mwalimu akiongoza harakati za kudai uhuru viwanja vya jangwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Namwona Nyerere na Bibi Titi. lakini huyo bwana mwingine ni nani?

    ReplyDelete
  2. huyu kama sikosei ni abdulwaheed sykes.alikuwa rais wa TAA kabla hajamwachia nyerere mwaka 1952.baba yake alikuwa anaitwa kleist sykes.huyu baba yake ni miongoni mwa waanzilishi wa TAA kama welfare association.kwa "bahati mbaya" watu hawa wamesahaulika kwenye historia ya tanzania.

    ReplyDelete
  3. Zemarcopolo, yafaa sana wataalamu wasomi (wanahistoria, siasa) na wazee waliobakia washirikiane kutuandikie historia hii.

    ReplyDelete
  4. Huyo Bwana mwingine ni Mzee John Rupia. kweli historia zetu wenyewe hatuna!

    ReplyDelete
  5. wazee hizi historia zipo na zilikua zinafundishwa mashuleni miaka yangu niliyokua shule ya msingi 1986-1992 sijui badae kama mambo yalibadilika lakini hivi vitu viko kwenye vitabu labda bwana misupu ajua zaidi mana kuna kitabu cha picha cha matukio yote muhimu kuanzia harakati za uhuru,muungano,kifo cha sokoine na mengineyo ila nimekisahau jina mana nilikisoma miaka ya 90.

    ReplyDelete
  6. Kwa anony wa 5:39pm.Hicho kitabu kama sikosei kinaitwa Ukombozi wa Tanganyika na ndani yake kina Sub title Sokoine Mtu wa Watu.

    ReplyDelete
  7. hahaha hapana jamani. ngoja nisaidie kidogo inaonekana mmesoma vitabu vya juu juu. kitabu ambacho utapata kujua historia kamili ya TAA, TANU, Nyerere, akina SYKes, RUpia, Kawawa na uhuru kamili wa Tanganyika.

    Soma kitabu kinaitwa,"UAMUZI WA BUSARA" kitabu hiki kimetayarishwa na Idara ya Habari ya Chama kwa kushirikiana na Idara ya Elimu ya Siasa ya Chama.
    kimepigwa chapa na NUTA PRESS LTD, P.O.BOX 2982 DSM.

    ngoja ninakili UTANGULIZI wa kitabu hiki:
    yapo mambo fulani ambayo yasingefanyika ni vigumu kujua historia ya nchi ingekuwaje leo hii, mathalani, kama TANU ingekataa kushiriki katika Uchaguzi wa Kura tatu mwaka 1958, sijui tungekuwa wapi.

    Hali kadhalika kama rais Mwalimu Julius K. Nyerere asingeamua kuacha kazi ya ualimu, histori ya nchi yetu huenda ingekuwa tofauti na ilivyo sasa.

    Kupitishwa kwa azimio la Arusha, kuukubali Mwongozo wa chama, na mengineyo mengi yaliyomo humu kitabuni ni mkusanyiko ambao ofisi kuu imeuita"Uamuzi wa Busara".

    Hivyo kitabu hiki ni cha maana sana kwa historia ya nchi yetu kwani bila Uamuzi uliomo humo Kitabuni, historia yetu isingekuwa kamili.

    KATIBU MTENDAJI MKUU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...