nina habari njema na mbaya toka homu. habari njema ni kwamba mfalme wetu wa bongo flava sir juma nature ni mmoja wa wasanii wachache wa afrika waliowini nafasi ya kwenda copenhagen leo usiku kwenye tuzo za mtv; mbaya ni kwamba msanii wetu nimeongea naye dakika chache zilizopita na akanambia hakupewa tiketi na waandaaji kwenda denmark, hivyo bado anagaagaa bongo, ndo kusema hata kama atachaguliwa kushinda hatokuwepo kwenye kupokea tuzo. uchunguzi utaendelea kukicha kwa nini imekuwa hivi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. yaani msanii wa nguvu kama huyu anakosa pesa ya kusafiria kwenda pale ulaya?? Au mambo yake hayajachanganya sana nin?

    Hongera sana bwana Juma Nature, pole sana kwa kuchacha, lakini hiyo zawadi italeta mambo mengi ikiwemo kuongezeka kwa kipato sababu watu wengi sasa watajua vitu vyako.

    ReplyDelete
  2. Congratulation Nature, really it is sad if not suck, what a waste of great exposure n opportunity.

    ReplyDelete
  3. Ukiwa nominated halafu hupewi ticketi ya kuhudhuria maana yake hujashinda.

    ReplyDelete
  4. Kuna issues mbili hapa

    1) kwanza it is kind of embarassing kwa msanii kama huyo kushindwa ku-raise nauli. Hata fans wake wangeweza kumpeleka - the round trip ticket would have been less than $1800.

    2) Nadhani ni swala la aibu sana kutegemea watu wa MTV wampe ticket huyo Mr. Juma Nature. Mimi nadhani wao wana assume kwamba kama mtu amefika huko alikofika should be able to take care of himself. Seriously jamani hebu fikirieni. Kweli $1800!!!! - i am just amazed

    ReplyDelete
  5. meneja wa huyu jamaa ni mbumbumbu kweli kweli ndiyo analiangusha pia hadi kundi la "wanaume" wangekuwa mbali sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...