Home
Unlabelled
butiama
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Tata,
ReplyDeletePozi tu…mzee mpendwa wa Tanzania, ulituacha...Lakini legasi yako itabaki siku zote, hususani kwa kazi nzuri uliyoifanya katika nyanja ya elimu nchini:
Uliamua kutoa jengo la TANU la Mtaa wa Lumumba kuwa chuo kikuu nchini – ukianzia na Kitivo cha Sheria – wanafunzi wa kwanza wakila na kulala hapo Dar es Salaam Chuo cha Ufundi.
Ulitoa ubaguzi wa rangi mashuleni hata kabla ya uhuru (nikiwa darasa la sita).
Ulitoa darasa la nane (nikiwa darasa la saba) ili wanafunzi waweze kuingia sekondari haraka.
Ulitoa kikwazo cha mtihani wa Teritorio Standadi Eiti ili wanafunzi wazidi katika shule za sekondari.
Uliruhusu wanafunzi wa darasa la saba kujaribu mtihani wa darasa la nane ili wakishinda waende sekondari.
Uliamua strimu ziwe mbili katika shule za sekondari (nikiwa darasa la nane).
Ulitoa kikwazo cha mtihani Teritorio Standadi Teni (nikiwa darasa la tisa hapo Bwiru Boiz).
Uliamua wanafunzi wa darasa la kumi na moja kujaribu mtihani wa Kambriji wa darasa la kumi na mbili ili wakishinda waende hai skuli.
ulitoa kikwazo cha skuli fizi (nikiwa darasa la 11).
Nilipokuwa darasa la kumi na moja, uliamua kuwepo na pri-selekisheni ya kuingia moja kwa moja hai skuli mwezi wa Januari bila kungoja majibu ya mtihani kutoka Kambriji mwezi wa Februari (mwaka wetu - 1963 - tukawa wa kwanza.
Uliamua kuwa wanafunzi wa darasa la 14 wakipasi prinsipo mbili na sabsidi moja waende chuo kikuu (nikiwa darasa la 13 Tabora).
Uliamua kutokana na Azimio la Musoma, wale wote waliomaliza darasa la 12 na kufanya kazi miaka miwili wawezeshwe kujiunga na chuo kikuu ili kupata wataalamu wengi.
Uliamua kila mwanafunzi wa Kitanzania achukuaye masomo ya sayansi pale Mlimani achukue pia somo la ualimu ili kukidhi mahitaji ya walimu katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu!
salam kwako baba wa taifa letu.wanao tunakusalimu.baba yetu tuna swali,twaomba utujibu japo kwa njia ya ndoto tukiwa usingizini.je iwapo filamu ya darwins nightmare ingetoka ukiwa rais ungechukua hatua zipi.tunakuombea upumzishwe kwa utulivu.
ReplyDeleteMungu Ailaze Pema Peponi Roho Yako Baba Wa Taifa Letu La Tanzania Utakumbukwa Daima Milele Pengo Lako halitozibika Kamwe.
ReplyDeletesikujua kumbe mwalimu kuna siku alikuwa anakwenda GQ namna hii, safi sana.
ReplyDeleteMwalimu Legacy...kila kitu anasa Mfalme wa bidhaa adimu.
ReplyDeleteFriji ni stove ni luxury
Ukifika Airport unatozwa kodi za ajabu kwa ajili ya kuwa na sharti au gauni mpywa kwenye sanduku
No sabuni, sukari, mafuta ya kupikia, betri, khanga (magendo), unga ngano, chumvi (ilikuwepo ya mawe tena chafu), dawa ya mswaki (Mwalimu alisema tumia miti), no ndala (watu walivaa matairi), niendelee?
Asante Sokoine na Mwinyi kwa kutokoa.
Huyu alimlostisha sana dingi wangu, kujenga kinyumba tu uswahilini alijaza form za ikulu kama mia kueleza alikotoa pesa ya kujenga nyumba, nakumbuka tulikuwa tukilipa kodi tv ya home wakati huo TV ilikuwa inashika TVZ na KBC ki 504 cha Dingi kilisababisha watu wa usalama kuja home kila siku kujua kama anahujumu uchumi na wakati huo Dingi alikuwa na post kubwa kitaifa na alikuwa na Masters siku hizo
ReplyDeleteIlikuwa ukimkanyaga vibaya unaamka asubuhi na kukuta maajabu yameandikwa juu yako kwenye Daily News na Uhuru na RTD! Tena maneno ya uwongo kabisa. Picha na stori zinatoka Ikulu. Na hao 'wahujumu uchumi' walikuwa na nini ukiona sasa una cheka.
ReplyDeletesera ya mwalimu ya kukataza vitu ilikuwa nzuri hasa kwenye kutufanya tujitegemee na tukuze viwanda vya ndani,tungekuwa tumeendelea sana kiuchumikama mwinyi angeiendeleza.
ReplyDeleteMwinyi asingeweza kuziendeleza sera za mwalimu za kiuchumi.Sababu kubwa ya kung'atuka kwa mwalimu ilikuwa ni kusukumwa na World bank na IMF kubadili mfumo wa uchumi.Nyerere alisema hatakuwa jiwe hivyo ni bora ubadilishwe na mwingine ndipo mzee ruksa akaachiwa gurudumu.Ivory coast ilikuwa na mfumo kama wa mwalimu na rais wake alikataa kuubadilisha,uchumi wao ukashuka sana na kukawa na tofauti kubwa ya uchumi wa wananchi matajiri na masikini na mwishowe vita vya wenyewe kwa wenyewe.Mwalimu aliona mbali ndio maana kwake ilikuwa bora kung'atuka kuliko matokeo kama haya.
ReplyDeleteAnonymous october 14, 2006 4:36:05pm - Sasa kama mzee alikuwa ana posti kubwa na alikuwa ana masters degree - kwa ni ni alienda kujenga uswahilini?
ReplyDeleteNyerere sitamsahau alikandamiza uhuru wa kuabudu sana.Alilazimisha watu kulima tumbaku kwenye mashamba ya vijiji vya ujamaa hata wale ambao imani zao ni tofauti. Waliokataa waliteswa sana.Tunashukuru Mungu hakuishi milele.Mbona tungekoma wengine!! wenye misimamo mikali kuhusu tumbaku.
ReplyDeleteMtazame usoni nyerere na nywele zake halafu mtizame Waziri mkuu Lowasa.Eti mitaani wanasema Lowasa baba yake mzazi ni Nyerere.Ndio maana sura na mvi kichwani wanafanana.Mama yake Lowasa aliwahi kuwanon`goneza wazee fulani wa kimasai wakataka kumchinja akajinyamzia kimya mpaka leo.Kila heri kwa uwaziri mkuu Edward Lowasa Nyerere.Kweli Baba yako Nyerere alikuwa msiri.
ReplyDelete