ujenzi wa barabara ya shekilango unaendelea kwa mwendo wa pole kutokana na mvua zinazonyesha. hapa mfanyakazi wa kampuni ilopewa tenda hiyo akiondoa maji ya mvua ili waendelee na kazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Je hii ni ile barabara Mh. PM aliyoagiza ijengwe mara moja, alipowabeba Mawaziri, RC Makamba, Mkurugenzi wa Manispaa, etc? Mbona haiishi??

    ReplyDelete
  2. hahahahahahah usinichekeshe michuziina maana huyu jama yuko katika kampuni au na iyo barabara inajengwa vipi,uuuuuuuuuuuuuuuui

    ReplyDelete
  3. HARI SINGH & SONS ni mabingwa wa kujenga mifereji na sio Barabara....Mfano ni ule mradi wa LOWER MOSHI IRRIGATION SCHEME.
    Sijui hii kazi ya barabara walijifunzia wapi???Mpenda Keroro.

    ReplyDelete
  4. Tatizo la miradi yetu ya bongo mpaka afe mtu pale kwenye mashimo ndipo kitengo cha maafa waziri mkuu kipate kazi na Kaimu raisi wetu atoke kukiuka katiba kwa kuhudhuria vikao vya bunge NDIPO AJE KUFUKUZA MTU usimamizi wa jaziba anaofanya PM wetu kwa kweli akitoka watu wanakuangalia kisogoni nahamna linaloendelea.,
    Ngoja uone sam nojoma kwa sababu mkuu wetu (JK )anakwenda kufungua 15/11 inatengenezwa kwa bidii yote MAMBO YA BONGO HAYO - JK hukuwa na sababu ya kukataa kufungua Hoteli ya waziri wako arusha na kuenselea kumpa uwaziri kutoka wizara moja akiboronga , unampa nyingine MUNGU AWAPE NINI MUHIDINI tubaki tu kupiga picha picha bora mwenzetu huwa wanakukumbuka kwenye tour USA nk safari hii mtalii kakutosa.

    ReplyDelete
  5. Ni bora wangesubiri tu hiki kipindi cha mvua kikaisha hii hali ya kuchota maji kwa ndoo mradi kazi iende, wataharibu kazi!

    ReplyDelete
  6. Ni bora wangesubiri tu hiki kipindi cha mvua kikaisha hii hali ya kuchota maji kwa ndoo mradi kazi iende, wataharibu kazi!

    ReplyDelete
  7. Nakubaliana na anonymous, kama wasimamizi wa kazi hii wasipokuwa makini, kazi itaharibika. Ni bora mkandarasi akasubiri mvua ziishe.

    ReplyDelete
  8. Hapo ndio mji namba moja wa TZ? Umaskini huu hii inji! Ona binadamu huyo anavyofanya kazi ktk mazingira ya ajabu machafu. Analazimika tu kwa kuwa hana kipato mbadala na vyombo vya serikali vinavyopaswa kukemea ajira za aina hii havipo au vimelala. Watanzania wengi wanafanyishwa kazi za ajabu maeneo mengi kama mahotelini, migodini, majumbani n.k. Watanzania wengi pia wananunua huduma duni kwa pesa nyingi kama mashule feki, gharama kubwa za simu, umeme n.k vyakula visivyofaa masokoni hii yote kwa kuwa serikali ama haina vyombo madhubuti vya kusimamia na kudhibiti maslahi ya walaji au kama vipo havifanyi kazi. Umaskini huu utakwisha lini jamani?

    ReplyDelete
  9. JAMANI HIVI SERIKALI NI MASKINI KIASI HIKI? YAANI MAJI KIBAO YA MVUA HUYU MLALAHOI ATAYAMALIZA KWA HAKO KAKOPO? MBONA MAFWEDHA KIBAO YANAPATIKANA KATIKA MSAFARA WA RAIS ANAPO KWENDA NJE YA NCHI NA WATU 100 NA USHEHE ANAKOSA KUNUNUA MASHINE YA KUNYONYA MAJI? SASA NAANZA KUONA NI JINSI GANI BARABARA ITAKAVYO CHAKAA SIKU MBILI BAADA YA MATENGENEZO KUISHA, YAANI TUKO CHEAP KIASI HIKI? AIBU GANI MUNGU WANGU...JAMANI UGHAIBUNI TUCHANGENI DOLLAR KIDOGO TUTUME MASHINE YA KUNYONYA MAJI JAMANI! NIMAMBO YA AIBU HAYA, KOPO LA KIMBO LITAMALIZA MAJI YA MVUA LINI? MTUME TOBAA!!!!

    ReplyDelete
  10. Hata mie nimejiuliza, hivi huyu jamaa ni mjenzi kweli au alikuwa mpita njia tu??

    ReplyDelete
  11. yaani kwa kweli tunatia aibu saana yaani barabara ipo jijini inatengenezwa katika staili hiyo,pm alivyotoa agizo hiyo barabara itengenezwe nilizani itatengenezwa ktk kiwango cha juu jamani viongozi wetu ndiyo kasi mpya hiyo huyo kijana atamaliza lini kwa ndoo hiyo,yaani pampu wameshindwa kununua?na huyo mkandarasi lazima kalipwa ma milioni ya sh,africa kweli ya moto but ilove u africa cause u ma home.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...