uwanja wetu dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2006

    Jamani wanablog huu uwanja mara tuu baada ya kujengwa na wafaransa kama sikosei kampuni ya Bouygues ulikuwa bomba sana AC,vyoo visafi,TV screens,utaratibu mzuri nk lakini tangu tukabidhiwe wazalendo mambo mengi yameporomoka!Nimekuwa nikipitapita hapo na kuhuzunishwa na hali halisi.Maswali meneja anafanya kazi gani?aiport tax wanapeleka wapi?wabongo tuna matatizo gani?Mapya niliyoona mwaka huu ni uhamiaji kuwa na scanners kutokana na paspoti mpya pamoja parking ya kulipia pale nje.Matitizo sugu ni Ac na luggage carriers ambazo zimefanywa mradi eti unasukumiwa na kutoa chochote!Duniani kote msafiri anatumia bure maana iko kwenye aiport tax!Jamani bongo aibu tupu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2006

    Yaah government need to think quick about the place...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2006

    Sio ndio hayo hayo tunasema watanzania tuko nyuma sana kielimu na kimanagement! Kuajiliwa kwa jina! CV za leaders utachekea chooni! Kuna sehemu nyingine zitaifishwe tu! Sababu kwa ubishi wetu mpaka rasilimali zina sink! Toka tulivyoachiwa na wakoloni ndio basi tena! Walioifaidi real Dar City na TZ ni watu wa miaka 10 baada ya ukoloni. Badala ya hapo........!
    Tunawatukana mpaka leo na kuwashutumu wakoloni! Je ni % ngapi hapa Africa wanawish kwenda kwa wakoloni kutawaliwa leo hii? Hellooo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2006

    Sidhani kama tatizo ni CV's, au elimu; nadhani tatizo ni uaminifu, ukweli na uwajibikaji.
    Warioba ana CV moja nzuri tuu, lakini sidhani kama utendaji wake wa kazi una-"reflect" CV yake.
    Mkapa amekiri kuwa alichemsha katika mikataba, jee kuna mtu yeyote anayefikiria kumuwajibisha? Kama aliingia mikataba kwa faida yake na hasara ya wananchi sasa kwanini asiwajibishwe?.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2006

    hili ndio tatizo la kuwapa watu kazi wasikuwa na uzoefu au utaalam nazo.
    ili mradi tu mtu ana degree au whatever award basi tena ataajiriwa popote pale.
    jamani hebu tuige wenzetu maana wao wanaajiri mtu mwenye utaala na hasa kama ni nafasi nyeti kama utawala na vitu kama hivyo.....
    hivyo inabidi government iangalie vizuri hili swala vinginevyo hata vikijengwa viwanja vipya, au kuletwa vifaa vibya kama hakuna muongozaji anaefaa tutaendelea kulalamika miaka nenda rudi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2006

    msiwe na wasiwasi kuna mradi mwingine wa kujenga airport nyingine ya kimataifa bwagamoyo itakayocost shillingi bilioni 50, helllooo!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2006

    Nakubariana na maoni ya ndugu wote hapa. ira naomba kuongeza kuwa nimefurahishwa sana kitendo cha serikali kuipa jina ra J.K NYERERE hapo wamefanya ra maana maana he was a great man.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2006

    kwa kweli nakubaliana na kigerera kwanini huo uwanja uliooza ndio tuupe jina la mwalimu nyerere...au tumeona aibu kuendelea kuita wa kimataifa kutokana na kutokuwa na viwango.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2006

    Wooo,kumbe hii ndo international airport ya bongo ? mimi nilidhani ni stesheni ya treni ya kigoma

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2006

    Kigerera, asante kwa maoni, ni kweri kabisa nakubariana na wewe, na I hope wahusika wanasoma maoni haya iri wafanye ukarabati kidogo wa hii Airport hasa kwa jina warioipa, ifanane na heshima zote, maana hiki kiwanja hakistahiri kuitwa International Airport, niritemberea chooni pare ni vya hari ya chini sana. naona pesa zinazopatikana wakubwa ni urabu tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...