mchezaji wa zamani wa soka selemani mathew akimuonesha waziri mdogo wa habari, utamaduni na michezo dk emmanuel nchimbi, afande tibaigana na sheikh khamis mfano wa akademi ya soka anayotarajia kuijenga sehemu za mtoni kijichi, dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hatua kubwa hii tunapiga kuelekea mafanikio ya soka.Skul ya Football hiyo na hakika ikikamilika,maelfu ya vijana wataonyesha vipaji vyao vya soka hali itakayotoa soko katika nchi za Ulaya.Cha msingi hapa ni kwamba vijana wachukuliwe toka kila pembe ya nchi na si Dar tu maana vijijini kuna vipachi kibao.Asante Mathew kwa jitihada zako.

    ReplyDelete
  2. Hapo zingetoka flat ngapi za 75m2 za 3 rooms, katika gorofa 6 tu, Ili ziweze kuwahifadhi wamama na watoto wasiokuwa na uwezo au baba, wa huko huko Mtoni Kijichi?
    Badala yake wanageza, hivyo ni vitu ambavyo huwa vinakuja baadaye wakati kila mkazi anaishi stable.

    ReplyDelete
  3. Huyo boss hapo juu ameandika nini ? hiyo si charity ni business ! ni mtu anawekeza capital yake kwa msingi wa kupata faida !
    Kalagabaho !

    ReplyDelete
  4. Hongera kaka Mathew! lakini wasi wasi wangu ni kuwa mpango huu umeanza muda mrefu sana!! Ila kila siku tunaonyeshwa model peke yake!!

    Kama uko serious nafikiri ungetuelezea pia source of funds. pia nakushauri uende kwenye mashirika kama NSSF,PPF,PSPF etc kuona kama wanaweza kukusaidia.

    Hongera kwa vision yako hiyo

    ReplyDelete
  5. nafikiri hilo ni wazo zuri na sion sababu ya huyo kusema funds kazitoa wapi. Hongera sana!

    ReplyDelete
  6. Mmmh Selemani Mathew una mambo umeibukia tena kwenye soka academy? Hata hivyo unajua kuzichanga akili ongeza jitihada. Ila hatujasahau usanii uliowafanyia wachezaji wakongwe wa Yanga na Simba kupitia kwenye ki NGO chako ambacho sijui hata kama kilikuwa kimesajiliwa.

    ReplyDelete
  7. Hivi huyu Nchimbi udaktari kasomea wapi?

    ReplyDelete
  8. Bongo kuna Madaktari wengi tu wa Siasa za majukwaani pasiipokuwa na Phd, usijeshangaa siku moja Yussuf Makamba nae atajiita Dr. Yussuf Makamba. Ili kuwapima inabdi kuwakusanya Madaktari vingunge wote waende katika vyuo vikuu vyetu wakatoe lectures kwa part time ili kuziba pengo la uhaba wa wahadhili.

    ReplyDelete
  9. YALEYALE.. WALISHINDWA KIJIJI CHA MICHEZO PALE UWANJA WA TAIFA MPAKA LEO NI MAGOFU, WANAKUJA NA JIPYA. MZEE MATHEW OMBA KIJIJI KILE WAKUPE UENDELEZE.

    ReplyDelete
  10. Hii model inaonyesha haijatengenezwa na architect proffesional. Inaonyesha uwanja wa football una magoli ya basketball! halafu milango ya hizo ghorofa iko kwa nnje!!! bila ngazi...Huu ni usanii.

    ReplyDelete
  11. Hii model inaonyesha haijatengenezwa na architect proffesional. Inaonyesha uwanja wa football una magoli ya basketball! halafu milango ya hizo ghorofa iko kwa nnje!!! bila ngazi...Huu ni usanii.

    ReplyDelete
  12. Muda wa kuchezeana akili umepita. Nchi isikubali ubabaishaji. Kama huu ni mradi hai, wadau washirikishwe. Polisi na michezo wapi na wapi? Au ndiyo kuandaa mazingira ya kupwepa pingu siku za mbele? Hata kama ni uwekezaji binafsi, unagusa Taifa moja kwa moja. Private Finance Initiative hiyo, lazima isimamiwe na mradi utimize lengo lake. Hongera sana Mathew kwa kubuni kinachohitajika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...