Kwa niaba ya wafiwa na familia zao, jumuia ya watanzania wa Michigan (TAMI)tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati wa upendo, ushirikiano na rambirambi zinazoendelea kutufikia kutoka pande zote za dunia kupitia njia mbalimbali za mawasiliano.
Kwa kweli upendo huu na mshikamano unatupa faraja kubwa katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Ifuatayo ni taarifa fupi tuu ya maandalizi ya kuwasafirisha Walter Mazula na Vonetha Nkya kwenda nyumbani Dar Es Salaam, Tanzania kwa mapumziko ya milele.
Makadirio ya gharama zote za usafiri na msiba (kuwahifadhi funeral home,kusafirisha Tz,tiketi za wasindikizaji, kutayarisha misa ya kumbukumbu, mengineyo) ni: $20,000 Kiasi kilichokusanywa mpaka sasa kupitia michango mbalimbali ni: $10,000 Kiasi kilichotumika (deposit funeral home, stationaries, mawasiliano, hall) ni $ 4,800 Kiasi kilichobaki kutoka makusanyo yaliopo ni $ 5,200 Pungufu kufikia lengo na gharama mpaka sasa ni ~ $10,000
Ndugu wapendwa kama mnavyoona bado tuna upungufu mkubwa kwenye kufikia lengo letu ili tuweze kukamilisha taratibu zote za kuwaaga na kuwasafirisha wapendwa wetu Walter na Vonetha. Tunashukuru sana kwa wale wote waliotusaidia na wanaoendelea kutusaidia.
Michango bado inapokelewa kupitia account ifuatayo hapa chini. Walter Mazula & Vonetha Nkya Trust Fund TCF National Bank Account Number: 6869101756 Route Number: 291070001
AU….
Rahma Baraka
Bank of America
A/c No: 003921449132
Routing:052001633
Baltimore , Maryland
Vile vile misa na kutoa heshima za mwisho itafanyika siku ya Jumamosi Sept 30, 2006 St Ives Catholic Church 29350 Lahser Rd Southfield, MI 48034-1425
Ibada – 12:45 PM – 2:30 PM
Heshima za mwisho – 11:00 AM – 12:30 PM
Kwa maelezo zaidi kuhusu michango na misa unaweza kuwasiliana na wafuatao:
Ayub - Michigan: (586) 354 5479 Brian - Michigan: (248) 730 0249 Dassu - Ohio: (614) 256 1107 Jimmy - Minnesota: (952) 393 9254
Kwa kweli upendo huu na mshikamano unatupa faraja kubwa katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Ifuatayo ni taarifa fupi tuu ya maandalizi ya kuwasafirisha Walter Mazula na Vonetha Nkya kwenda nyumbani Dar Es Salaam, Tanzania kwa mapumziko ya milele.
Makadirio ya gharama zote za usafiri na msiba (kuwahifadhi funeral home,kusafirisha Tz,tiketi za wasindikizaji, kutayarisha misa ya kumbukumbu, mengineyo) ni: $20,000 Kiasi kilichokusanywa mpaka sasa kupitia michango mbalimbali ni: $10,000 Kiasi kilichotumika (deposit funeral home, stationaries, mawasiliano, hall) ni $ 4,800 Kiasi kilichobaki kutoka makusanyo yaliopo ni $ 5,200 Pungufu kufikia lengo na gharama mpaka sasa ni ~ $10,000
Ndugu wapendwa kama mnavyoona bado tuna upungufu mkubwa kwenye kufikia lengo letu ili tuweze kukamilisha taratibu zote za kuwaaga na kuwasafirisha wapendwa wetu Walter na Vonetha. Tunashukuru sana kwa wale wote waliotusaidia na wanaoendelea kutusaidia.
Michango bado inapokelewa kupitia account ifuatayo hapa chini. Walter Mazula & Vonetha Nkya Trust Fund TCF National Bank Account Number: 6869101756 Route Number: 291070001
AU….
Rahma Baraka
Bank of America
A/c No: 003921449132
Routing:052001633
Baltimore , Maryland
Vile vile misa na kutoa heshima za mwisho itafanyika siku ya Jumamosi Sept 30, 2006 St Ives Catholic Church 29350 Lahser Rd Southfield, MI 48034-1425
Ibada – 12:45 PM – 2:30 PM
Heshima za mwisho – 11:00 AM – 12:30 PM
Kwa maelezo zaidi kuhusu michango na misa unaweza kuwasiliana na wafuatao:
Ayub - Michigan: (586) 354 5479 Brian - Michigan: (248) 730 0249 Dassu - Ohio: (614) 256 1107 Jimmy - Minnesota: (952) 393 9254
Mahakama Kisutu yambana Mahita
ReplyDelete2006-09-28 08:54:49
Na Hellen Mwango na Rosemary Mirondo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku 19 kwa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP) Omar Mahita, kuwasilisha utetezi wake dhidi ya madai ya kutomtunza mtoto wake.
Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mtumishi wake wa ndani, Bi. Rehema Shabani, mkazi wa Jijini Dar es Salaam, anayedai kuzaa na Bw. Mahita.
Kesi hiyo namba 2 ya mwaka huu, iliyofunguliwa Agosti 10, imesikilizwa jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Bi. Pellagia Khaday wa Mahakama hiyo.
Mdaiwa ambaye aliwakilishwa na wakili wake Bw. Charles Semingalawa, aliiomba mahakama kutoa tarehe ya kuwasilisha majibu ya utetezi wa madai hayo, kwa kuwa mdaiwa yuko safarini.
Hata hivyo, mahakama ilikubali ombi la upande wa mdaiwa na kutoa siku 19, ambapo Oktoba 16, mwaka huu, unatakiwa kuwakilisha utetezi huo.
Hali kadhalika, mahakama hiyo pia iliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 17, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Katika madai ya msingi, inadaiwa kuwa Mahita alimtelekeza mtoto wake mwenye umri wa miaka minane bila kutoa matunzo.
Madai hayo, yalifunguliwa na mwanamke huyo kupitia Kituo cha Haki za Binadamu cha Jijini Dar es Salaam.
Katika hati ya madai mwanamke huyo alidai kuwa Juma Mahita ni mtoto halali wa mdaiwa.
Pia aliiomba mahakama hiyo itoe amri ya kumtaka mdaiwa kutoa Sh. 100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto huyo.
Aidha, alidai apewe Sh. 100,000 kila mwezi za matunzo ya nyuma tangu mwaka 1997 hadi kesi itakapomalizika.
Bi. Rehema alidai mahakamani hapo kuwa uhusiano wake na mdaiwa ulianza Mei hadi Oktoba 1996 huko mkoani Kilimanjaro, wakati akiwa mtumishi wa ndani wa Bw. Mahita.
Mdai alidai kuwa, wakati huo Mahita alikuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo(RPC).
Alidai kuwa katika kipindi hicho cha uhusiano wao, alipata ujauzito ambapo mdaiwa alimtaka kuondoka na kurudi kwao Kondoa mkoa wa Dodoma, ili mke wake asijue.
Hati hiyo pia ilieleza kuwa mdai alipewa Sh. 40,000 na kuahidiwa na mdaiwa kutumiwa fedha za matunzo kila mwezi.
Pia ilidai kuwa mdaiwa alijifungua mtoto huyo mwaka 1997 na alipewa jina la Juma.
Hati hiyo ilidai kuwa mdaiwa hakupinga ujauzito wala mtoto huyo, ila alimtaka mdai kufika nyumbani na ofisini kwake kudai fedha za matunzo.
Hata hivyo, Bi. Rehema alidai kuwa mdaiwa hakupeleka fedha za matunzo ya mtoto kama alivyoahidiwa na mwaka 2003, walijaribu kujadili naye katika ofisi za Ustawi wa Jamii lakini juhudi zake hazikufanikiwa.
Hati hiyo ya mashtaka iliendelea kudai kuwa, mdaiwa alimtuma askari wa kikosi cha kutuliza ghasia aliyemtaja kwa jina moja la Peter na mtumishi wa ndani aliyemtaja pia kwa jina moja la Hussen, ambao walimchukua mtoto huyo bila idhini yake na kumpeleka sehemu isiyofahamika.
Aidha, iliendelea kudaiwa kuwa mdai baada ya kufuatilia mtoto wake aliko alikamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Kati, kwa madai kuwa ametenda kosa.
Ilidaiwa kuwa mwaka huu mdai alipeleka shauri hilo tena Ustawi wa Jamii, lakini mdaiwa hakuwa tayari kumaliza nje ya mahakama ndipo akaamua kulipeleka mahakamani.
Shauri hilo limeahirishwa hadi, Oktoba 17, mwaka huu itakapotajwa tena.
Wakati huo huo, baada ya shauri hilo kuahirishwa, Bi. Rehema aliomba msaada wa nauli kutoka kwa wasamaria wema.
Aliomba nauli hiyo ili iweze kumfikisha yeye na mwanaye anayesoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mwongozo, aweze kuhudhuria masomo baada ya kutoka mahakamani.
Waandishi wa habari waliokuwepo mahakamani hapo, walilazimika kupitisha mchango wa dharura na kufanikiwa kupata Sh. 5,000 ambazo walimkabidhi mwanamke huyo.
Wakati huo huo, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Abdallah Zombe, leo anatarajiwa kufikishwa mahakamani dhidi ya kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wanne.
Kesi hiyo imehamishiwa Mahakama Kuu ya Tanzania.
SOURCE: Nipashe
tuna uchungu lakini isiwe ikawa biashara £20,000 ni maisha bongo.
ReplyDeleteInatuuma sana juu ya kifo cha vijana wetu wapendwa, lakini US$20,000 mbona ni nyingi sana....Hebu toeni mchakato mzima hadi kufikia ghalama hizo.Kwenye msiba kutoa ni moyo
ReplyDeleteanony wa 12:48 na 11:10 neno ni gharama na siyo ghalama, kama unaishi Marekani au Canada hili suala liko wazi kabisa kusafirisha maiti unahitaji at least dola elfu saba kwa mtu mmoja, kumbuka ni watu wawili,elfu kumi na nne, mpaka hapo, kuna gharama za funeral home, at least, dola 3000 mpaka 5000, ambayo imezidi hata hiyo 20,000 uliyozungumzia, na msibani watu hawakai wakaaangaliana na kulia tu hata nyumbani Tanzania kumbuka,kutakuwa na watu kutoka sehemu tofauti za US na Canada, na haya ni makisio ya karibu tu, na kwa taarifa yako mimi sihusiani na hao watu kwa aina yoyote zaidi ya kuwa Watanzania wenzangu, lakini sitokaa nihoji, nitatoa niwezacho, kwa hiyo ndugu kama mtoaji toa kama siyo kaa kimya , sababu kwanza ni ANONY hivyo basi hamna atayekusimanga fulani hajatoa mchango, sawa ndugu? kila la heri.
ReplyDeleteAhsante ndugu hapo juu kwa jibu lako unajua watu wanasema tu hayajawakuta ndio maana siku zote ngoma isikie ikilia kwa mwenzio ikilia kwako kelele ndio hayo sasa hiyo 20,000 ndogo sana mbona jamani tutoeni tuwe pamoja leo wenzetu hawa kesho sisi hatujui lini na sababu ipi itatupeleka huko kwahiyo mwenzio akinyolewa wewe tia maji.
ReplyDeleteJamani ndugu wanaohoji mbona tunakuwa hivyo jamani, halafu tunafananisha na bongo sawa hiyo hela ni maisha bongo lakini kwa babati mbaya hawa watu wamefariki huku na kwa watu wote tunajua gharama za kuzishi huku sio ndogo sasa unataka upigiwe hesabu vipi.
ReplyDeleteKama ni mtoaji wala huwezi kuuliza hayo mambo nyie mnaotoa hayo maneno sidhani wala kama mna nia ya kusaidia mnataka kuwapotezea watu muda wa kuanza kuandikia mlolongo wa matumizi halafu wala msitoe, mimi kama rafiki wa familia japo najua kwamba tunahitaji hiyo hela lakini hatuwezi kukaa na kuomba na kuwapa watu kama nyie kuhoji kama tunashida hivyo kama ni mtoaji utatoa bila huu upuuzi kwa nyie wengine ngojeni shida ifike kwenu ndioo mtaelewa na kumbuka GOD DONT LIKE UGLIES, cheza na kazi ya mungu kama vile wewe una mkataba wa kutopata matatizo
Kutoa ni moyo usembe si utajiri.
ReplyDeleteNyie wala msijisumbue kujibu watu wa namna hiyo. Waacheni tu, sisi tufocus kwenye kusafirisha miili ya ndugu zetu. Watu wengi wanaelewa costs za mazishi Marekani na wanaoelewa hawaulizi, so achaneni na hao watu wasi na huruma.
ReplyDeleteR.I.P Walter and Vonetha. You'll forever be missed!!
h
ReplyDeleteYaani nyie wabongo wa USA mnataka kuniambia mlivyojazana huko na mnavyodai mnapata 20,000$ a week, yaani hiko chama chenu hakina hata hela ya kusafirisha maiti?
ReplyDeleteIla hela ya kujirusha, kufanya maparty na kuishi kwa fantansy ipo.
Wakati kawaida chama kinakuwa hela kama hiyo ya immergence, iko ready, mchango wenu na wa embassy, unaenda kwa wafiwa pamoja na msiba nyumbani.
Haya mnalo hilo! Midomo fyaa! Mnatuonyesha wenyewe! Halafu tukisema oooh, kunde, choroko, wivu, tunaomboleza, nyanya, kitunguu, bla, bla, bla, na msimzike huko tutawalaani kufa!
Anony wa 8:27pm, whats your problem? mbona nyie watu hivi jamaa? una bahati sana , kwanza nimefunga,pili ni msiba,but even with that it doesnt change the fact that probably on the most disgusting day god made heartless idiots like you.
ReplyDeletesasa ukileta tena upumbavu tutaweka msiba, ramadhani, nini sijui pembeni, tuendelee na mambo mengine kama inavyokuwa siku zote,ustaarabu ni kama shati tu unavua na kuvaa kiurahisii....ISHAKUWA UJINGA SASA!!!
anony wa 8:36 kama vile una point.jamaa walijitapa wenyewe kwamba wanavuta dola 20,000 kwa wiki sasa kwanini hicho kiasi kupitia mchango kinakuwa shida kiasi hicho mpaka mnafikia kutoleana maneno machafu ili hali ni msiba?jamani toeni hizo dola tuwazike ndugu zetu nyumbani
ReplyDeletehamna mtu aliyesema juu ya 20000 kwa wiki kama nakumbuka kulikuwa na wakina dada walidai wanaingiza 2000 kwa wiki na hata kama ni kweli japo ni matata hata hiyo lakini still haina maana kwamba ni lazima watoe hela zote wenyewe.
ReplyDeleteKwa mfano kwani bongo watu wangapi wanaiba na kuwa na mamilioni ya hela kwenye account, lakini arusi za milioni nne tano bado zinachangiwa ama nadanganya, so kama una akili timamu utakubali kwamba sio kwamba watu hawana hiyo hela lakini utatumia vipi hela yote kwa ajili ya mtu kwa ajili ni mtanzania mwenzako tu, acheni hivyo jamani kwanini lazima mtu uongee kitu kama vile kuna mashindano ya walio bongo na walio huku tumieni mida yenu kufanya na kuongea ya maana basi
Hi everybody,
ReplyDeletekwanza kabisa napenda kutuma rambi rambi zangu kwa wanafamilia zote mbili kwa msiba mzito..poleni sana na Mungu atawapa nguvu na faraja..Amen
Then secondly,kwa wabongo wote wale wenye kutoa maneneo ya kishenzi kwenye hii blog ya maana na yenye wingi wa rehema ya ustaarabu cos mwenye nayo siyo chizi.
Hahahahhahahah,eti mmesahau msemo ule wa SIBAGUI SICHAGUI ATAKAYENIZIKA SIMJUI,zingatia hili katika maisha yako yote ya pumzi za bure za Mungu.
kuhusu kuchanga hata ukichanga ama usipochanga ni hiari yako,tena bora usichange kabisa maaana unaweza kutoa hela haramu kwa wahusika ,nikiwa na maana kuwa hela za wizi za wazungu toka kwenye credit cards zao,ama za longo longo ama za manung'uniko sasa ni heri kukaa nazo mwenyewe ili kuepusha Nuksi kwa marehemu na wafiwa..
Jamani kweli wabongo wa ughaibuni ni watu wa kujisahau sana sana ,nimeamini hilo KWANI MMNAVYONG'ANG'ANIA huko mtazani mna ubia napo wakati wenye nchi hawawataki hata,visa zenyewe mpaka mwende kwa Kalumanzira sasa umepata bahati ya kuja huku bado unaleta NYODO,Kweli fadhila fadhilata,na punda wa pundata...kurudi kwenu hamtaki hata kidogo na je MNA MKATABA NA MUNGU KUWA MTAFIA WAPI??? sasa kama unataka teh rest of your life iwe huko je UTAKUFA WAPI??NA KUZIKWA WAPI???au mmetengeneza masafe ya kuhifadhi hela za MIILI YENU NA HIZO FAMILIA ZENU TAYARI..watch out siyo mnaropoka tu kuonekana kama unajua kuongea kumbe pumba tupu.si ajabu muongeaji wa kuponda kuhusu kuchanga na mambo mengine hapo wewe ndio wa kwanza katika UKOOO MZIMA WA BABA NA MAMA kwenda ughaibuni na ndio TEGEMEO NA MAJUKUMU yamekupanda hadi yanakuzeesha sasa NDIO MAANA UKIAMBIWA MCHANGO maneno yanakutoka kama chiriku....acha upana kama picha ya Xray ndugu yangu,wewe changa kama unaweza huwezi acha na funga bakuli lako,kutoa ni moyo usambe si utajiri ,leo kwao ,kesho kwako na kwangu...
Naomba kuwauliza hao ma against ,je katika familia walizoziacha Bongo hakuna waliokufa akashindwa kuja kuwazika ???NI WENGI,wapo tunaowajua wamefiwa na wazazi bab na mama na wameshindwa kurudi kuja kuwazika,either mambo ya Vibali ama nauli,....sasa ishi na watu vizuri uvae viatu...na ongea na watu vizuri upate vya watu.....sasa watu ukiwaomba watashindwa kukusaidia....na hii point inaonyesha jinsi gani mpumbavu anavyoshindwa kusave na kushindwa hata yeye kuja BONGO KUZIKA WAZAZI WAKE ,......SASA ATAWEZA KUTOA MCHANGO KWA MWINGINE KWELI ,NAKATAAA HAPA ATAKACHOWEZA NI KUTOA MANENO KASHFA NA KEJELI MCHANGO MSAHAU...MAANA HATA YEYE KUJIKIMU NA MAISHA NI NGUMU SANA KWAKE ,JE KWA MWENZAKE ATAWEZA??????THUBUTU sasa ndio kama tunavyojionea kwenye blog hii upande wa maoni,na mtu mwenye akili tu utapata jibu kuwa huyo uwezo hana...
ila Mungu awasaidie sana na pia msome kweli siyo mambo ya kuhang hang kwenye kazi zisizo na future wala proffesional,ukiulizwa niko chuo,mwaka wa 5 sasa kumaliza humalizi hakuna hata CERTIFICATES ulizowahi kuwasilisha nyumbani(bongo) watu wakajua kuwa unasoma ,starhe na wewe wewe na starehe,mabinti,wanaume ndio zenu,jamani msitake kuumbuaana humu,kwani watu wako kila kona ulipo wewe kuna mwenzako ufanyacho anaona na anajua sasa mkileta za kuletwa tutawatoa nishai ...bora mnyamaze tu ...someni pateni vyenu then Nendeni ama Njooni home mjinge nchi yenu...kazi kuibondea nchi yenu na kuendekeza utumwa tu ,na kuwasahau wazazi wenu,bila wao ULAYA ama USA mmngeijua nyinyi aaacheni dharau na majigambo yamepitwa na wakati....mrudi mfanye maendeleo ...kwani maendeleo ya Nchi yanatokana na Wananchi Wenyewe,siyo mnarudi na mabegi ya nguo tele na kuja kujirusha billicanas na viwanja vingi vya DAR na kutaka umaarufu wa kuwa umetoka ughaibuni watu wanawaona Mafala tu na wabongo wanapenda mteremko wanakuchuna ukiondoka wanakuona huna maana ,Angalau MJE MJENGE AMA KUNUNUA NYUMBA HUKU MAANA UGHAIBUNI NYUMBA HAMNA NA BONGO NYUMBA HAMNA SASA NYINYI MMEKUWA NDEGE MTAISHI KWENYE VIOTA HEEE MNACHEKESHA BASI,sasa kama mna akili kaeni mfikiri.NA NAWAKUMBUSHA KUWA KUFIWA HAKUNA MMOJA NA HATA HUKU TUNACHANGIANA SANA MAANA NAAMINI KATIKA KILA MBONGO ALIYEKO HUKO AMA HUKU HAKUNA NDUGU YAKE AMBAYE HAKUFA UKIMWI NAKATAAA KWANI UKIMWI NI JANGA LA TAIFA, SASA NAWEZA KUWA NIMESHAWAHI KUCHANGA AMA WEWE AMA NDUGU ZAKO WAMESHACHANGA KWENYEE FAMILIA ZETU KWA AJILI YA MSIBA.....SASA KUTOA NI KAWAIDA BLAA BLAA MPUNGUZE...
JAMANI TUELIMIKE TUTACHEKWA NA WATU SANA KWA UPUMBAVU NA UJINGA TULIONAO WABONGO HATUFANYI KITU BILA MAJIBIZANO..HATUKO WELL ORGANIZED MWEEEE,LINI NA SISI TUTAKUWA FRESH...YAANI TUFANYE KITU BILA KUHOJI...
POLENI WAFIWA SANA NA MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. NA AWASAMEHE WALE WOTE WASIOJUA WALITENDALO MAANA NAO HAWAJUI SAA WALA SIKU...ZAIDI YA BLAA BLAAA NA NYODO.
AMEEEN.
mshikaji hapo juu umesema ukweli ila umezidi mipaka chonde mzee au dada usiseme kila kitu jus keep beneath your heart
ReplyDeleteAnony 9:26 Am Kasema Ukweli sana safi sana napo soma mtu anaweka vitu wazi kama hivi,maana watu awapendi kuaccept reality.Hii ndiyo hatua moja kama kila mtu akiiweka maoni ya huyo jamaa(september 29,2006 9:26 AM in considerations na kuyafanyia kazi ndiyo mwanzo wa ujenzi wa Taifa letu.
ReplyDeleteMzee wangu hapo juu 9.26 umeelezea kiurefu japo umechanganya mambo mengi lakini kuna ukweli umeutoa juu ya wabongo tulivyo.
ReplyDeleteTatizo moja watu wanashindwa kutofautisha hili, kama kulivyo kokote kuna wapuuzi wako huku waliokuja kupoteza muda wao, lakini vilevile tuko watu wenye akili zetu tunaojua tunafnya nini na kujaribu kujiboresha kila siku. Sasa ukianza kufanya kama unaongea na watu wote walio nje ya nchi kwamba ni wajinga na hatuna cha maana tunachofanya utakuwa unakosea na hayo mashindano sidhani kama kuna haja yake, kwa sababu japo kweli kuna watu wako huku wakiishi maisha ya kujirusha kila siku lakini ukweli ni kwamba atleast mtu anajua anacho kinachoingia kufananisha na bongo ambako watu wako kila siku baa kunywa bia za kuomba.
So angalau kama unatoa point kama zako mzee hapo juu wa 9.26 tofautisha basi watu na usichanganye watu wote kama ambavyo hautataka tukujumuishe na wale wapuuzi wa misheni town bongo na wewe.
Kama watu walivyosema mapema tujishughulishe na yalio muhimu kwa wakati huu, kwani kama ni mtanzannia mwenzangu utakubali kwamba hii kitu inaweza kumfikia mtu yoyote kama ilivyokuwa bahati mbaya kwa ndugu zetu hawa, tuweni na moyo wa kibinadamu basi
Jamani wabongo ni jambo la msingi tukijifunza au tukijijengea utamaduni wa kuheshimu maamuzi ya watu itatusaidia sana.Kuingilia utaratibu au mtindo wa maisha ya mtu na kuanza kuhoji ni uhaba wa fikra!Nasema haya nikilenga mijadala iliyokua ikiendelea humu bloguni.kuna mvutano kati ya waliokua ngambo na wale walioko nyumbani! yote haya yameletwa na watu wasiojua kuheshimu taratibu na maamuzi ya watu mtu akiamua kwenda ulaya na kusafisha vyoo ili arudi nyumbani kutesa hayo ndio malengo yake na akiyatimiza basi kwake maisha ni mazuri na yenye furaha si lazima afuate utaratibu au mtindo wako unaofikilia wewe kua ndio mafanikio maishani au mtu akiamua kukaa bongo na kua kondakta akifanikiwa ktk hilo, basi ndio maamuzi yake tuyaheshimu! tungekwenda kwa mtindo huo matusi yote yasingejitokeza. Wengi wetu ni duni kwakua hatuangalii malengo yetu tunataka kufuatilia mambo ya wengine!Nina mengi ya kuwaeleza watanzania wenzangu ila yanaweza kujaa kitabu mwenye akili na aelewe! tusipoacha haya tutakua duni milele na milele amina!
ReplyDeleteALOO ANON 8:36 BIG UP!aibu wa2 wazima.na mungu kaamua kuwaeleleza na midomO yao ya chuchungi.misifa mingi hamna lolote!asie jua wanakula joto ya jiwe huko marekani nani?Maisha magumu ila wanaamua kufurahisha midomo yao...ooooh petha ipo!mnajirusha roho wenyewe.Na mwenye pesa hata cku moja ndugu zangu hajigambi,unless kama huyo m2 ni maskini sana,na ndo uwaga kuna msemo maskn akipata matako hulia mbwata!action jamani, action action ,action ,action,tuonyesheni mna delay mno hata mkisema mchangamke sasa 2late maana mmejiabisha kupita maelezo.
ReplyDeletepoleni wafiwa wote,
mola awapunguzie adhabu ya kabri marehemu wetu!hii ni kwa wale wenye visebengo!tuko pamoja ktk sala.
AMEN
we anon 4:40 kama ulikua unaona wosia haukuhusu si ukae kimya na kuendelea kutafakari vilivyo bora kwako,kuanza kujikomba tena ohh amimi asio ayule.inahusu?????nyie ndo wale wanaopoteza muda huko ila hamtaki kukubali ukweli coz najua ukweli siku zote unauma.
ReplyDeletemungu azilaze roho za marehem pahali pema peponi.
AMEN
MUNGU WALAZE MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI ...AMEN.
ReplyDeleteAIBU, AIBU, AIBU, AIBU, AIBU, KWA WATU WA MAREKANI! ANONY WA SEPT 28, 8:27 AMEWAPASHA, PENDANENI, SHIRIKIANENI, JIFUNZENI KUTOKANA NA HILI KOSA AMBALO SIO SIRI KWENU LIKO WAZI.
HATA KAMA MNA WIRE HUKO LAKINI, HELLOOOH! SAFIRISHENI MAITI HIYO. NA KUANZIA LEO WACHENI UONGO! UZENI UZENI KALENDA HIZO, PIGENI PIGENI VIFAGIO HIVYO, BAMIZENI MIZENI, WANAWAKE UZENI UZENI URITHI WA BIBI HUO, WHATEVER MTAKAVYOFANYA, IT DOESN'T MATTER SAFIRISHENI MAITI HIZO.
N:B NAJUA HAMKOSI KUNDE CHOROKO....MNAKARIBISHWA.
ANONY WA 9:26 AM NA MWENZAKE WA 7:11 PM mmejitahidi ku-analyse hili suala la watu kutoa majivuno ya hapa na pale yasiyokuwa na msingi wowote.Ni sawa kupanga ni kuchagu lakini kwa kuishi Marekani hilo siyo jambo la kuringia sana kwani maisha ni popote pale.Kwa kuwa tupo msibani si vema haya malumbano yakaendelea ila cha msingi nyie ndugu zetu mlio huko mnakokuita ughaibuni na kutuambia mna maisha ya raha fanyeni haraka(samahani) muisafirishe hiyo miili ya ndugu zetu kwa ajili ya maziko katika ardhi ya TZ.nI KWELI DOLA 20,000 si hela ya kubeza inahitaji ushirikiano lakini kwa kipato cha dola 2000 kwa asilimia kubwa ya walio ughaibuni naamini hicho kiasi si suala la kusumbua vichwa na kutukanana humu globuni.Mwenyezi Mungu wapumzisha marehemu wetu kwa amani.
ReplyDeleteWell kwa nyie mlioko bongo ambao mnataka kujiingiza kwenye majibishano ya kwamba wapi ni bora tuache kujidanganya na soma haya ukikubali sawa kama unaona sio sahihi poa pia but atleast soma wkanza.
ReplyDeleteKitu cha kwanza cha kuzingatia hata utake kusema nini juu ya bongo ukweli ni kwamba kwa ijana wengi maisha ya kukaa na kufanya miseni town ni ya hatari, kazi za ofisini hazipatikani na option inayobaki ni kutafuta maisha bora mengine duniani,mtakubali kwamba style hii ya kukimbia TZ ilisababisha watu wengi waanze kuzamia meli kwenda SA, na Europe.
Miaka ilivyozidi kupita na maisha hayabadiliki vijana wengi tukaanza either kuja kusoma nje,kuondoka kiskaut, au hata kuonga serikalini ili waje na msafara.
Lakini ukweli ni kwa nini watu waliondoka bongo ni kutafuta maisha bora zaidi pengine, sasa wewe baada ya kupata nafasi ya kutengeneza $2000 kwa mwezi au zaidi,utamwambia vipi mtu kwamba ni mjinga kwa kuosha vichaa au kupaki maboksi atleast anafanya kazi yenye uhakika na yenye kumpatia kiasi cha kutosha kuliko wewe uliye TZ na kufanya kazi miaka nenda rudi bila kuwa na la maana kwa ajili ya kulipwa $100 kwa mwezi.
Juu ya ndugu zetu kusafirishwa na kuzikwa bongo, sio ukweli kwamba watu hawawezi kupata hiyo hela tatizo ni kwamba wabongo hatuna subira, maneno yote hayo yalianza wakati ndio kwanza watu wamepata habari, lakini michango imeingia na tunamsafirisha mTZ mwenzetu kama ilivyo pangwa na hela imepatikana within week moja.
Sasa kwa wale wanaotaka kufananisha maisha ya huku na hayo ya bongo hii ni test moja kubwa tu, kwa mfano tungechukua watu kama 5000 wanaofanya kazi nzuri tu TZ na kuomba wachange milioni 20 within a week ni kiasi gani tungepata, ukweli ni kwamba sema utakavyo ukweli ni kwamba hela na uchumi wetu ni mdogo sana kuwatisha watu kwamba maisha ya huku sio bora kuliko hukonjoo ukae kwa mwaka na uone kama hautaona ninayoyasema
Eeh anony wa juu,
ReplyDeleteNilitaka kumleta mdogo wangu aje huko USA lakini umenistusha, asante sana.
Huku huo mshahara ni social help ya bure ya single person bila mtoto after taxi. Ukiwa unafanya kazi ya kawaida tu unapata double ya hiyo. Plus matibabu na elimu ni bure huku.
Anyway hata viongozi wenu wakijaga huku wanashangaa, wanasema Scandinavia kuna the best FAIR system in the world.
Na believe me nobody is homeless...only by willing, noboby over 18 get less than 1,800US$ a month! Is illegally here.
Anyway system za nchi ziko tofauuti niliona nilivyokuwa huko watu wanaishi kama Africa wengine.
we hapo juu, first of all go learn some proper english, if you can't write then andika kiswahili maana mambo ya "ilegally" sijui ndio nini. Pili, kama umeona watu wengi wanaishi kama Africa then tembea uone, you seem to be hanging out with the wrong crowd.
ReplyDeleteHe hanged out with the wrong crowd indeed Goddamnit! huko Scandnavian countries si mnajilipua tu, kwa jina jingine wengi wenu ni wanariadha a.k.a wakimbizi wa kujitakia, mnakaa makambini.
ReplyDeleteSi uende kwenye net uangalie statistic ya wakimbizi Scandinavia uone weusi ni wangapi.....Nikijaga huko kwenu likizo, wazungu wanatupapatikia wanaona "wazungu real" wameingia watatengeneza pesa.
ReplyDeleteNightclub zote California e.g malaya wakijua tu mgeni unatoka Scandinavia hata kama mweusi kama mimi kumamae wanakupapatikia wanajua wamepona, England, France wote mavi yenu mdomo tu! Mna dhiki sana! Wazungu wenyewe wanakubali lakini nyie eti mnatetea kama kwenu!
Usilolijua litakusumbua, wabongo wangapi tunao huku hawataki kurudi huko?
Tetea Tanzania nchi yako, sio nchi ya wenzio, mnakufa na kamba shingoni babae!
vijana wenzangu wa kitanzania,mnatia aibu!!!!badala ya kufatilia mambo ya msiba mnaleta chuki zenu binafsi , hasa nyinyi mlio huko bongo mna chuki binafsi!!!si mkubali tuu,mnababaishwa na wabongo wachache wanaojigamba lakini mnasahau some of us , tupo nje ya tanzania na tunasoma tunapata best education, sio kama nasema education ya huko mbaya lakini na kugoma huko watu wanakogoma sijui mnasoma lini!!!mmezidi kuwasema ndugu zetu wa US at the same time hao hao mnawapigia simu kila leo kuwaomba msaada wawaletee hela,by the way kazi ni kazi mtu akipata haki yake anayostahiki ni bora kuliko kukaa kijiweni, inabidi kwanza mnyamaze mfanye maendeleo sio kutukanana, matusi hayasaidii chochote, na ukweli ni kwamba wengi wenu mngependa muende huko US mpate hizo hela na nyinyi mtese!!!!kwanza mnakaa kijiweni na mishen town zisizo na mpango, amkeni mfanye mambo ya maendeleo!!!!!!!
ReplyDelete