Michuzi!

kwa vile leo ni boxing day nimeona nikuletee khabari hii.

Kuna kijana Mbongo anaitwa Rogers Mtagwa ni bondia hodari sana wa kulipwa ambaye anaishi Philadephia, USA. Nimeona pambano lake. Simjui, niliona tu akichapana na Pereira wa Brazil, nikaamua kumtafuta kwenye mtandao na nikampata ktk www.peltzboxing.com/fighters.cfm

Ebu jaribu nawe kumtafuta huyu kijana. Na kama kuna wadau wenye habari zaidi watupatia. Kwa kweli nafurahisha kuona Mbongo akitamba ughaibuni.

Happy Boxing Day!

NYUPI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. huyu jamaa ni mzuri mno, labda ni miongoni wa mabondia hodari kabisa kutoka matumbi(TZ). Nimeona mapambano yake mengi tu, jamaa si mchezo. Amekomaa kinoma. Anajulikana kama Mexican Killer!

    ReplyDelete
  2. Huyo kijana Rogers mimi nimeshuhudia mapambano yake mawili Elhambra club s. Philly na Rode Island masikini ya mungu promoter wake ni wale Italian gangs wa S.Phill vile jamaa hana makaratasi wanamfanyisha wanachotaka wao,ni bwana mdogo kati ya 25 au 26yrs.Namwonea huruma sana mpaka afike 30yrs kama atakua hajachukua title ya kutosha basi atakua mzigo kwa familia yake.Pambano lake moja mimi nilikwepo alishinda lakini alikua hata hawezi kuongea roho iliniuma kichizi.

    ReplyDelete
  3. Michuzi, umeandika, "kwa vile leo ni boxing day nimeona nikuletee khabari hii."

    Boxing Day has nothing to do with ubondia!

    Si siku inayofuata sherehe za Krismasi---siku ya kufungua makasha ya zawadi za Krismas!

    ReplyDelete
  4. Kuniradhini, si Michuzi aliyeandika niliyonukuru hapo juu.
    Mwandishi ni NYUPI!

    The error is regretted!

    ReplyDelete
  5. jamani boxing day sio siku ya ngumi ni siku ya kufungua zawadi baada ya xmass

    ReplyDelete
  6. Kijana ni mkali nimeona mapambano yake kama matatu, michuzi tuambie anaundugu na Beki JELLA MTAGWA? baba yake alikuwa Mahili sana nakumbuka alitoka mpaka kwenye Stampu ambayo sidhani kama Posta alilipwa maana TZ hatujui kuwaenzi Mashujaa wetu pia nilisikia aliumwa sana kiasi cha kukosa msada wa matibabu ni kweli?

    ReplyDelete
  7. Acheni utumbo, na hiyo picha ni zawadi huoni kuwa umejua kuwa Tz tunakijana wetu mwana Ndondi mimi ni zawadi tosha. Zawadi sio lazima ununuliwe shati au maua zawadi ni kitu chochote, kwangu nimejua kuna kijana anaitwa Rogers Mtagwa,Ashante ISSA MICHUZI Kwa zawadi hii tutamtafuta kwenye mitandao

    ReplyDelete
  8. Bwana Michuzi acha utani bwana.. wewe jina lako limeshatangazika kama sio kukubalika miongoni mwa wabongo waishio huku ughaibuni. Najua umetoka mbali.. nakumbua enzi zile ukitupiga picha YMCA wakati wa disco Boogie ukitoza Shs. 80 kwa copy...lakini pamoja na hay yote usituabishe...Kwa kifupi huku ughaibuni hasa hapa USA holiday season huanza tangu siku ya Thanksgiving ambayo husheherekewa Alhamisi ya mwisho wa mwezi Nov. Kuanzia siku hiyo watu hufurika madukani kununua zawadi za xmas huku wakivutiwa na sale za bei poa..Ni utamaduni wa wamarekani kubadilishana zawadi wakati wa xmas na kutegemeana na umaarufu wako unaweza kuapata zawadi nyingi kiasi cha kuhitaji siku nzima kufungua ma-box ya zawadi tendo ambalo lilizaa Boxing Day.. I hope kama mungu akitujalia tukiiona xmass ijayo utatuletea kitu kinachohusiana na boxing day ya kweli na sio Rashid Matumla akiwa jukwaani akizichapa "Ndondi".... Kazi kwako muheshimiwa....

    ReplyDelete
  9. NYIE WABONGO, KWANZA TUNATIA AIBU SANA WENGI HUMU NDANI KWENYE BLOG YA MICHUZI MNAINGIA KUHARIBUNI NA KUTUKANA WATU NA KUELEZEA MATATIZO YAO ETI HAWAJASOMA, KATOE TONGOTONGO NA WENGI WENU HUMU NDANI MNAJITIA MMESONA MNABEBA MABOX HUKO UGHAIBUNI NA KUOSHA HALAFU MNALETA DHARAU NA MATUSI ACHENI HIZO MBONA HAO WANAO WANAOWABEBESHA MABOX HAWAWADHARAU? KAMA MTU HAKUSOMA AU AMESOMA YOTE KWANGU NI KHERI TU ILIMRADI SIMPI MSOSI WALA KUMLIPIA MJENGO WAKE, NAMCHUKULIA NI BINAADAMU KAMA MIMI NA ANAHAKI YA KUCHANGIA CHOCHOTE KILE. NDIO MAMBO YA UDINI NA UKABILA MNAYALETA.MICHUZI WANAJIFANYA WANAYAJUA MAMBO YA THANKS GIVING,SASA BOXING DAY INAHUSIANA NINI NA ZAWADI ZA X-MAS MAMBO YA THANX GIVING? TUAMBIANE WASOMI, TUSIOENDA SHULE TUJUE

    ReplyDelete
  10. wewe unamjua MATUMLA, sasa kwa taarifa yako huyo sio Matumla umepewa site uingie na ndio utoe comments zako

    ReplyDelete
  11. Ohyaa Mzawa acha kuchemka...kama zungu linapanda here you go:
    the name given to the December 26th public holiday, which was synonymous with the boxing and exchanging of gifts.
    Kazi kwako

    ReplyDelete
  12. YAANI KUNA KITU NIMEGUNDUA HUMU BLOGINI KUNA WATU NI MALIMBUKENI SIJAPATA ONA... AU WANAJIFANYA KUJUA KILA KITU HUMU DUNIANI. SAD ENOUGH WOTE WANAKURUPUKA TUU NA KUTOA MAONI BILA KUFIKIRIA VIZURI. SIDHANI MICHUZI KATIKA UMRI WAKE HAELEWI MAANA YA BOXING DAY WHETHER NI MPAGANI MKRISTU AU MUISLAMU... SO HAPO MMECHEMSHA.

    APART FROM KUELIMISHANA HII BLOGU NI SEHEMU YA KUSOCIALIZE WHICH MEANS WATU WANARUHUSIWA KUWEKA JOKES (KWA MFANO HUYO ALIYEPOST HIYO PICHA) TO MAKE OTHERS HAPPY LAKINI UJUMBE KATIKA PICHA HIYO NI KUJUA KUWA WATZ TUNA KIJANA BONDIA MAHALA FULANI... HIVYO KAMA NI KUCHANGIA IT SHOULD BE ON THOSE GROUNDS NA SIO KUJITIA KUTUELIMISHA KUHUSU BOXING DAY AU THANKSGIVING... AMBAVYO KILA MTU ANAJUA NA HATA HIVYO SIO MUHIMU.

    KWAHIYO SOMENI NA MUELEWE MAUDHUI YA PICHA KAMA KUNA INFO KUHUSIANA NA HILO HAZIKO SAHIHI NDIO VITU VYA KUCHANGIA. NA PIA SIO ZIONYESHE WENGINE HAWAJUI AU WASIOJUA NI WAJINGA... NO WAY!!

    dadakee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...