Home
Unlabelled
oyaaaa!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mmmmh kwema jamani, maana mambo ya Dar pengine kumesha amka zali mmh,
ReplyDeletehapo mlimani- utawala , i know that place inside out!!!hapo peingine wanafunzi washaandama kuhusu maswala ya posho
ReplyDeleteHapa UDSM utawala vijana wanamatch kuelekea nkuruma hapo. hii picha ya lini michuzi bado hawajafunga chuo kwani. Napakumbuka sana hapo nilishawahi kupasua kioo hapo kwenye hizo mbao za matangazo siku tuliandamana kudai hela za off cumpus enzi zetu. tukamwiita luhanga ashuke tuongee nae akakataa basi tulianza kuvurumisha mawe nilikula kioo kimoja hapo huwaga mpaka leo najiuliza nilikuwa na akili za aina gani mpaka nikafanya mambo kama hayo. mambo ya shule wee yaache tu unakujaga kujilaumu baadae sana ukishamaliza lakini ukiwa humo sijui unakuwaje
ReplyDeletehahahahahahaha Anony hapo juu umenikumbusha mbali.
ReplyDeleteAnony hapo juu unanikumbusha enzi hizo, nakumbuka siku moja lakini tulikwenda wizara ya sayansi Dr. bilari akapandishwa kwenye meza barabarani(pale mbele ya sayansi). Mkapa yuko juu(waziri wakati huo).Hapo ni posho tu na kelele kibao. Kumbe polisi tunao tunapiga story, wale bwana FFU walipokuja ni mabomu tu hata hawakujari polisi wenzao na polisi wakatugeuka ni ngumi tu. Mimi nimkimbiaji maarufu, lakini siku hiyo mbio zote ilikuwa kama mwendo wa kinyonga. Nilibahatika tu nyumba zilizoko pale waliniokota mpaka nilijikuta chumbani wakanimwagia maji.
ReplyDeleteNikapata auweni, baada ya hapo sikutafuta hata daladala. Nilikimbia kwa miguu mpaka UDSM tukaenda kumalizia hasira kwa Luhanga. Tukakaa maeneo hayo mpaka jioni tunamsubiri luhanga. Tukasema tunalala hapa tuklimpata tu hasira zote kwake.Mpaka kieleweke. Kesho yake posho zikatoka.
Haya jamani mimi sina maoni ya kuhusu hii picha bali ni maoni ya kuhusu majina mbalimbali tokea blogu hii ianze nimeona wanablogu jinsi walivyo na majina ya kufurahisha tukianzia na bwana rhxoqsa ee bwana mimi jina lako nimetafuta kwenye kamusi silipati sijui umelitoa wapi na kulitamka ni vigumu sana,sasa nimefikilia inawezekana ndio jina gumu kuliko yote kwenye blog hii na inawezekana umelipata kwenye password ya hii blogu wakati wa kutuma maoni wa pili ni emergency poison kama wewe ni kweli kutokana na jina lako pamoja na maoni yako na kufafanisha na mchezaji wa zamani wa simba Malota Soma [ball juggler]ukiingia kwenye blogu wakati imebakia dakika 15 unabalisha matokeo haya mwingine ni grill hili jina sijui umelichukua kwenye album ya nelly ft paul wall [Grill]au wewe ni mgumu wa pesa mpaka ije treka ndio maana unajiita grill.
ReplyDeleteHaya mwingine ni universe da!wewe ni mtu tokea sayari ya mars au unaishi na kufanya kazi kwenye satelite kama ndio hivyo hongera sana,mwingine ni kigerera katika jina linalofurahisha na la ajabu basi ndio hili sijui wewe ni mtu wa wapi Tz tunamakabila 150 na zaidi lakini kwenye utafiti wangu sijaona kabila lolote lenye jina kama lako sasa wewe umetokea wapi?
ReplyDeleteSUMUYAHARAKA naona umerudi siku nyingi tulikukosa maana, nilidhani utakuja na jina jipya au umebadilika kumbe bado vile vile huwezi kumaliza bila tusi. Tafsida kwako NO.
ReplyDeleteJamani nani alikuwepo UDSM wakati wa ule mgomo wa kumuondoa Mutungirey. Mnakumbuka siku ile tulivyomshusha pale Nkuruma akiwa High table. Mnayakumbuka yale mateke aliyokuwa anarusha na kwato zake. Hii picha imenikumbusha mbali.
ReplyDeleteAnony wa july 20, 2006 12:50:10 AM nashukuru umenikumbusha mbali sana siku mweshimiwa mtungilehela aliposaini cost sharing(Wale ambao hawajui kiini cha matatizo ya cost sharing ni huyu bwana) Nakumbuka alivyokuwa amelala pale mbele karibu na stage. Viti vinampiga kila sehemu.
ReplyDeletePia nakumbuka aliyorusha teke kiatu kumbe hakijakaa sawa kikaruka pia watu wakapiga ngwala chini kabisa. kama siyo dean of student huyu jamaa marehemu sasa hata na ubunge asingeukwaa.
Kipindi hicho mambo yalikuwa moto kweli, ilikuwa kweli UDSM. Nakumbuka waheshimiwa walioshiriki sasa hivi ni watu wakubwa kabisa hila mtungirehi nafikiri bado anawaheshimu make hawakuwa na mchezo. Walimtandika kweli kweli.Mpaka akapewa ulinzi wa polisi wawili wenye siraha kumpeleka darasani anafundishwa mpaka kumtoa darasani na kulinda mlango wake. Mpaka tukafukuzwa wote. Namkumbuka Mwita chacha(Commerce) sijui yuko wapi? Kayungiro(Mechanical Eng.) na wengine wengi.Hawa hawakutaka mchezo.
Yah Mtungi Rey ndio mojawapo wa watu waliosababisha hali mbaya ya elimu ya UDSM wanaopata wadogo zetu mpaka leo. Sijui sasa hivi huyu Pimbi anafanya shughuli gani hapo Tz bado yupo na huyo mzee wa Kiraracha au? Mmenikumbusha mbali kuna mtu alikuwa anaitwa Lenganasa Ole sijui nani, Mushi(wa economics), wapo wapi hawa watu? Kwa kumbukumbu nilizo nazo kwa mara ya mwisho nilisikia CHACHA kwa sasa ni mmojawapo wa senior commissioner wa Wizara ya Fedha hapo Tz.
ReplyDeleteMtungirehela alikuwa amekwaa ubunge kupitia kwa mzee wa kiraracha(TLP). Lakini safari hii(2005) alitundika madaruga baada ya kasi kumukumba(na kumkata bogi) na kumuacha karagwe, sasa hivi ni mkulima mzuri wa kahawa(haki ya nani ukifanya mabaya lazima malipo). Lenganasa huyu ni jamaa wa wa kule kwa akina busy (aliyerithi mtungirehela). Kayungiro ni mmoja wapo wa maboss BP(T) sasa, Mushi sijui yuko wapi? Huyu chacha inawezekana make huyu alikuwa anajua mambo kweli na haogopi mtu.Hila kuna jamaa sijui jina lake alikuwa mlemavu(Chemical Engineer) aliyemshika mtungirehi stage naona huyu kama bado yuko mtaani. Nilipokuwa bongo miaka hiyo nilimuona akikata mitaa ubungo.
ReplyDeleteYah huyo Engineer alikuwa anaitwa Namasaka kama sikosei. Ndiye aliyemshika Mtungi pale stage. Mpaka leo nakikumbuka kile kiatu cha Mtungi kilivyoruka wakati anarusha mateke yake. Kazi kweli kweli.
ReplyDeleteOk jamani tunashukuru michuzi maana story iliyoko hapa kwa wale ambao hawakuelewa ilitokea Mlimani UDSM, na lilikuwa tatizo la vyuo vyote Tanzania mwaka 1994(mwezi wa kumi hivi) Wakati serikali imeleta mswada wa cost sharing. Vyuo vyote vilikataa, ikiwepo UDSM bahati mbaya Mtungirehela(hii ni patented jina ya Mzee punch), jina alisi ni Mtungirehi, akiwa president wa DARUSO alisaini kwa UDSM.
ReplyDeleteChacha alikuwa Vice president. Akauza info. kuwa mkataba tayari,D. Kamala(Waziri) nafikiri alikuwa MZUMBE president wakati huo. Ulikuwa mwanzo wa Mikopo kwa wanafunzi tanzania. Na vyuo vingine vikafuata tu.
Ndio kisa kizima cha mtungihehi na polisi. Michuzi tunashukuru make kuanzia hapa ndio mwanzo mzima wa picha iliyoko pale juu na mpaka sasa hivi ni mwendo huo huo. Ni kitu ambacho wanafunzi wa wakati huo walipredict. Na mpaka sasa kinaendelea.
Asante Anony wa hapo juu umefafanua kila mtu akaelewa. Ina maana vurugu zote wanazopata vijana wa elimu ya juu bongo kwenye mikopo source ni Mtungirehela. Hivi jamani wale ambao mpo UDSM na ambao mmetoka hapo siku si nyingi MZEE PUNCH BADO YUPO AU?
ReplyDeletenafikiri Mzee punch alisambaratishwa, mwanzoni mwa miaka ya 2000.Vizazi vyenye nguvu viliisha vimebaki vizazi za siasa haviwezi kufanya hizi kazi. make zilikuwa zinafanywa na wanaume wa shoka. Yap mtungirehela alihusika kwa kiasi fulani pamoja na kwamba serikali haukuwa na njia kipindi hicho.
ReplyDeleteAnony hapo juu, hakuna cha mzee punch wala nini siku hizi, siyo kama enzi zenu chuo kimebadirika sana.
ReplyDelete