akiwa kiongozi wa mstari wa mbele katika ukombozi wa afrika, hakuna siku mwalimu alifurahi kama hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Winnie Mandela, shujaa wa ukombozi wa Africa kusini ambaye anasahaulika, hebu tumuenzi kwa kazi yake kubwa, hasa kwa miaka yote Mandela aliyokuwa gerezani, mama huyu aliendeleza kazi yake.

    ReplyDelete
  2. kazi gani unayosema wewe anoy hapo juu? hujui kama alikuwa cheater huyu dada winnie? alitenda tendo la ndoa kinyume na matarajio ya wengi has mumewe mandela, one mistake one goal? acha asahaulike ingawa atakumbukwa kwa kula uroda na kijana mdogo..samahani Michuzi for my language...

    ReplyDelete
  3. Nyerere ulitutosa watanzania .Tulichangia damu zetu,pesa na wanajeshi kumsaidia Mandela. Leo wanaofaidi ni wakenya ambao hawakuchangia kitu. Wakenya waweza kwenda Afrika ya Kusini bila hata kulipia Viza.Wakina Mandela walipokuwa wakimbizi wa kisiasa tuliwapokea kwa wingi bila kinyongo kwa mikono miwili,leo hii vijana wetu wa kitanzania ambao ni wakimbizi wa kiuchumi wanaokimbilia Afrika ya kusini,wakikimbia hali mbaya ya uchumi wa Tanzania ulioharibika sababu pesa zetu nyingi za kigeni tulizitumia kupigania uhuru wao,Vijana wetu hutimuliwa na kukimbizwa mitaani kama wanga na serikali ya Mandela na kurudishwa na pingu.

    Mandela turudishie damu tulizochangia,Pesa na tulipe fidia kwa vijana wetu waliofia Afrika ya kusini wakikusaidia kupigana.

    ReplyDelete
  4. Nakubaliana nawe anoy 12:35 mwalimu alikua na mtindo wa "tenda wema nenda zako usingoje shukrani" na nafkili mtindo huu hauafikiwi wa wabongo wengi.Tulipigana Uganda kuwatoa ktk makucha ya nduli Idd Amin hakuna alichodai naskia madeni ya vita waganda walitulipa ktk awamu ya tatu ya uongozi wa mkapa not even ktk awamu ya pili.Tulikua mstari wa mbele kuikomboa sauzi hakuna lolote tulilopata sanasana raia wao ulituulia kiongozi wetu shupavu ndugu Sokoine.Vilevile kuna habari kwamba waLibya waliochukuliwa kama mateka wa kivita huko Uganda walirudishwa bila kutulipa chochote wakati Ghadafi alikua tayari kuwanunua.leo hii tuna shida ya mafuta na wao wanayo kibao hawawezi kutuuzia kwa bei ya kirafiki! huu ni ushenzi!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Chief Burito,
    Ulitegemea Uganda watulipe papo kwa papo baada ya vita? wangetoa wapi hilo fuba wakati vita na utawala mbovu wa Amini vilikuwa vimeiweka nchi pabaya?
    Hata hivyo nakubaliana nanyi kuwa Wasouth ni watovu wa fadhila sana wanakuja kutuibia wakijida wawekezaji, TANESCO,NBC na Melerani

    ReplyDelete
  6. Wewe mizzou wa 11.12 kwanini nisimsifie Winnie? Kwanza hivi unajua aliyofanya, na unaweza kufanya hivyo au ndo nyie hata mkiitwa muandamane kudai haki zenu mnaingia mitini mkiona FFU?
    Winnie ni mke wa pili wa Mandela, wa kwanza waliachana baada ya miaka 13, sababu mojawapo ikiwa kazi zake za siasa. Haya nikuulize, una uhakika kama Mandela alikuwa mwaminifu? Na kama Winnie angefungwa miaka 27 Mandela angekaa mwaminifu? Hakuna mtu mwenye uhakika wa lolote, tatizo mshamfanya Mandela kama mungu fulani, na Winnie kama mshenzi. Kwa taarifa yako, Mandela alipokuwa gerezani hakuweza kufanya lolote la maana zaidi ya kuandika, na kubaki jina ambalo liliwahamasisha watu, nenda kasome historia, Winnie amefungwa gerezani mara nyingi(kuanzia 1958), na hata kifungo cha nyumbani, mara nyingine kwasababu ya kwenda kumuona Mandela na ni kazi za watu kama Winnie waliokuwa nje zilizoendeleza mapambano. Jambo lilimletea doa kubwa kimataifa ni mauaji ya Stompie, na wala sio huo upuuzi unaosema. Hakuna ajuaye uhakika wa jambo hili, ila aliomba msamaha kwa makosa yaliyotendeka wakati wa harakati za ukombozi. Kwa watu wanaosoma historia, huyu mama ataendelea kuwa mtu muhimu katika mapambano ya Afrika kusini, na nitarudia, tuendelee kumuenzi. Kama unataka kulaumu watu, hebu anza na Mandela ambaye kasamehe makaburu, lakini kashindwa kumsamehe mkewe, mwanaharakati mwenzake, hata siku ya kuapishwa ilibidi Thabo Mbeki ndo amwalike Winnie, halafu kamaliza hapo kamwoa Graca..eeh sasa? nikupe mfano wa Clinton, tena mkewe yupo hapohapo bado kafanya upuuzi, lakini bado anakumbukwa kwasababu ya kazi yake nzuri kama rais hasa kiuchumi, na kidiplomasia.
    Cha muhimu, kila mtu ana makosa, lakini kama ana mchango mkubwa lazima tuuenzi pia, ndio maana tunampenda Nyerere hata kama uchumi wetu uliharibika, alikubali makosa...

    ReplyDelete
  7. Mama Winnie anatakiwa aenziwe sana. Ni mmoja ya wanaharakati wa kuigwa SA: Wanaomzalau Winnie ni wale wasiojua Historia ya Ukombozi ya SA. Hata kama alifanya kosa . Maandiko matakatifu yanasema samee saba mara sabini.Mathayo 18:21-22.

    ReplyDelete
  8. Jamani Watanzania tuliothirika na vita ya Uganda tuichukulie hatua Libya.Nyerere alikataa kupokea fedha za kulipia kununua mateka askari waliotuchokoza wa Libya.Lakini Nyerere alisahau kuidai Libya ilipe fidia hasara tuliyopata kwa uvamizi ule kabla hajawaachia bure mateka wa Libya.Kwa kuwa serikali iliwaachia mateka wa Libya wakati wananchi tulioumia hatukupata kifuta machozi chochote nawaomba wanasheria andaeni kesi dhidi ya serikali ya Libya na Kanali Gadafi iwalipe wanakagera fidia na watanzania wote walioathirika na hali ngumu ya Uchumi wengine hadi wakavaa magunia sababu ya vita ile.Wanasheria na wanaharakati simameni na raia tuishughulikie Libya mpaka ilipe fidia maana ushahidi upo kuwa walituvamia na raia waliteseka kutokana na uvamizi wao.Serikali iko kimya.Raia tuje juu dhidi ya Libya,ambayo haina hata ubinadamu wa kutuuzia mafuta kwa bei nafuu kipindi hiki.

    ReplyDelete
  9. Wewe Mizzou unasema nini? huyu mwana mama amekaa kwa kuvumilia na kunyanyaswa miaka yote zaidi ya ishirini ambayo mumewe alikua ndani. Kosa la kutoka na huyo kijana ambaye alikua anamzidi miaka sita haliwezi kumfanya tumuone kwamba alikua mtu mbaya. Mbona Clinton aliyefanya mapenzi na sectretary wake tena white house bado anapeta na bado anaheshimika sana duniani? kwanini isiwe vivyohivyo kwa Winnie Mandela? Inabidi usome autobigraphy ya Winnie kuweza ku-appreciate alichofanya yule mama wakati mumuwe akiwa lupango.

    ReplyDelete
  10. Nimegundua kuna watu duniani wanapata umaarufu kwa sababu ya kujipendekeza tu na si lolote. watu hao ni kama Mandela, Mkapa, Museveni, Obasanjo, kagame na wengine.
    hao wanajipendekeza kwa wazungu na wanaonekana ni bora sana mpaka wanaheshimiwa sana lakini hakuna kubwa walilolifanyia bara letu la Africa.
    Nilikuwa naangalia hotuba ya mwalimu Nyerere ya 1997 alipolihutubia bunge la SA huru, bunge la mseto, wakati Mandela ni raisi na Mbekhi ni makamu. Yaani kwenye hotuba ile, Mandela alikuwa kama mwanafunzi wa chekechea tu, aliyekuwa anajifunza toka kwa Prof aliyebobea duniani. Hotuba ya Mwalimu, kama zilivyo hotuba zake zoote, huwa inadumu miaka mingi ijayo na zinaendelea kudumu kuwa kweli na applicable kwa ulimwengu huu hasa barani Africa.
    Utashangaa wazungu, wanampendelea Mandela na kumpa Nishani ya Nobel, na kuonekana kama ni mwafrica wa aina yake, au utashangaa wazungu hao hao wanajidai kutengeneza UN ya kimtindo wake na kuiita kamati ya utandawazi na kumpachika Mkapa kuwa sijui raisi wake. Waongo wakubwa, wanaotoa fadhila kwa vibaraka wao tu.

    Ukisoma kwa mfano kitabu cha mwalimu kilichoandikwa miongo takribani 3 iliyopita nyuma "FREEDOM AND UNITY" utaona maelezo na mambo kwenye kitabu hicho bado ni hot cake mpaka hivi sasa. lakini hapo hapo soma kitabu cha Mandela kilichoandikwa miaka si zaidi ya 15 iliyopita nyuma, "LONG WALK FREEDOM" utaona hicho kitabu hakidumu wala hakina jipya la kukifanya kuizike ulimwengu mzima na kutafsiriwa kwa lugha mbalimbali.
    Anyway nilichotaka kusema, Mandela si lolote si chochote kwa Mwalimu Nyerere, ingawa mwalimu walimbania kumpa Nobel, lakini anayo zaidi ya Nobel toka kwa watanzania na wapenda maendeleo na amani wote duniani

    ReplyDelete
  11. Nishani ya NOBEL haipatikani kwa mtu kuwa bingwa wa kuhutubia bali kwa utendaji hasa.Raisi wa Kenya MAREHEMU Kenyatta aliwahi kuulizwa Je?Kenya na Tanzania zinazidiana eneo gani akajibu kuwa Ukitaka wahutubiaji wazuri sana nenda Tanzania utawapata wengi lakini ukitaka watendaji wazuri wa kazi maofisini na katika biashara na uchumi njoo Kenya.Mandela alikuwa na haki kupewa Ile nishani sababu kwa muda mfupi tu kaibadilisha Africa Kusini kuwa mbabe kiuchumi na kuwa na wawekezaji katika karibu kila nchi Africa wakati Nyerere amejaza mavitabu ya fikra na hotuba zake nzuri kwenye makabati ya jumba la makumbusho Butiama.Mimi sitaki tena kusikia hotuba ziwe,Za nyerere,Kikwete,au wewe uliyeandika hapo juu ni vizuri msihutubie mkae kimya miaka hata yote mitano lakini tuone maendeleo.Waliokataa kumpa Nishani ya Nobel Nyerere nawapongeza.Huwezi kumpa nishani domokaya kama Nyerere ambaye kutwa kazi yake ni kuongelea sera zisizotekelezeka za ujamaa na kujitegemea.Mandela oyee!!Kikwete jibu hoyee!! upesi.

    ReplyDelete
  12. sawa kaka, lakini ungejua kwamba uchumi wa SA haukukuzwa na Mandela, ulikuzwa na wakoloni walioikalia SA kwa miaka mingi nyuma.
    Nyerere alijitahidi sana kukuza uchumi wa Tanzania, hasa kwa kutumia sera zake za vijiji vya ujamaa.
    anyway nadhani wewe na wakenya wako, au kama wewe ni mkenya, endelea kuwa hivyo, ila hata Kenya hakuna lolote zaidi ya uchumi mbovu kwa 70% ya wananchi wake wa kawaida. Ukilinganisha na watanzania wa kawaida, wabongo uchumi binafsi uko juu zaidi.
    fanya research kabla hujaongea

    ReplyDelete
  13. Kweli wabongo kwa hotuba hamjambo jamaa ameshaanza kusifia vijiji vya ujamaa vilivyokufa siku nyingi. kwa taarifa yako Profesa RENE Durmond Mfaranza aliyeandika kitabu maarufu cha Africa Inakwenda Kombo alipotembelea Tanzania walimuuliza kuhusu Operation vijiji vya Ujamaa ya nyerere akaponda bila kuogopa akajibu kuwa hiyo siyo operation vijiji bali ni operation hamishia watu kando ya barabara yenye lengo la kuanzisha vimiji vidogo vitakavyokuwa miji baadaye.Akasema kijiji maana yake ni nyumba ya kila mwanakijiji kuzungukwa na mashamba makubwa kabla ya kumkuta mwanakijiji mwingine.Nyerere hakusikiliza ushauri huo kama kawaida yake akachukulia kuwa huyo profesa ni beberu tu aliyetumwa na CIA.Nyerere akaanzisha vimiji midogo (Vijiji vya Ujamaa) ambapo watu wanalundikana pamoja kama mijini wakisafiri mbali kwenda kulima ambako mtu anachoka hata kabla hajafika shamba matokeo yake wengi wakageuka machinga,wauza maandazi na wapika chips,na chapati kwenye hivyo vimiji vidogo alivyovianzisha Nyerere.Mpaka leo wengi wanakimbilia mjini sababu nyerere mwenyewe alichochea watu kupenda vimji badala ya vijiji.Nyerere ni chanzo kikubwa cha watu kupenda mijini kuliko vijijini.Vijiji vya ujamaa havikuleta maendeleo bali viliua maendeleo ya vijijini kabisa vikaleta mfumuko wa watu kupenda miji kama yeye alivyokuwa akipenda kukaa Msasani karibu na bahari akipunga upepo na kimwana wake Maria baada ya kuwalaghai watanzania waliomaliza elimu ya msingi ya darasa la saba ya bure ya UPE ambapo walimu wakuu wa shule zao walikuwa darasa la saba wenzao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...