naposti hii picha nikiwa na simaro lutumba wa bana oke fasi ya kishasa pamoja na maelezo haya kwa fahari kwani leo natimiza posti yangu ya 2000 na ushee. asante wadau kwa kunipa kampani. naahidi kutowaangusha na kuliendeleza libeneke la blogu. asante ndesanjo macha kwa kunitoa tongotongo la tekelikujualo pale helsinki siku ile septemba mwaka jana. nashukuru pia kwa kupata wageni zaidi ya 600,000 na ushee kwenye blogu hii ya wabongo wote, ingawa nasikitika kwamba imenibidi nikontoroo komenti kwani kuna wadau wenye hobi ya kupitiliza ya kutajana majina. hata hivyo nafarijika kwamba natemebelewa na takriban wadau karibu dunia nzima wapatao 100,000 kwa siku...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Michuzi, hongera! Lakini takwimu zako zaonekana kuwa umezi-dokta au (kwa kutumia msamiati mwingine wa Kiingereza) umezi-sex up!

    Sasa hivi nilipofungua hapo chini upande wa kulia kulionyesha kuwa 609,625. Yaani imefunguka mara 609,625. Hii haina maana kuwa nilikuwa mtu wa 609,625 kutembelea blogu hii! Kama kwa muda wa dakika mbili nitaifungua blog hii mara tano pekee duniani (bila mwingine kuifungua), automatically itaongeza idadi hiyo na kuwa 609,625 + 5 = 609,630!

    ReplyDelete
  2. Born Again Pagan, hiyo bado ni sawa kabisa kwa mahesabu ya Michuzi na teknolojia. Kama ukiingia na kutoka, na baadaye kuingia tena hizo zote ni ziara tofauti na unahesabika kuwa umetembelea mara kadhaa. Takwimu hizi haziangalii 'mtu' bali zinaangalia 'hits'

    ReplyDelete
  3. Michuzi, unaweza kutupatia picha kadhaa za ule ulilokuwa uzinduzi wa Twanga chipolopolo dayamondi?
    Hongera kwa 2k picha!
    Kila la kheri, unatufaa sana sisi tuliougaibuni..

    ReplyDelete
  4. Sasa maana yake anatembelewa mara kadhaa na siyo idadi ya watu.Born Again upo sahihi na GHMM si kila kitu unakijua.

    ReplyDelete
  5. Kwa mehesabu yenu hapo juu, kama ni "hits" basi takwimu za hits 100,000 kwa siku sio sahihi. La sivyo idadi ya hits ingekuwa zaidi ya 600,000 toka aaanze-anahitaji siku sita tu kufikia 600,000!

    ReplyDelete
  6. Which is why nilisema hapo juu kuwa ....kwa kutumia msamiati mwingine wa Kiingereza) umezi-sex up!"

    ReplyDelete
  7. Michuzi hongera kwa kazi unayofanya.Ila niseme tu si vyema ukakontrolu baadhi ya maoni ya watu juu ya mambo unayotupa.
    Nafikiri acha watu wazungumze, unafikiri tutajuaje waheshimiwa wetu wana vijitabia fulani visivyokubalika ktk jamii? Magazeti yetu yanawalinda wakubwa na hata macelebrite wa bongo.
    Ni vizuri acha kwani matusi si yako ila yanawakilisha jinsi mlengwa alivyo kinyume na tumjuavyo.
    Ni ushauri tu ila we pima uone kama itaathiri staha yako basi uamue.

    ReplyDelete
  8. Unajua hata mimi niliposoma hiyo ya wageni 100,000 kwa siku nikasema duh kwa hesabu hiyo unazungumzia zaidi ya wageni laki sita kwa kipindi chote ambacho hii blog imekuwa hewani, nadhani labda maximum hit iliyowai kupata kwa siku 100,000 nimesema nadhani kwa sababu sidhani kama alikuwa anania ya kupika hiyo taarifa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...