaba Tauzani, yanga ina wenyewe jama na mimi ni mmoja wao.
    Michuzi inasemekana tokea miaka ya nyuma kwamba JK ni Yanga la ngumi( ikibidi hata mkono mtaweka)ni kweli hizi habari?

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 03, 2006

    Michuzi, yupo wapi Salvatory Edward? huyu jamaa kwa mara ya kwanza niliona akimpiga mtu kanzu kwa kichwa!! ilikuwa Taifa Stars na Sudan, japokuwa ilikuwa jukwaa la Simba ilibidi tu na wao washangalie, si unajua itikadi hizi zilikuwepo hata kicheza timu ya taifa
    nimeangalia mechi nyingi ligi mbali mbali, world cup kadhaa ile bado sijaona!!! haijarudiwa!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 04, 2006

    Michuzi unaniacha hoi sana kunikumbusha enzi hizo tamu.

    ReplyDelete
  22. Bwana Michuzi chama lilikuwa linatisha, nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja alikuwa beki 4 wa majimaji sasa namba mbili wao akaumia jamaa akaambiwa atroti kuchukua namba akajifanya ameumia wakati alikuwa benchi wakati huo lunyamila alikuwa anakimbiza balaa na Yanga ametoka kuifanyia umafya Coastal iliyotimia 5-1, Uganda chama lilikuwa hivi
    1. Stephen Nemes/Riffat Said
    2. Mwanamtwa Kihwelo/Mwakalebela
    3. Keneth Pius Mkapa
    4. Willy Mtendawema
    5. Isa Athuman Mgaya
    6. Method Mogella Fundi
    7. Zamoyoni Mogella DHL
    8. Stephen Musa/ Gagarino
    9. Said Nassor Mwamba Kizota
    10.Mohamed Hussein Mmachinga
    11.Edibil Jonas Lunyamila
    Naitwa Martin Chacha-Chacharino

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...