nimeupenda mchoro huu uliopo kwenye kuta za jukwaa la chuo cha sanaa bagamoyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mchoro unanikumbusha "Chakubanga" (najua huyu siye Chakubanga wala Chukulubu!). Hivi Michu-Boy swahiba yako Washokera, Radi bin maaruf yupo wapi siku hizi, bado anamuendeleza Chezo na Anti Soni?

    ReplyDelete
  2. uncle michuzi nilifikiri kuna uhuru wa MEDIA hapa, kama kweli uhuru upo basi tuwekee maoni katika picha ya CRITIC ! Na ile katuni ya waandishi wa habari wakimlamba miguu kikwete ni kuhusu waandishi kama MWANAKIJIJI, wewe sijakuona ukimfagili kikwete kwa sana ! keep it up my uncle !!

    ReplyDelete
  3. aisee michuzi si mchezo ama kweli kuna wachoraji jamani....

    ReplyDelete
  4. Sijui wenzangu mnaona nini kwenye picha hii ! mi naona mzee wa pwani aliyeridhika na umasikini wake !
    muda huu aliokaa hapa labda ungetosha kuikandika nyumba yake (labda ya bi mdogo hii !) na kuzuia miji tachungulia !
    The painting is so detailed michuzi anzisha kaduka fulani hivi kwenye net picha namna hii zingeweza kuuzwa pia papa hapa

    ReplyDelete
  5. wabongo wavivu tunashabikia picha ya mtu kusinzia.

    ReplyDelete
  6. huyu ndumilakuwili jamani

    ReplyDelete
  7. Ni mojawapo ya picha nzuri ulizowai kuweka katika web. Inaonyesha hali halisi ya Watanzania wanavyoishi kuleee Tanganyika.Ni picha yenye mafundisho mengi kwa watu wanaoelewa sanaa ya michoro.

    Sio vibaya kama utaweka ile katuni ya waandishi wa habari wa TZ mnavyomlamba JK miguu.Ni heri wakenya wametusaidia kuwaonya waandishi wa TZ na tabia ya kujipendekeza kwa JK.Mnawadanganya watu wachache, wenye akili wanafahamu jinsi gani vyombo vya habari vinavyopigana vikumbo kua karibu na Ikulu.Je mnataka yatimie yale maneno ya rais wa awamu ya tatu kwamba waandishi wa habari wa TZ ni wajinga, na hawana akili ya kufikiri kwanza kabla ya kuandika habari?

    ReplyDelete
  8. Hii picha imenikumbusha Tabora.

    ReplyDelete
  9. Hiyo katuni ya Kikwete iko hapa. Aliyechora ni Mtanzania anayeishi Kenya.


    http://photos1.blogger.com/blogger/4301/672/1600/controversial%20cartoon.jpg

    ReplyDelete
  10. yap prportions zimeenda kushoto, ila maybe ni njia mojawapo ya usanii, kwamba focus ni huyo baba, na nyumba ni background fulani...
    anyway hii picha inasikitisha, ndiyo kazi kubwa ya wazee nyumbani, asubuhi akiamka anapata chai na vitumbua, mchana ugali wake, jioni kahawa, kashinda hapo kutwa nzima. Mama ndo akauze dagaa na mboga sokoni wale. Madai yake, shambani hamna kitu mvua haiukunyesha...akiishiwa, anaoza binti ale mahari.
    kwa mtindo huu tutafika kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...