wadau wa soka, mwamkumbuka huyu?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Daud Salum " Bruce Lee". Siye wapenzi wa Simba tunamkumbuka huyu zaidi mara ile alipomzuia winga machachari wa Vita ya Zaire, Mayanga Maku!
    Asante sana Michuzi kwa kutukumbusha mbali.

    ReplyDelete
  2. Namkumbuka sana huyu (BRUCE LEE), nilisoma naye Tabora Boys miaka ya sabini. mara ya mwisho nilipoonana naye alikuwa anafanya kazi Nasaco

    ReplyDelete
  3. Michuzi huyo ni Daudi Salum (bruce LEE) beki mmoja Hatwari sana namkumbuka sana huyo yuko wapi? maana ni miaka ya sabini na nne nikiwa OLYMPIO PRIMARY SCHOOL darasa la 2 alikuwa Favorite wangu ktk wekundu wa mzimbazi.

    ReplyDelete
  4. Ama kweli wanamichezo wanapofuata maadili na kutunza afya zao kwa kutolewa, kuvuta n.k hawazeeki. "Bruce lee" hapa anaonekana "ten years younger" anaweza hata kukipiga tena. Hajachoka.

    ReplyDelete
  5. HUYU ANGEKUWA ANACHEZA MPAKA LEO KILA SIKU KADI NYEKUNDU. MTU ANARUKA SARAKASI KWENYE FOOTBALL MPAKA ANAITWA BRUCE LEE!!! SOKA LA ZAMANI NI MANGUVU AKILI NDOGO !!

    ReplyDelete
  6. Bruce lee siku hizi ame kuwa Pai

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi, huyo si mwingine mwanangu ni "Bruce Lee" mwenyewe-Daud Salum NO 2 ya Simba Sports Club wekundu wa msimbazi miaka ile ya mwisho mwisho ya sabini na mwanzoni mwa themanini. Alikuwa hapiti mtu. Yanga wanamjua sanaa

    ReplyDelete
  8. Anony wa 5:39:56am umenifurahisha kwa hilo neno la pai,neno la zamani hili,yaani lilikuwa linatumika kipindi hicho cha daudi salum akiwa beki mbili wa msimbazi,pai siku hzi ni wazee wa jengoni....nakumbuka wakati wa bruce lee,kandambili alipigwa bao miaka mitano mfululizo kuanzia 1977 hadi 1980,lunyasi golini yuko omari mahadhi bin jabir(RIP),beki kulia mwenyewe bruce lee,beki shoto mohamed kajole machela(RIP),nne athumani juma,mkoba mohamed bakari tall,sita nicodemus njohole,saba george kulagwa best,nane ezekiel greyson jujuman,tisa jumanne hassan masiment,kumi mwenyewe king kibaden/adam sabu/martin kikwa,kumi na moja alikuwepo thuwein ally.....'77'gongo wazi alipewa goli sita kama kasimama

    ReplyDelete
  9. Kumbe inawezekana mtu kutunza afya yako na kupendeza mpaka age hiyo !I bet not many of his agemates wangekuwa tayari kupigwa picha !
    enzi hizo list ilikuwa
    1.Omar Mahadhi
    2.Daud Sallum Bruce Lee
    3 Mohamed Kajole Machela
    4 Athuman Juma
    5 Mohamed Bakari Tall
    6 Nico Njohole
    7 Ezeikel Grayson Juju man
    8?
    9
    10
    11Thuweni Ally
    Wengine nisaidieni !
    Abdul

    ReplyDelete
  10. Nane alikuwa anapiga Khalid Abaeid,tisa Jumanne Masmenti na kumi King Kibaden.

    ReplyDelete
  11. mimi si mpenzi wa simba lakini Thuweni Ally alikuja baadae hakuwapo huyo mechi mnayozungumzia.

    ReplyDelete
  12. Ewaa, sasa huu ni wakati muafaka, jana tu nilikuwa nafikiria mwenyewe, jamani vipi PETER TINOO?? Historia inasema huyu ndiye mchezaji aliyefunga goli pekee liliyoipeleka TANZANIA kwenye africa cup kwa mara ya kwanza na mwisho mpaka sasa, kwa kifupi aliibeba Bongo yote mgongoni kwake, LAKINI, habari za kusikitisha, huyu shujaa nasikia ni choke taabani hadi kandambili zina matundu, mteja, wengine wanadai alikuwa kibaka uchwara, kama bado yu hai.
    OMBI KWAKO MICHUZI uwasilishe, au kina TENGA kama mnaingia humu, hamuoni kuna haja ya kumsaidia huyo mtu ikiwezekana apewe hata uchua misuli kwenye hiyo timu ya sasa inayojiandaa kungia kwenye michuano hiyo, nina uhakika mchango na uzoefu wake unaweza sana kusaidia kwenye uhamasishaji ha hata kumsaidia yeye binafsi kimaisha jamani, nchi nyingine yeyote huyu TINO angekuwa NATIONAL HERO!!!
    MICHUZI nakuomba sana ulifanyie kazi hili jambo sababu wahusika una mawasiliano nao ya karibu kuliko sisi wengine, Mungu ibariki TANZANIA.

    ReplyDelete
  13. aaaaaah...habari za kusikitisha sana kuhusu Peter Tino,nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa huyu jamaa nilikuwa na picha zake nyingi sana kwenye kitabu changu,duh pole sana ,i wish ningeweza kumsaidia hata kwa dola mia lakini niko mbali sana ughaibuni lakini kama brother michuzi ukisoma hii na unaweza kumpata huyo jamaa tuwasiliane najua utafikisha ujumbe my email snslondo@yahoo.com

    ReplyDelete
  14. ...sorry nimekosea email ni snslondon@yahoo.com

    ReplyDelete
  15. Wabongo ni wazuri wa kuongea wala si vitendo. Tungeweza kuvitumia sana vipaji vya Veterani hawa. Zamani ndio kulikuwa na wachezaji bongo siyo sasa wavaa vipuri na wasuka nywere. Wanatumia maguvu sio akili? hao wa sasa wanaotumia akili wamefikia fainali za Africa? Nani anamfikia Sunday Manara, Niko,Kibadeni Tall, n.k kwa sasa. Watu mwanzo walikuwa wanapenda mpira wa Bongo kwa kuwa wachezaji walikuwepo. Sasa macho Premier League. Hongereni veterans rekodi yenu bado haijavunjwa

    ReplyDelete
  16. Ahsante bwana Michuzi um
    nipeleka mbali saana ...ee bwana "Nyupi" uko wapi unamkumbuka rafiki yako wa Olympio aliyekuwa anakaa Uhuru na Msimbazi - JNg.!? Unakumbuka Mama masi pale Mfaume? nitumie e-mail: saxon-1@hotmail.com.

    ReplyDelete
  17. Huyu ni Daud Salum (Kaburu) Hili ndilo jina ambalo tulimpaga wakati tuko shule ile ya jeshi kule Tobora... Nasikia siku hizi kapata kibarua swafii cha sirikali!!!

    ReplyDelete
  18. Kumbe huyu ni Daudi Salum, aisee singemkumbuka kabisa. Tulikuwa naye pale Tabora School. Nakumbuka alivyozua tafrani ni Mwalimu Kyando (nasikia marehemu) mpaka mwalimu akabwebweta akisema "...(Daudi Salum) kanitukna bila kusema k..nyoko wala k..nina, ila kaitukana." Aliondoka pale TS mwishoni mwa mwaka 1976 kabla hajamaliza form 5 ili kuendeleza kandanda akiwa DAR. Sijawahi kumwona tangu hapo

    ReplyDelete
  19. Anony wa 17/11/06
    Ile list kuongezea tu nasikia hawa pia ni marehemu
    Mohamed Tall (RIP)
    Jumanne Masumenti (RIP)

    ReplyDelete
  20. daudi kaburu alisoma Tabora, alikuwa pale na abdallah mwinyimkuu,lucas nkondola halafu wote wakajiunga na simba katikati ya 1975 nakumbuka walikuwa wanakujaga dom kwa mashindano ya shule za sekondari, nakumbuka watu dodoma walikuwa wanampenda sana kwa sababu alikuwa mwana riadha shupavu, the guy could run and jump like a gazelle/kudu lakini tusimsahau shaban baraza,kama sio ajali ya dec 1974 daudi asingechukua nafasi fullback right, baraza alikuwa beast.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...