Home
Unlabelled
mama lao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Bibi Titi alikuwa ni moto wa kuotea mbali. Kiongozi hasa aliyepania kulitumikia taifa lake kwa moyo na si kwa fedha.
ReplyDeleteHUYU NDIO THE ONLY ONE -A TZ WOMAN FIGHTER, YEYE NDIO KAPIGANIA KUTOA KUTI KWENYE MANYUMBA ZA WATU, NA HAKI YA MTOTO NA MWANAMKE, SEMA TU WALIM....."MABLACKMAN" KUONA ANAKUJA KWA KASI, KWANI MIDENDA NDIO ILIKUWA INAWATOKA KWA UCHU WA WIZI YA MALI YA UMMA!!! NA WALIFANIKIWA KWELI KUBLOCK, MPAKA LEO SI MNAONA WENYEWE WALAJI NI WALE WALE!!!!!!NA WAHOI NI WALE WALE WANAIBUKA KWA DHAHARI TU MASIKINI!!!!!
ReplyDeleteNilikuwa na bahati ya kuongea na Bibi Titi kabla hajafariki. Nilivyokuwa naongea naye, nilihisi ana huzuni fulani.
ReplyDeleteBahati mmabya kisomo chake kilikuwa kidogo na watu walimtumia, hasa ile jaribio la kumpindua Nyerere enzi zile. Na naomba mnisahishe kama nimekosea.
Bibi Titi alisema Bungeni, "We want fire in Magomeni, fire in small bottles!' (Yaani tunataka umeme Magomeni)
Ndo Nyerere kasema Bungeni waongee kiswahili.
Tukumbuke mema aliyofanya marehmu Bibi Titi. Ni mmoja wa mashujaa wa kike wa Tanzania.
BIBI TITI OYEE!
ReplyDeleteKusema "we want fire in magomeni" siyo kosa, ili mradi ujumbe uliwafikia walengwa.
ReplyDeleteHivi siku hizi wanawake wa hivi Bongo kwa nini hakuna? Kwanini hakuna wanawake wana "Siasa"? samahani sizungumzii wabunge hapa.
Sisi wanaSiasa tunakosa wake wa kuoa kwa sababu hatukutani na wanawake wanasiasa.
Jamani hivi hamuoni sasa hivi tuna kizazi kipya AMINA CHIFUPA wa MPAKANJIA, huyu ni koto wa kuotea mbali
ReplyDeleteHuyu Bibi na pia Kawawa ,watu walipenda sana kuwatungia matani. Huyu mama matani yake yalikuwa yajisi asivyotumia kingereza sahihi, halafu Kawawa maswala ya manners. Sidhani kuwa ni ukweli huyu mama alikuwa anachemsha kiingereza namna hiyo .Na sidhani kuwa ni ukweli yale ya Nyerere kumuambia Kawawa funika kikombe yote yalikuwa ni ukweli.
ReplyDeletekuna mdau wa blogu hii kaniletea hii leo...
ReplyDeleteKUTOKA MAGAZETI YA ZAMANI
Kesi ya uhaini:
Mkurugenzi aendelea kutoa ushahidi
Uhuru, Jumamosi Agosti 1, 1970
"KATIKA mkutano huo, Kamaliza alimshauri Leballo aende London kwa Kambona kumwomba atume fedha zaidi, Kamaliza alimtaka Chipaka amwandikie barua Kambona na kumtumia noti ya shilingi 10/- ili Kambona aitie saini ije isaidie katika kuwashawishi Wabunge na baadhi ya mawaziri kumuunga mkono Kambona.
Noti hiyo pia ilikuwa isaidie katika kuchangisha fedha za mapinduzi na kuwashawishi watumishi wa TANU na NUTA kuipinga serikali.
"Kamaliza alimwambia Leballo kuwa hakukuwa na shaka wafanyakazi wa Tanzania wangeliunga mkono mpango wa mapinduzi kwa sababu Rais alikuwa amemwondoa (Kamaliza) kutoka NUTA kinyume cha matakwa ya wafanyakazi.
"Leballo alikutana na Bibi Titi nyumbani kwake tarehe 23 Juni na Titi alimweleza kwamba alikuwa amekwenda Nairobi kwa muda wa siku nne na kwamba alimpigia simu Kambona kutoka Nairobi na kumtaka atume shilingi 1,000,000/- kwa ajili ya mapinduzi katika muda wa wiki mbili.
"Titi akampa Leballo shilingi 400/- na kusema kwamba alikuwa amepokea shilingi 2,000/- kutoka kwa Kambona, 1,000/- za Chacha kwa matumizi madogo madogo. Titi alimwambia Leballo atampa shilingi 600/- baada ya siku chache na alifanya vile tarehe 26, Juni". Fedha hizo zilitolewa mahakamani kama ushahidi kamili.
"Tarehe 28 Juni Chacha alipanga kukutana na Leballo tarehe 30 Juni ili amjulishe Leballo kwa Meja Herman.
"Chacha na Luteni - Kanali Marwa walikwenda nyumbani kwa Leballo tarehe 30 Juni saa 3 usiku. Chacha na Leballo walikwenda katika chumba cha kulala na kumwacha Luteni - Kanali Marwa sebuleni. Huko chumbani Chacha alimwambia Leballo kwamba alikuwa tayari kuipindua serikali kama angelipwa shilingi 20,000,000 na akamtaka Leballo amwambie Kambona atume fedha hizo kwa haraka.
"Leballo na Chacha walikutana tena tarehe 3 Julai huko makao makuu ya Jeshi kwa maombi ya Chacha. Chacha alimwambia Leballo kwamba alikuwa amesikitishwa na ukawiaji wa fedha.
Akamtaka Leballo aende huko Lugalo katika bwalo la maafisa ambapo Kapteni Lifa Chipaka atamjulisha kwa Meja Herman.
"Leballo alikwenda kule, akamkuta Kapteni Lifa anamsubiri. Kapteni Lifa alimwambia Leballo kwamba hakuwa anamwamini Meja Herman katika mpango wa mapinduzi kwa sababu alikuwa Chotara kutoka Iringa na kwamba yeye angempa orodha ya maofisa ikiwa pamoja na jina la mtu mmoja kutoka kisiwani. Kutoka kwenye orodha hiyo mtu wa kuongoza mapinduzi angechaguliwa. Baadaye Kapteni Lifa alimfahamisha Leballo kwa Meja Herman.
"Baada ya mkutano huo Leballo alionana na John Chipaka na Kamaliza wakiwa pamoja katika ofisi ya shirika la wafanyakazi la NUTA. Wote walizungumza na kumtaka Leballo aende London kwa Kambona kumtaka atume fedha zaidi.
"Kama saa kumi na robo alasiri siku hiyo Leballo aliitwa tena kwenye ofisi hiyo. Aliwenda na kumkuta Kamaliza peke yake. Kamaliza alimwambia kwamba alikuwa amemtuma mtu mmoja kwa Kambona "U That" akalete fedha.
"Kamaliza akamwambia Leballo kwamba yeye alipendelea Meja Herman aongoze mapinduzi kuliko Chacha".
Washitakiwa saba ambao wamekana mashitaka matatu ya uhaini na moja kuficha siri ya uhaini ni Gray Likungu Mattaka, John Dustan Lifa Chipaka, Bibi Titi Mohammed, Michael Marshal Mowbrya, William Makori Chacha na Alfred Philip Millinga.
Kesi inaendelea Jumatatu asubuhi.
--------------------------------------------------------------------------------
Kiwanuka hataki kuhama nyumba ya serikali
Mwafrika, Ijumaa Oktoba 5, 1962
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Uganda, Bw. Benedicto Kiwanuka, amepelekewa barua kali na serikali ya Uganda akiambiwa ahame katika nyumba ambayo alipewa na serikali wakati wa uchaguzi mwezi Aprili.
Kwanza wiki jana Bw. Kiwanuka aliandikiwa barua akaambiwa ahame kwa muda wa siku tatu, ama angeshitakiwa kortini, Hakujali barua hiyo.
Bwana Kiwanuka akanieleza kwamba aliijibu barua hiyo akisema, "Mkitaka njooni mtutoe, hatung'oki, lakini hawakufanya chochote", aliniambia.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Geofrey Binaisa naye ameniambia kwamba serikali inaitaka nyumba hiyo ili mtu mwingine wa serikali ahamie, lakini Bw. Kiwanuka anagoma kutoka.
"Tumemwambia ahame kabla ya tarehe 31, Oktoba mwaka huu kama hatahama, nitampeleka kortini", alisema.
Kuhofia maisha
Bw. Kiwanuka anachachamaa kuhama katika nyumba hiyo akisema kwamba alipewa nyumba hiyo na serikali wakati wa uchaguzi kwamba alihofiwa maisha yake yalikuwa katika hali ya hatari.
Hana pa kuhamia
Ameeleza, "Serikali sasa inaniambia nihame, lakini haijanieleza kama hali ya maisha yangu ssa iko salama ama bado kama nitarejea katika nyumba yangu ya zamani".
Na pia hivi sasa nyumba yake ya zamani imevunjwa ili ijengwe upya, na hana pa kuhamia.
--------------------------------------------------------------------------------
Askari na shitaka
Ngurumo Alhamisi Mei 1, 1969
ASKARI wa Polisi Idi Juma, Mnyaturu mwenye umri wa miaka 18 majuzi alikana shitaka la kuvunja na kuiba shilingi 5 kwa askari mwenzake Andrew wa huko Ukonga Field Force.
Mshitakiwa alikataa mbele ya Hakimu wa Wilaya, Bwana Osakwe kwa kusema yeye hakuvunja wala hakuiba shilingi 5 mnamo tarehe 28/9/69 wakati wa usiku yeye alikuwa kazini huko Oyster Bay na kurudi kambini wakati wa usiku wa saa nane na tarehe 28/9/69 aliitwa katika ofisi yake na alipofika alijulishwa kwamba mwenzake, jirani yake amesema kwamba ameibiwa shilingi 5.
Id alisema kwamba yeye hajui kabisa juu ya wizi huo wala hausiani nao.
Ushahidi mbalimbali ulitolewa na askari pamoja na Tax Dreva ambaye alisema yeye alimchukua mshitakiwa kutoka mjini hadi Ukonga bila kumlipa fedha siku hiyo ya tarehe 27/9/69 akiwa yeye na Koplo Msadu.
Hakimu Bwana Osakwe alimuulza mshitakiwa wewe una umri wa miaka 18 uliingia lini jeshini?
Mshitakiwa alijibu kwamba yeye aliingia jeshini mwaka 1967, Hakimu alisema bila shaka mshitakiwa aliingia jeshini akiwa na umri mdogo usiotakiwa.
Hakimu Bw. Osakwe aliahirisha kesi mpaka tarehe 5/5/69 wakati atakapotoa hukumu yake.
--------------------------------------------------------------------------------
Nyumba yenye shetani yasusiwa
Paka akutwa na hereni
Uhuru Ijumaa, Agost 15, 1969
NYUMBA nambari B/21 ya shirika la Taifa la Nyumba, ya huko Temeke imekuwa wazi tokea Juni 18, lakini hakuna atakayehamia humo. Bwana John Mnyamani aliyekuwa akikaa humo hapo mwanzo amesema kwamba nyumba hiyo ina shetani.
Bwana Mnyamani alirudisha funguo za nyumba hiyo mwezi Juni kwa afisa wa shirika hilo, baada ya kueleza kuwa mali yake yote imetiwa moto na 'kiumbe kisichoonekana'. Bwana huyo alipewa nyumba nyingine huko huko Temeke.
Afisa mmoja wa shirika la nyumba alisema jana kwamba uchunguzi unafanywa hivi sasa kuhusu jambo hilo; na kwamba litakuwa tukio kubwa la pekee iwapo kweli shetani atagundulika nyumbani humo.
Bwana Mnyamani mwenye umri unaozidi miaka 40 na mwenye familia alikaa katika nyumba hiyo tokea Desemba 1966 mpaka hapo Juni alipoliendea shirika na kueleza juu ya nguo zake, magodoro na shuka zilizoonekana zikiungua usiku.
Baada ya kuihama nyumba hiyo, Mkuu mmoja wa TANU akifuatana na wananchi wengine waliiendea nyumba hiyo kuifanyia uchunguzi na humo walimkuta paka aliyekuwa na hereni masikioni. Paka huyo alikutwa chooni akiwa amezungukwa na maandazi! Habari ilipelekwa polisi haraka.
Hapo jana majirani walikataa kumweleza kitu mwandishi wetu alipoulizia juu ya jambo hili na kwamba hawakufuatana naye alipotaka kulikaribia jengo hilo.
Ingawa hivyo, barua moja ya ombi kukaa katika nyumba hiyo limepelekwa katika ofisi ya shirika la nyumba.
--------------------------------------------------------------------------------
Ngurumo, Jumatano, Mei 20, 1964
WAKATI wa sherehe ya kufungua jengo jipya sehemu ya Muslim School Moshi Bw. Ramadhani Saidi ambaye ni Mjumbe wa TANU National Executive, alikusanya kiasi cha shilingi 481/71 hapo hapo.
Miongoni mwa wachangaji alikuwa Area Commissioner Officer wa Upare Mwalimu Kihere pamoja na Executive Officer wake Sheikh Kassim Liku shilingi 100, Bw. Amiri Popat shilingi 100, Bw. H. Ladakh Khanji shilingi 100, Bw. Kiraia na mkewe shilingi 100 na Bw. Ramadhani Said mwenyewe shilingi 20, jamaa wengine waliongezea zilizobaki.
Bwana Ramadhani aliwashukuru sana wageni wote waliotoa michango na wale walionuia kutoa baadae akiomba radhi kuwa aliwashtukiza, na kwamba angaliwaarifu angaliweza kukusanya maelfu ya fedha kwa ajili ya shule hiyo. Pia aliwashukuru wananchi kwa kazi yao kubwa waliyofanya na jitihada ya kumaliza jengo hilo.
"Serikali haikatai kusaidia, daima husaidia wanaojisaidia wenyewe, serikali hii bado changa na mpaka hivi leo imefanya mambo makubwa ambayo haikutegemea, tufanye kazi kwa bidii, serikali ni sisi wenyewe, tusizubae zubae ati tukaongoja misaada toka kwa watu wengine. "Hii ni aibu", alisema.
Ahimiza
Akidokeza juu ya umoja, Bwana Saidi aliwahimiza wananchi wote washirikiane bega kwa bega ili wamalize jengo jingine la shule hiyo akisema kwamba ni jambo la busara na la kufurahisha kwa kila mwananchi kushiriki katika kazi za kujenga taifa.
Alimaliza alisema: "Misaada yenu haitasahauliwa na kila mtoto atakayesoma hapa akikumbuka kuwa fedheha ya ujinga imemtoka".
Area Commissioner wa Same Bw. M.M. Kihere akiwa mmoja wa wageni alisema; "Tumefurahi sana sababu mkutano huu umejitolea, jambo ambao linatutia moyo mkuu sisi tulioalikwa, hata hivyo nikiwa kama mgeni, nawaomba wenzangu wote wajitose katika kukamilisha jengo hili kwa njia ya kujitolea kwa kazi za mikono na michango zaidi ya kununulia vifaa; moyo na ari ya nchi ndiyo kitu kinachojenga taifa", alimaliza.
Bila shaka
Bwana Elimu wa Wilaya ya Kilimanjaro Bwana Muhina pia alisimama na kuushukuru mkutano huo wa wazazi akisema kwamba; "Tumeitwa hapa kuonyesha shida na matatizo yanayowatinga wazazi ili serikari iweze kusaidia - vema-misaada ikipatikana bila shaka mtapewa", Bw. Muhina aliwaomba wazazi wazidi kuendelea na moyo wao wa kujitolea kwa ajili ya watoto wao.
Hapo mwanzoni Chairman wa Muslim School Bwana Yusuf Nasir akifuatana na Headteacher wa shule hiyo aliwatembeza wageni mahali pote ili wakajionee wenyewe kazi kubwa iliyofanyika. Baada ya matembezi hayo chai iliandaliwa kwa wingi, wakati huo huo watoto wa shule hiyo waliwaburudisha sana wageni kwa vyombo na vichekesho mbalimbali, baadaye bendi ya shule ilipiga wimbo wa taifa, hapo basi watu wakasambaa.
--------------------------------------------------------------------------------
Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji
--------------------------------------------------------------------------------
Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua kwa: webmaster@islamtz.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook
Muhidin,
ReplyDeleteTafadhali naomba utuletee picha ya Mama Martha Wejjah.
Mama Martha Wejjah sijui kwa nini Dada Mija hajamuingiza kwenye ukumbi wa wanawake wa shoka. Mama Wejjah alifanya yasiyotarajika, kwa asiyetarajiwa, wakati usiotarajiwa, na kuleta matokeo yasiyotarajiwa.
Halafu kama itawezekana kupata kutoka magazetini naomba utuletee nukuu za ile kesi. Mimi nilihudhuria ile mpaka leo naiona picha ya ukumbi wa mahakama kuu na Jaji Dan Mapigano akiisimamia ile kesi..nazisikia sauti za kina Profesa Mgongo Fimbo na Profesa Issa Shivji wa Chama cha Wanasheria wa Kujitolea Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakimtetea Mama Wejjah, huku Wakili Murthazar Lakha akimtetea Mzee Kitwana Kondo.
Nikikumbuka hala hala za ile kesi najisikia kama nashangilia goli la mpira.
F MtiMkubwa Tungaraza.