Wapiga kura wametamka:
Kura zimepigwa kutafuta saa ya mkutano wa kwanza kabisa wa wanablogu na wapenzi wa blogu wa Tanzania. Mkutano utafanyika saa nane mchana saa za Tanzania, Novemba 18, 2006.

Wapiga kura waliochagua saa nane mchana wameshinda. Hakuna masanduku ya kura yaliyoibwa wala kura zilizoharibika. Wala hakuna pingamizi lolote.

Maandalizi ya mkutano yanaendelea katika ukurasa wa wiki ambao utaupata kwa kubonyeza hapa. Tafadhali shiriki kwenye maandalizi. Ukipata tatizo la jinsi ya kuweka maoni yako kwenye ukurasa wa maandalizi ya mkutano, bonyeza hapa usome maelezo mafupi.

Kura 22 zimepigwa kuchagua saa nane mchana kwa saa za Tanzania
Kura 19 zimepigwa kuchagua saa sita mchana kwa saa za Tanzania
·
Hivyo: Mkutano wa wanablogu na wapenzi wa blogu wa Tanzania ni tarehe 18 Novemba, 2006, saa nane mchana saa za Tanzania.

Kama unataka kujua saa nane za mchana Tanzania ni saa ngapi hapo ulipo (kama upo nje ya TanzaMkutano huu utafanyika kupitia teknolojia ya Internet Relay Chat, hivyo utakuwa ni mkutano wa mtandaoni. Bonyeza HAPA uende kwenye tovuti ya mkutano.

Maelezo:

Maelezo haya ni muhimu sana maana usipoyafuata hutaweza kushiriki.
1. Nenda kwenye tovuti ya IRC@Work (http://www.ircatwork.com/)
2. Ukifika hapo utakuta kisanduku kina sehemu tatu.
3. Sehemu ya kwanza inasema Nickname. Andika jina lako kwenye kisanduku hicho.
4. Sehemu ya pili inaitwa Server. Usiandike chochote au kubadili chochote hapo
5. Sehemu ya tatu inaitwa Channel, hapo utaandika: #blogubongo
6. Baada ya kufanya hivyo, bonyeza pale panaposema Login
7. Utakuwa umeingia ndani ya ukumbi wa mkutano.
8. Ukishaingia, upande wa juu kulia utaona majina ya watu wengine walioko ukumbini.

Ukitazama chini kabisa utaona ufito mwembamba ambao ndio utautumia kuandika mchango wako kwenye mkutano. Ukishaandika unabonyeza Enter kwenye kompyuta yako ili mchango wako usomwe.



ILANI

Watu wengi tunajiuliza blogu ni kitu gani? Tunatembelea blogu, tunazisoma, tunashawishika kutaka kuanzisha zetu, ila bado tunakuwa tunajiuliza, “blogu ni nini?” Soma makala alizoandika Mfalme wa Blogu Ndesanjo Macha kujaribu kutoa jibu la swali hili. Makala hizi ziko katika sehemu tatu. Bonyeza hapa.

Pia kuna makala fupi katika Wikipedia ya Kiswahili inayojibu swali: blogu ni nini? Bonyeza hapa uisome.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Asanteni sana nyote mnaoshiriki kwenye maandalizi haya ya awali. Swali; tunaweza kuingia chumba cha mkutano kabla ya mkutano? Kwa vile mmetuonyesha njia ya kwenda huko, kuna akina sisi tunaotaka kujaribu kuipita njia hiyo kabla ya hiyo Jumamosi. Maana huku Bongo foleni si za magari tu, tuna foleni za intaneti pia kwa maana ya connections na mashimo mengine ya barabarani!

    ReplyDelete
  2. Kweli kaka maggid umenena.Zile makala zilizokuwa zinakosha moyo katika gazeti la Rai zinatoka leo.Nitazimiss sana. lakini, nasikia mmepandisha bei ya gazeti la Rai?.

    ReplyDelete
  3. Habari hii ya wanablog wa TZ inakuja wakati muafaka wa kuuliza je huu ni ungwana kweli kwanini serikali imeivunja blog ya bwana Metty Jaduong jana mchana ?

    http://mettyz-bongoland-reflections.blogspot.com/

    ukitaka kuona kivuli chake hapa

    http://64.233.161.104/search?q=cache:hHe2D7U0GLUJ:mettyz-bongoland-reflections.blogspot.com/+/metty&hl=en&gl=us&ct=clnk&cd=5&client=firefox-a

    ReplyDelete
  4. Jamani,

    Nadhani kulikuwa na tatizo dogo tu la kiufundi. Blog yangu bado ina dunda...mimi mwenyewe roho kidogo initoke lakini, kwa sababu sikujua ni nini kinaendelea.

    Nimefuata ushauri wa "kiufundi" wa Bw. Jeff Msangi na naona mambo yamerudi kama kawa. Nawahakikishia tu kwamba bado nipo kwenye mchuma wa kublogi.

    Metty.

    ReplyDelete
  5. Egidio!
    Maswali yako nitakujibu nikija kukutembelea kwenye blogu yako, maana nimeona una kahawa na kashata za India!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...