katika mfumo mpya wa polisi mkoa wa dar sasa ni zoni maalumu na imegawanywa mikoa mitatu ambayo ni ilala, kinondoni na temeke ambako kila mmoja una rpc wake. hawa hapa ndo hao maa-rpc wakiwa na afande msika (kushoto) anayetoka makao makuu ya zoni na ni kaimu wa kamanda wa zoni afande tiba. wengine ni afande mgassa (rpc ilala), afande kandihabi (temeke)na afande rwambow (rpc kinondoni. hapa ni hoteli ya movenpick royal palm wakati wa mkutano wa amani wa burundi juzi. anaeongea na simu nyuma yao ni igp mwema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Naaamu wasikilizaji Kwa mbali pale naona Timu ya wezi na wala rushwa ikipanga mstari ikisubiriwa kukaguliwa na mgeni lasmi, Na inaonesha wako fiti hao ata Timu pinzani (PCB) wanaonesha udhaifu wa kukwaana nao. teteteh

    Mpira ni dk 90 usikae mbali, tutarejea live baada ya tangazo lifuatalo:

    TIBAIGANA NA WENZAKO ACHENI WIZI NA KURA RUSHWA.

    Akhasanteni ndugu wasikilizaji, Naam na kweli huyo Rais Mpya anajifanya anapinga Rushwa wakati anamfungia macho Afande Tibaigana na Viongozi wengine wa serikali kwa Wizi na Rushwa wanao ufanya na kumpandisha cheo pia na kuwa Kamanda wa kanda maalumu. Ama kweli hivi ndio vioja Rais na Serikali yake hawana kitu ni wale wale wizi na wala rushwa. Kwa habari nyingine za karibuni amemteua mwizi na mla rushwa mwingine Yusuph Makamba kuwa mbunge wa kuteuliwa ili kutimiza Timu yake ya wezi na wala rushwa ndani ya nchi.

    Kwako Msomaji mwingine, changieni maoni yenu kama mnayo.

    ReplyDelete
  2. ESPIONAGE!

    ONA ULIVYOSHUSHUKA, KWANI HAKUNA ANAYEKUJIBU KWA KUWA WOTE SI ZUMBUKUKU.

    TAFADHALI NAKUOMBA WEWE NA HAO WENYE TABIA KAMA YAKO MKOME KUNICHAFULIA BLOGU YANGU KWA KIVURI CHA MAMBO YA KAWAIDA.

    KAMA UPUUZI WENU HUU UNGEKEWA 'MAMBO YA KAWAIDA' MBONA HATUMEZI MATAPISHI AMBAYO NI CHAKULA KINACHOTOKA TUMBONI.

    MKOME NA WALA HAMNIKATISHI TAMAA. MWENDO MDUNDO NA ALUTA KONTINUA.

    NACHUKUA NAFASI HII KUWATAKA RADHI WOTE WANAOSHAMBULIWA NA WATU KAMA ESPIONAGE AMBAO NADHANI WANAONA GERE KWANI SASA NATEMBELEWA NA WATU ZAIDI YA 20,000 KWA SIKU!

    ReplyDelete
  3. Bro. Michuzi hayo ni kama maoni usi maind sikuwa ktk kukuchafulia taswira yako bali kutoa maoni yangu kwani sio kweli hao watu ni wala rushwa na wezi!! au una watetea? Mimi hapa sijakutaja jina lako wala nini bali nimewataja watu wa ktk picha. Na wala sijatumia matusi kama wengine au una waogopa nilio wasema? Kwa taharifa yako mimi nilikuwa nafanya kazi sehemu moja na hao watu kila baada ya wiki walikuwa wanakuja kuchukua mzigo wao (Pesa) au wanatuma watu kuchukua sasa utaniambia nini? Sio wakati wa kuwaogopa au kujikosha. Sijakutukana wala sijatumia matusi wala sijakusema wewe.

    ReplyDelete
  4. We Espoinage uongee vitu ukiwa na evidence sio unabwabwaja tu. Kwa taarifa yako Mh Makamba alitaka kustaafu na alishatangaza kabla lakini akaombwa aendelee na ndio akapewa tena ukuu wa mkoa, na kuhusu yeye kupewa ubunge wa kuteuliwa anastahili kabisa kwa sababu kazi aliyoifanya ndani ya hili JIJI lake ni kubwa sana ingawa na yeye pia ana mapungufu yake kama binadamu

    ReplyDelete
  5. Kweli watu ni wagumu kuelewa na kuona nyie mnawasifia wao wanajua wanayo tenda! Ni kweli na ni wazi Tibaigana, Makamba na Viongozi wengine wa Serikali ni wezi na wala rushwa na sio kuwa na nina bwabwaja kama ulivyo sema.

    Serikali ingekuwa ni ya wazi na inaweza kunipa Ulinzi wa maisha yangu na familia yangu ningetoa ushaidi nilio nao kwa hao viongozi wote wa ndani ya Serikali.

    Rais mwenyewe anawajua ila wanafichana!! Mrema alisema anawajua wala rushwa wote lakini yupo tayali kama Serikali ikimpata ulinzi wa maisha yake na familia yake. Kwa taharifa yako hawa watu wapo lazi ata kuua ili mradi tu waweze kujilinda maslahi yao.

    Kila kitu kipo na ushaidi upo na inawezekana ata PCB wanajua bali ndio kulindana kwakua ni vigogo, Kusema nitasema ila ushaidi siutoi hapa maana nikiutoa hapa watafahamu ni nani anaye sema hayo na kunimalizia familia yangu ukizingatia nipo DSM kabisa!!

    Ni Mapolisi wangapi ni wala rushwa na wezi lakini wote wanajuana kwamba ni wala rushwa wanaogopa kuwafukuza kazi na walicho fanya ni kuwabadilisha mikoa!!

    Kama kweli PCB wapo macho na kuona haya ninayo sema ni vizuri waweze kuwafuatilia wote ninao sema na mtaona kila kitu. Kama wewe ujui kuhusu hawa watu hacha kabisa kuongea chochote maana hawa watu ni wezi na wala rushwa wakubwa na wana ludisha tanzania nyuma.

    Narudia tena, Hawa watu ni kama timu na wanajuana na kulindana, wana nguvu zaidi ya PCB, Ni mawaziri, Makamanda wa polisi na Polisi wadogo wadogo wote wa kawaida, trafiki, nakazalika, Wabunge, Wakuu wa mikoa na wasaidizi wao, n.k wote ni wala rushwa na wanajulikana ila ndio wanalindana wao kwa wao na serikali, PCB, Rais.

    Wanajua yote haya katika mioyo yao kwamba ni wezi wakubwa na wala rushwa, Uliza kwamba wanapokea mshahara Shilingi ngapi ili waweze kuwa na mali, pesa nyingi katika akaunti zao.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2006

    Simba rudi nyumbani bwana au tukuchangie, wewe tangia 2002 hujarudi bongo. Ndio maana unaweza kuibiwa unadhani ni polisi maana naona huwezi kutofautisha polisi na matapeli. Pole sana bro.Marekani hao hawapo kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...