Home
Unlabelled
katuni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Waswahili husema kulia na kucheka,zote ni kelele tu.
ReplyDeleteSasa festi ledi kumpiga kibao mwandishi na hiyo ya waandishi kumlamba miguu president,vyote ni Udhalilishwaji wa majonalisti... no diferenti!
KUMZABA MUANDISHI KIBAO NI MATOKEO YA MTU KUTOPENDA WENGINE KUWA NA MAWAZO TOFAUTI NA YEYE.NI HULKA YA WENZETU,HATA KWENYE BUNGE LAO PIA TUNASIKIA HABARI ZA WATU KUPIGANA NGUMI NA KUCHAPANA BAKORA WAKIPISHANA KWENYE HOJA.....VILEVILE SIONI HAJA YA KULUMBANA KUHUSU KATUNI HII KWA SABABU HAITABADILI UHUSIANO KATI YA RAIS NA WATANZANIA,ALIECHORA KATUNI HII NI MWENZETU LABDA AELEZEE ALIKUWA NA MAANA IPI.....VINGINEVYO NADHANI TUSIWAPE HAO JAMAA MTAJI WA KUENDELEA KUPATA SABABU YA KULUMBANA NAO....
ReplyDeleteGodfrey Mwampembwa (GADO)is Kenya-based Tanzanian cartoonist.
ReplyDeleteHe drew this cartoon particularly after Bush talked about Kenya in his meeting with JK and after the JK's press recent conference.
Well, not all Kenyans are of the same view like he is.
Read the comments of the Kenyan Ambassador to TZ, Mr Boaz Mbaya.
http://kumekucha.blogspot.com/2006/10/kenyan-envoy-in-tanzania-hits-out-at.html
KAKA Michuzi huyo jamaa kainama kwenye mguu wa kikwete wa kulia ni wewe NINI? fafanua basi vizuri....
ReplyDeleteHivi na marehemu Mwalimu Nyerere anafanya nini hapo?
ReplyDeleteHiyo imezidi mwalimu angecomment hangetoa tamko lakini nafikiri kidogo Jk hana haja ya kuongea nao hawa jamaa watanzania huwa tuna uvumilivu hivyo anaweza kukaa kimya kabisa na kuona mwisho wake.
ReplyDeleteJamani labda sina macho lakini anony wa 4.50 we nyerere umemuona wapi hapo?
ReplyDeletetuweke upinzani pembeni, hivi inawezekana huyu jamaa ana point? there has been very little criticism of JK kwenye media so far, na karibu kila mtu JK kiboko, hivi ahadi zote zile anazotoa lini atatimiza kama kurekebisha basic needs kumetushinda, leo dar hamna maji, umeme ndo umerudi kwao Afrika Kusini, watoto wa form four mizengwe hadi kwenye uandikishwaji, bado siku chache kufanya mitihani hawana namba kisa watu wameingia mitini na hela zao, mawaziri wa kumwaga wanachokifanya hatuoni, ila JK ziara haziishi na upambe wa waandishi unazidi kupamba moto, sasa sie tusemeje?
Asante sana anony wa 6:45. Wabongo watu wa ajabu sana, wanaangalia katuni bila kuitafakari. Huyu JK anamwagiwa sifa kila kukicha huku nchi ikiteketea Kisa hao waandishi wanaoijikomba kwake. Ati sisi ni bora kuliko Wakenya wakati hata utaratibu wa kuwawezesha watoto kufanya mitihani unatushinda!!
ReplyDeleteMichuzi ni bora kupigwa kibao na fest ledi kwa sababu ya kuandika ukweli. Kuliko kujipendekeza kwa JK kwa kuandika uongo.Ukweli unauma ndio maana Kenya MEDIA walipigwa kibao.
ReplyDeleteni kweli tupu, waandishi wa kwetu mmezidi, mkiongozwa na ipp-media.sijui mnapewa pesa au ni kujipendekeza tu!mkumbuke JK sio mfalme ni Rais. viongozi wa siasa hawapambwi na maua kila kukicha,hata kama wanafanya kweli.
ReplyDelete"hongera sana Mwampemba unasaidia kutoa tongotongo,tunahitaji watu kama nyinyi Tanzania"
Dr Ishengoma
Michuzi asante sana kwa kutuingizia hii katuni, nilikuwa na hamu ya kuiona.
ReplyDeleteMichuzi asante kwa kutuletea katuni hii.Ongera mwampemba kwa kua mkweli.Tanzania inaitaji waandishi wengi kama wewe.IPP MEDIA na vyombo vingine vya habari TZ sasa vinashindana na magazeti ya chama tawala kumpamba kikwete.Heshima ya TZ MEDIA inazidi kurudi nyuma, na inarudishwa nyuma na waandishi wenyewe wa TZ kwa kujipendekeza kwa JK.
ReplyDeleteI know this Guy Gedfrey Mwampebwa amesoma Mlimani Primary na mama yake alikuwa ni mwalimu wa hesabu darasa la nne...
ReplyDeleteJk amevitia vyombo vyote vya habari mfukoni mwake. Sawa kabisa anony hapo juu media yote sasa ni propaganda ya CCM. Lakini tusiwalaumu waandishi hawa maana njaa ya bongo inajulikana.
ReplyDeleteMimi mpaka sasa siamini kama kuna siku 100 za JK, pale niliona waandishi wamechemka. hata Yesu hakupewa siku 100 za mafanikio. jamani tumsubiri JK baada ya miaka 3 au 4 tuone nini amefanya. Nadhani hata kaka yangu Michuzi tunaona nae alivyo kwa kutuwekea picha za JK tu, bila kutuonesha mambo mengine ya upande wa pili wa siasa za bongo.
ReplyDeleteGado, yuko huru kutoa maoni kwa ajili ya maendeleo ya nchi yake. Kuna mmoja alitoa maoni kuhusu mapanki na akachora jinsi wabunge wanavyohangaika bungeni kufokea kitu kilichokwisha toka (darwing's night mare) bunge likaja juu. Anyway bado uhuru si mkubwa kiasi hicho, lakini tutafika.
MICHUZI ALIKUWA ANAKATISHA KWA MGUU UPANGA KWENDA DAILY NEWS.SASA HIVI MAMBO JUU YA MSTARI AMTUAKANE AU KUMPINGA KIKWETE YEYE ANAKICHAA!!!I CAN UNDERSTAND MICHUZI
ReplyDeleteWakenya , wanafahamika siku zote wanajifanya wanajua sana !Lakini katika jambo la kushangaza mpaka leo hii bado wanasherekea ukabila . Ni kweli kuna matatizo kwenye vyombo vyetu vya habari , ila watuachie sisi watz tulizungumzie hilo !
ReplyDeleteHapa signal waliotutumia wakenya ni kwamba wanajua wanachofanya. Hila kikubwa sana watanzania inabidi muelewe ni kwamba kati ya watanzania 1000 ni watanzania 10 wana uchungu na nchi yatu. Kwa wakenya kati ya wakenya 100, wakenya 90 wana uchungu na nchi yao. Kwa hiyo bado tuna kazi kubwa, unajua wakati wa uchaguzi wakenya kutoka marekani, Uk nchi za kiafrica huwa wote wanaamia nyumbani. Ukienda nchi kama south Africa, Botswana huwa wanachukua magari kuamia nyumbani.
ReplyDeletePia sio maneno wanajua mambo na ukiangalia baada ya NARC kuingia madarakani na kusahau kanu mambo yamebadilika kabisa. Hivyo jamani achana na wakenya wenzetu tayari wameisha tengeneza mambo yao. Unaona na nchi kubwa zinaanza kuwaogopa, let tanzania build tanzania na tuachane na mambo ya majirani.
Lakini vile vile tuna safari ndefu sana kwa wale wanaoweza kuona mbali, tunaoneana aibu.
Taabu watanzania wengi hawana uzalendo .Katuni hiyo imechorwa na mtanzania asiye na uzalendo na nchi yake.Inawezekana anafanya hivyo kutafuta hifadhi ya kisiasa kenya akiona anaandamwa na watanzania kutokana na kuchapisha kikatuni hicho kutukana waandishi wa nchini kwake.Biblia inasema asiyependa wa kwao ni mbaya kuliko asiyeamini.Huyu mtu ni mbaya.Msiwalaumu sana wakenya.Aliyechora katuni hiyo Mwampemba ambaye ni Mtanzania mwezetu Yuda Iskariote wa Tanzania asiyejali watu wa kwao.Ni vizuri tu aitwe ubalozi wa Tanzania kule kenya ashauriwe umuhimu wa kutanguliza utaifa mbele anapofanya shughuli zake za kuchora katuni iwe chini ya mchanga au kwenye magazeti uchwara ya kenya.
ReplyDeleteKenya tunaijua kwa ufisadi.Vyombo vya habari kenya huwa haviandiki habari za umma ziwe za chama tawala,cha upinzani wala Serikali mpaka wapewe rushwa ndipo zitoke.Ndio maana kenya utakuta magazeti yamejaa habari za watu binafsi na Makampuni binafsi na kurasa nyingi za magazeti hujaa matangazo ya biashara na vifo ambayo huwa yanalipiwa pesa.Hongera waandishi wa Tanzania maana mnajali habari zaidi za umma kuliko za binafsi kama ilivyo katika magazeti ya kenya.Habari za serikali ni muhimu kuliko kujaza habari za makampuni binafsi na wanachosema watu binafsi.Mimi sihitaji kujua mtu binafsi anasemaje kuhusu serikali,napenda zaidi kusikia serikali inasemaje kuhusu raia wake ili nijue nina nini cha kutarajia serikalini.Wakenya ni wambeya wakubwa wanalopenda kuandika watu binafsi,na makampuni binafsi yanasemaje.Kwa ufupi wanapenda kuwalamba miguu watu binafsi na makampuni binafsi ili waishi.Heri niilambe miguu serikali kuliko mtu binafsi sababu mtu binafsi anaweza kukunyea au kukujambia ukimlamba wakati serikali haiwezi.
ReplyDeleteNyie watu wa (uhasama)usalama wa taifa acheni mambo yenu. Ati Uzalendo uzalendo gani unaongelea wewe anony wa oct 10 saa 12:42? Yaani Mabalozi walionunua nyumba hewa kwa mabilioni ndio wazalendo, huyo Kikwete aliyetuingiza kwenye Mkataba wa IPTL ndio mzalendo, anayekanusha watu wanakula mapanki wakati ndio chakula chao ndio mzalendo? Ni ukweli ulio wazi waandishi wa Tanzania hasa IPP wamezidi kumsifia Kikwete kwa vitu ambavyo havipo. Hilo la juzi kasema tu walimu walipwe IPP wamerukia kumsifia utafikiri ndio mara ya kwanza kusikia kauli kama hizo.
ReplyDelete