Home
Unlabelled
umoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
wacha tufe tu lakini hiyo kondom ya kike haitafanya kazi.
ReplyDeleteNaona hao wanafunzi kwa nyuma kule wanacheka kama vile kuna kichekesho kinafanyika hapo. Hii ndio tabia inayopelekea kutozingatia hata kile wanachofundishwa hapo. Hili jambo la kujikinga maabukizi si la mchezo kabisa, huu ugonjwa ni hatari na hauchagui. Sasa sitegemei wanafunzi kama hao watatilia maanani kweli na kuwa na msemo wa kutaka kitu kama hicho kitumike kama wakibanwa kwenye 'kona'.
ReplyDeleteKaka Michuzi,hii sasa kali,naogopa hata kuchangia mada.
ReplyDeleteInapendeza kuona watu wakitoa hamasa juu ya mapenzi salama hadharani, kwa wale walioko serikalini watakuwa wananielewa juu ya matumizi ya pesa ya TACAIDS katika kueneza VVU. Inauma kuona budget ya kuhudumia nchi nzima katika VVU inakaliwa na watu wawili na bila kujali umuhimu wake kwa watu wengine.
ReplyDeleteMichuzi nadhani unanielewa juu ya hili, kwa ufupi ni seminar za ukimwi na matumizi yake maofisini najua nawe ni mmoja wa watafunaji hapo kwenu daili nuez.
KIJU
Eh! Anaelekeza matumizi ya kondomu ya kike kwa wanaume! Na labda ni mkakati sahihi.
ReplyDeletengono salama!! mmhhhhhhhhhhhh
ReplyDeleteNaona huyo mwanaume naye anasikiliza kwa makini juu ya hiyo kondom ya wanawake. Mie nafikiri hii ni vizuri, ila nina wasiwasi hawa wanaume wanaweza kukataa ngono wakigundua kuwa mwanamke amevaa hiyo kondom-
cha maana zaidi katika hii vita ni kuwaelimisha akina mama kujua kusema hapana kwa ngono ambazo hazina mipira-mara nyingi akina mama wanalazimishwa kufanya ngono zisizo salama sababu za kiuchumi. wanaume ambao hawapendi kuvaa mipira ya kiume nafikiri hawatapenda mipira ya kike pia.......
Hata mimi nacheka kuona anatumia mboo bandia katika demonstration! Tena ina mapumbu.
ReplyDeleteUKIMWI unatufundisha kuzingatia uaminifu, ukweli, uwazi, kuepukana na unyanyapaa na kulinda afya zetu na jamii yetu. Kondomu ya kike ni nzuri hasa kwa kuwa wanawake wananyanyaswa sana na wakati mwingi wanashinikizwa kufanya ngono zembe. Hivyo wakichukua uamuzi wa kulinda afya zao, basi tuwapongeze na kuwasaidia. Tatizo ni kwamba huyo mkufunzi amekosea kidogo katika kuonyesha vielelezo vyake. Pengine ingesaidia angemwachia mwanamke atoe mafunzo hayo.
ReplyDeleteJambo la kusikitisha ni kwamba UKIMWI umefanywa mgodi wa watu wengi[Sina maana ya kuwa huyo pichani ni miongoni mwao]. Na hizo kondomu za kike zinawafikia akina nani kwa bei gani? Mama, dada, bibi, na shangazi zetu huko vijijini wanaziona hizo? Je walala hoi wanaziona hizo/ Watazipata kwa bei gani? Kweli tusipoangalia UKIMWI utawaangamiza zadi watu wenye maisha duni! Mungu kaibariki sana Tanzania na Afrika kwa ujumla. Sasa tubadilishe na wimbo wa Taifa tuseme Mungu Iokoe Tanzania na Afrika!