wanakinshasa wakivinjari

nilipigwa butwaa kukuta kumbe Kinshasa, tofauti na dar wenye kumbi kibao (japo za kubabia) za muziki, hakuna kumbi nyingi zaz muziki kama utavyofikilia.

Grande hotel, iliyo katikati ya jiji na moja ya hoteli mbili kubwa jijini hapo, ndio kama diamond jubilee yao. Wanamuziki wazito wote na wa nje hupiga hapo, kwenye kitu inaitwa ‘salon congo’. Vinginevyo ni baa ama kama ni onesho basi hufanyikia uwanja wa mpira ama sehemu chache zenye kumbi ndogo ndogo.

Matongee, kitongoji unachoweza kufananisha na manzese, ndipo kwenye kumbi za baa na utakuta bendi kama zaiko langa langa, bana oke na wengineo wakitumbuiza. Koffi utamkuta sehemu inayoitwa quartie latin, ila yeye kwa vile ni heviweiti hufanyia shoo zake grande hotel, na mama yake mzazi ndo anakaaga getini kukusanya faranga.

Yeye koffi na wanamuziki wengine mara nyingi huwa Kinshasa kwani maisha ni rahisi kuliko nje, ila wanasafiri sana kwa maonesho na kurekodi. Kina tshala muana, mbilia bel, redi hamisi, wazekwa na wengineo wako tu Kinshasa wanadunda. Wengi wao hutembea wakiwa na kundi kubwa la mabodigadi

Sehemu ingine yenye starehe ya muziki ni chez ntemba, katikati ya jiji, ila ni klabu cha usiku kaka jj blue ama bilikanas, hivyo muziki ni wa disko tu. Mmiliki wake, kayembe chez ntemba anaishi afrika kusini na ana matawi zambia, Johannesburg na Zimbabwe.

Hakika kinshasa mokili mobimba kweli kweli…

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. michuzi hiyo gari, mimi sitaki uchokozi

    ReplyDelete
  2. Michuzi bwana mie uandishi wako unanitia mashaka, mbona kama vile hujaedit kile unachoandika. Au labda mie naelewa tofauti, nikisikia mwandishi najua ni mwandishi wa habari, au wewe ni mwandishi mpiga picha tu? Naomba ufafanuzi plz!

    ReplyDelete
  3. Eti wanamuziki maarufu Kongo huwa natembea na mobodiguard !! Michuzi acha uongo wale ni wabeba unga wa kuuza wa wanamziki!Wanamuziki wengi wa Kongo ndio zao hizo.Ungewapekua hao mabody guard ungeona mambo

    ReplyDelete
  4. Gari bomba sana hii ni ya mama yake mzazi Kabila. Ingekuwa hapa Bongo ukiipanda ingekuwa rahisi kuwahi foleni kwa sababu halina breki, kila dereva hata wa daladala na Askari Trafiki angeipisha njia kwa kuogopa kugongwa.Matokeo ya kupishwa yangekuwa kuwahi unakoelekea.Napendekeza magari yasiyokuwa na Breki kama hilo yasajaliwe mengi Dar ni ufumbuzi wa foleni na trafiki waliozoea kusimamisha magari ghafla na hovyo kwenye taa.

    Bei gani hilo Michuzi mimi nalitaka.

    ReplyDelete
  5. Michuzi ni kweli hii gari inaruhusiwa kuwa barabarani? au jamaa wana-ect tu?.Is very sad!!, hawa jamaa uchumi wao unaliwa na wafaransa.Na mbaya zaidi wanasujududia mno Ufaransa, kiasi cha kutopenda nchi yao.Sasa kutembea na kundi la walinzi si utumwa huo, raha hapo hipo wapi?

    ReplyDelete
  6. Wanamuziki wengi kule ni Recording artists.Biashara inalipa zaidi kwa kuuza CD,DVD nk kuliko kupiga kwenye maholi kila wikiendi.
    Na sisi Bongo naona hivi karibuni tutakua hivyo.

    ReplyDelete
  7. Bongo hatuna waandishi wa habari, tuna "reporters" tuu.

    ReplyDelete
  8. Michuzi, asante kwa ujumbe kuhusu Kinshasa. Nina rafiki toka Congo amabaye kila wakati anambia twende Kinshasa tukatanue. Basi picha yangu ya Kinshasa ilikuwa kwamba kwa miziki huko ndo kwenyewe mithili ya bongo. Kumbe wanapigia Matonge! Anyway, tambola na mokili omona makambo...its worth going!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...