utakumbukwa daima hayati mzee mwinamila wa tabora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bwana Michuzi nahisi nilikuwa nimelala kidogo nimekuwa natafuta sana habari za huyu Nguli Mwinamila (Kinyamwezi) au Ng'winamila (Kisukuma) , Bwana Fadhili maswali yako sijui nani atayajibu, RTD nina imani kwamba wana kazi nyingi sana za Nguli walo tangulia mbele za haki. Nafikiri RTD kama wangekuwa na kipindi kwa mfano tuseme " Sanaa zetu" kipindi hiki kingepata watu na vijana wangetambua na kuipa kipao mbele sanaa ya asili. Uhifadhi wa vipaji nafikiri inategemea sana mtu binafsi, ukiijali basi utaihifadhi (sanaa)

    Kama mtu anajali kitu nilazima atakifuatilia nakukipa nafasi katika maisha yake, kwa maana ya kujifunza na kuendeleza. Jambo jingine ni vyombo vya habari,( wandishi, wapiga picha n.k) ni watu muhimu sana ktk uhifadhi, ukiachilia mbali mafundi wa sauti (wenye studio za kurekodi). Baraza la sanaa pia.

    Lakini pia ujitambuaji wa wasanii wenyewe kuweza kuratibu kazi zao ni chanzo cha uhifadhi. Lakini changamoto inakuja; wanapata wapi pesa za kuweza kurekod nyimbo zao na kuweza kuziratibu? Na nani yuko radhi kuwafadhili wakati soko la huu muziki halipo?

    Vitu vinavyo reza changia sanaa ya ngoma na nyimbo za asili kuinuka tena ni vyombo vya habari (radio, Tv) nyimbo zikiwa zinapigwa na video kuoneshwa nakwambia kutakuwa na badiliko kubwa saaaana.

    Na hapo vijana watapenda kurithi tamaduni zetu na kurithi uendelezaji wa sanaa hii ya ngoma na nyimbo za asili.

    Michuzi nikupongeze sana kwa kufikiria kuanzisha uga huu.

    Mimi nacheza hizi ngoma na kuimba pamoja na kutunga, hivi Juzijuzi nimefanya usali (interview) na mzee mmoja kiongozi wa kundi la Hiari ya Moyo kundi alilokuwa analiongoza mzee Mwinamila. Maana nina andika andiko kuhusu ngoma ya Hiari ya moyo.

    Bwana Fadhili sio watasahaulika, wamesahaulika!
    Kia leo niishie hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...