naposti posti hii maalumu kumshukuru ndesanjo macha aliyeniambukiza haka kaugonjwa ka kublogu mwaka mmoja na siku moja kamili zilizopita kule helsinki, finland (tazama kumbukumbu ya septemba 2005, picha ya chini kabisa).

waama, nawashukuru wote mlionitembelea na mnaozidi kunitembelea kila siku kiasi sasa blogu yenu hii itafikisha watu laki mbili. asanteni sana.

nitakuwa mtovu wa fadhila nisipowashukuru baadhi ya mabloga walionikaribisha barazani na kunipa moyo. wako wengi mno na kuwataja wote itakuwa ngumu, lakini nitoe shukrani za pekee kwa wanachama wa klabu ya chelsea pale finland, wakiongozwa na mti mkubwa kwa kuwa wa kwanza kunipa taff.

vile vile wanazuoni makene, jeff msangi, mwaipopo, mark msaki, damija, chemi chemponda, simon kitururu, charahani, kibanda, mzee wa sumo bukuku, na wengi wengine kwa kuwa nami katika raha na karaha zinazoambatana na mambo ya blogu.

ndesanjo, nakupa salamu mkuu kwa kuahidi kufuata maelekezo yote uliyonipa kupitia kwa jeff. nakuahidi kwamba mwendo mdundo na nitaendeleza libeneke bila kuchoka wala kukatishwa tamaa na lolote na yeyote.

aluta kontinyuaaaaaa!!!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. MK POPOTE ULIPO SIJAKUSAHAU.

    KWA HESHIMA ZOTE NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA KAMA HESHIMA MAALUMU KWA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWAKO KWA KUNICHONGEA BLOGU YETU HII. UBARIKIWE!

    ReplyDelete
  2. Hapibethidei Michuzi, kumaliza mwaka ni faraja sana katika kazi ya kujitolea hasa ukizingatia wengi wetu tumedhani kuwa lazima tufanye kila jambo linalolipa fedha za hapo kwa hapo. Gazeti Tando hili lina heshima yake na historia yake bila shaka wakati ukifika wa tuzo za magazeti Tando ya Tanzania ambazo zinawzea kuanza mwakani 2008 unaweza kutajwa katika sehemu nyingi tu.

    Tumejifunza mengi kupitia hapa kwako na kubwa ni uvumilivu kwa wanaowekwa picha zao hapa na wewe mmiliki. Katika mafunzo haya pia tumejikumbusha kuhusu kufahamu kabla hujamtendea mtu jambo kumbuka pia kama jambo hilo lingefanywa kwako lingekuathiri kwa namna gani. Pia tunapaswa kukumbuka kuwa jambo unalolifanya kwa kudhani upo peke yako ikitokea likafahamika kwa umma na huku likibeba athari ya maisha ya wengine je utapata tuzo gani! Nimejifunza pia kuwa matukio ya kijasiri uhitaji fikra za kijasiri. Mtu makini hujiandaa kuutafuta umakini na jamii hufuata kupaka rangi pale paliokwisha kuanza kupendeza na sio kuzalisha kitu kipya.

    Mwezi ujao nitakuwa natimiza sherehe hizi za kuzaliwa kwa matukio matatu. Nitaanza kuweka tathmini pale kwangu. Kikubwa niwasalimu umma wa wasomaji wa gazeti tando hili na kuwatakia heri fanaka katika maisha, niwaombee kwa Mola abariki kazi za mikono yenu na awakumbushe kutafuta zaidi ili kuneemesha jamii yetu changa na maskini katika nyanja nyingi. Nisimalize haraka maana mwaka unaelekea pia ukingoni, ni muhimu kukumbuka kufanya tathmini ya mwaka hadi mwaka. Tumevuna mengi toka kwako Michuzi na tunatarajia kuvuna mengi zaidi mwaka unaoanza sasa. Mungu abariki nguvu hii uliyoianza na ubebe msalaba huu kwa maringo kabisa hata kama unahisi maumivu usikubali kuutua.

    Wakatabahu,

    Komredi Makene

    ReplyDelete
  3. Hongera kaka Michuzi kwa kutimiza mwaka, Mungu akuzidishie nguvu ya kutuletea vitu na nguvu ya ustahimilivu.

    Ndesanjo ushukuriwe sana, huwa nakufananisha na mchungaji mwema wa kondoo anavyofanya bidii kuwakusanya katika zizi na kuhakikisha hakuna anayepotea, hii inajidhihirisha pale mwanakondoo mmoja anapokuwa hajapandisha habari kwa muda mrefu, mchungaji wewe lazima utamuuliza kulikoni mbona kimya?

    Ubarikiwe.

    ReplyDelete
  4. I do think Ndesanjo is smart, wise and good looking. He is really something. Are you married Ndesanjo or something? Love your locks too fine and healthy..

    ReplyDelete
  5. Eee bwanaeee ndesanjo umekolea babakeeee! jibu basi kama umeshavuta jiko.

    ReplyDelete
  6. Michuzi,
    Itabidi moja ya sikukuu ya kuzaliwa kwa blogu hii ya aina yake ifanyike pale klabu ya Chelsea, pale Helsinki, Ufini. Mti Mkubwa Sana atakuwa mwenyekiti wa maandalizi.

    Michuzi, mwanazuoni Makene amezungumzia suala la kutathmini tumefika wapi na tunakwenda wapi. Blogu hii ni moja ya mfano wa mafanikio makubwa ya blogu zetu. Unajua ule msemo wa: Picha moja huzidi maneno elfu moja. Umekuwa ukituelimisha sana kupitia picha zako. Sio tu picha unazoweka, bali ubora wa picha zenyewe. Wengi tumekuwa tukifuatilia picha zako toka miaka ile ukitoa machozi pale Daily Newe (Noise?) kwa kupondwa na msomaji. Sasa hatuhitaji kuwa na nakala ya Daily News and Sunday News ili tuweze kufaidika na kamera yako. Umekuwa ukitupa picha za matukio mbalimbali muhimu nchini, picha za kihistoria (picha hizi zinanikuna sana), picha za jinsi Bongo inavyobadilika, picha za matamasha kama zile ulizopiga Zanzibar, na sasa tunasubiri picha toka tamasha la sanaa Bwagamoyo.

    Niliwahi kusema kuwa blogu hii ni kama vile jumba la makumbusho la taifa kwa picha mtandaoni. Unachofanya ni kutunza kumbukumbu za taifa letu. Iwapo kutatokea baa kama mafuriko au moto (Ruwa/Nguluvi/Mulungu/Kyumbi/Izuva/Ngai apitishie mbali)na kuharibu kumbukumbu katika maktaba za daily news, picha zako hapa zitaendelea kuwepo. Kwa maneno mengine, jumba hili la makumbusho ya taifa litaendelea kuwepo daima milele.

    Na wale wanaokuja hapa kutoa maneno machafu wakiwa wamejibana nyuma ya choo utafika wakati watajua kuwa wanayofanya hayana faida yoyote kwa taifa letu au kwao binafsi. Ni aibu kubwa kunapokuwa na ukumbi kama huu ambao maelfu wanafaidika, siku haiwi tamu bila kuja hapa, lakini wanatokea baadhi yetu wanakuja kuuchafua kwa matusi. Michuzi hujatukana mtu, hulipwi kutuwekea picha hizi, unatumia muda wako kuelimisha na kuburudisha umma. Sasa hao wanaokuja kwa matusi sijui wametoka Tanzania ipi. Tunalalamika nchi haiendelei, anatokea mtu anafanya jambo kama hili kwa kujitolea wanakuja watu wanaanza kurusha matusi kila kona.

    Kwanza niache kuwazungumzia. Tuwaache maana hakuna sababu ya kupoteza muda. Tuendelee na kazi Michuzi. Jua kuwa maelfu tuko nawe, tunafurahia sana kazi yako. Na tunategemea mengi zaidi mbeleni.

    **Haya: kuna aliyetaka nijibu swali kuhusu mimi kuwa na jiko au la.
    Jibu: kama nina jiko au sina sio tatizo maana unajua tena sisi Waafrika huwa tunaruhusiwa kuchukua zaidi ya moja. Waislamu wao mwisho ni namba nne. Sisi hatuna mwisho. Si unaona mfalme wa Uswazi ana 13 sasa?

    HERI YA KUZALIWA ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM

    ReplyDelete
  7. Happy Anniversary Mr. Issa Michuzi and issamichuzi.blogspot.com.

    Many Thanx.
    ©2006 MK

    ReplyDelete
  8. Hongera sana michuzi na uzidishiwe na kuendelea kutuletea picha nzuri za nyumbani...Hongera kwa kazi nzuri

    ReplyDelete
  9. Michuzi,
    Hongera nyingi sana kwa kutimiza mwaka mmoja.Naamini,kama walivyosema wengi waliotangulia,tathmini ya mwaka mmoja tu tangu uanzishe hii blog yako ni ya aina yake.

    Cha muhimu ni kuendelea kuelimisha,kuburudisha na hata kuanzisha mijadala migumu kabisa.

    Makene,Ndesanjo,Da Mija,Trio Kaka wameandika maneno ya busara sana ambayo naamini sote tukiyazingatia basi tutafika safari yetu bila matatizo.Hongera sana.

    ReplyDelete
  10. Ongera michuzi kwa kutimiza mwaka, blog yake imetufanya tuwe karibu na nyumbani japokuwa tupo mbali, imekuwa ikituelimisha na kutufundisha na pia imetufanya kutokuwa nyumba na matukio mbalimbali ya nyumbani.
    Bw.Michu\i kazi yoyote inayohusu public inahitaji uvumilivu wa hali ya juu, hivyo husife moyo na wachache wanaokuvunja moyo na hii blog kwa kutumia lugha chafu na kutoa maoni mabaya kuhusu blog yako.Yuor doing fantastic job', kikubwa zaidi imejijengea heshma kubwa sana kwa watanzania wanaoishi ughaibuni.
    Huu ni mwanzo kwako hivyo, wewe kama katibu wa wapiga picha wa Tanzania naomba utoe ushauri kwa wenzio nao wawe na mwelekeo wa kisasa kama wewe, wako wapi kina Mpoki Bukuku, Madanga Shaaban Madanga, Kwitema, Benny Kisaka, Athumani Hamis, Richard Mwaikenda na wengine ili nao tuzione kazi zao ambazo ni kumbukumbu tosha kwa vizazi vijavyo.
    ongereza sana rafiki yangu

    ReplyDelete
  11. we anon,mbona unamuulizia kaka wa watu hivyo?unataka kama hajavuta jiko akuoe wewe nini?talk abt proactive....hehehehehehhehe!

    ReplyDelete
  12. HI Bros, mambo yako makubwa na yanaelimisha kweli kweli, wanaojaribu kutukana wanafanya hivyo kwa sababu wana wivu wa kijinga. Wewe kaza buti braza, endeleza kazi ya ku blogu kisawasawa, siye tuko pamoja na wewe. Eti wanataka wakufanye wewe ni malaika wakati wao hata halufu yake hawaiwezi

    ReplyDelete
  13. kazi nzuri. kaza nia, endelea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...