leo nawapa kikosi kamambe cha redio doche welle ya ujerumani akiwepo mkuu wa idhaa andrea schmidt (mwenye suti nyeusi) ,msimamizi wa studio nina Markgraf ambaye naambiwa ni mzungumzaji´fasaha wa Kiswahili, wa pili kutoka shoto msitari wa mbele ni munira muhammad kutoka kituo chamatangazo ya televisheni ya watani wetu wa jadi nchini kenya-ktn. munira yuko mafunzoni hapo idhaa ya kiswahili ya dw. kulia namwona kaka sekione kitojo, wa pili shoto ni aboubakar liongo a.k.a zigo, na kati nyuma si mwingine ila ni mkongwe abdul mtullya a.k.a mzee wa mitemba. naibu wa idhaa mohamed abdulrahman ni huyo wa pili kulia. unaambiwa hawa jamaa wanatisha! mie kila saa nawasikiliza. na umeona kaka abuu liongo alivyokwiva?? kaka abuu hujachacha, ulaya ulaya tu shekhe! lakini msondo wanakumiss amana! mjomba anakusalimu sana, anasema sasa yuko fiti baada ya kuugua kwa muda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hapa katika hiki kikosi anamiss Oumilkheir Hamidou.ana style fulani ya kutoa taarifa,akianza tu kuongea ni vigumu kubadili station kabla hajamaliza!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...