Home
Unlabelled
kiswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hi mto ua makongo high school? mbona wanatumia chalk ubaoni?
ReplyDeletehallow bwana zablon mgonja!
ReplyDeletehongera sana kwa kazi unayoifanya ya kuwafundisha lugha yetu ya kibongo hao wanaughaibuni,naamini kwa mchango wako wewe ipo siku kiswahili kitakuwa mojawapo ya lugha za kimataifa,
Mungu akubariki
kumbe marekani kubwa kweli. maana kuna majimbo unaweza usione mtu mweusi siku nzima akipita mbele yako. hili jimbo linaonekana kuwa na wamarekani weusi wengi sana.
ReplyDeletehivi ina maana hakuna weupe kabisa huku (wazungu) ? kama wapo, je hawapendikusoma Kiswahili? afu pia kuna sehemu usa ingekuwa vigumu sana ku-publish picha kama hii, hadi upate kibali cha kila mmoja aliyemo kwenye picha, tena cha maandishi. lakini nadhani Tennessee inaenda kibongo bongo. safi lakini.
mlalahoi.
Hey mlalahoi unaonge apumba kweli. Kwani lazima mzungu ajifunze kiswahili. Kwani mzungu ni nani? Halafu kuhusu picha uko nyuma kweli na law. Once unachukua picha na camera yako. Kila aliyepose hana legal right. Kama umemcchukua mtu picha bila idhini yake ndio huna right ya kuiweka. Kila state ina weusi sijui kama upo USA mahali pamoja na hutembei. Tembea uone. TN ni state nzuri sana tu.
ReplyDeletePamojana sifa zote zilizotolewa hapo juu, ukiishi nje kiswahili hakina nafasi kabisa. Kwani ukiwa unafanya kazi, instructions zote ziko in english, na hata ukienda dukani kutafuta mahitaji wanaouza dukani wanaongea english. Kwa hiyo ndugu msidanganyike na hii info mkafikiri watu wanaongea kiswahili mitaani. Bado english ni more importnant ukiwa kama U.S., au U.K. Lakini kama una mpango wa kuishi TZ milele, sawa kuza kiswahili.
ReplyDeleteMlalahoi,
ReplyDeleteFisk University ni moja kati ya HBCU (Historically Black Colleges and Universities) kwa hiyo utakuta enrollment yake karibia 95% au zaidi ni Blacks. Kwa hiyo haishangazi kuona kwenye hiyo picha ya hayo wanafunzi wanaosoma kiswahili karibia wote ni weusi. Wazungu wengi wanaosoma HBCU hupewaga scholarships ili kuongeza diversity.
Hiyo pia hutokea kwenye shule ambazo unakuta 95% au zaidi ni Whites na inabidi kutoa scholarships kwa Blacks ili kuongeza diversity. Michezo kama Basketball na Football ni sehemu nyingine inayosaidia kuongeza Blacks kwenye vyuo ambavyo vina Whites wengi.
Ebwana Mlalahoi, we huoni caption zinasema ni Fisk University?? Fisk ni moja ya HBCU's Marekani kwa hiyo usitegemee kuona wazungu kibao. Halafu ni Tennessee. Ni jimbo la kusini. Asilimia karibu 56 ya Wamarekani weusi wanaishi kwenye majimbo yaliyo kusini. Sasa unachoshangaa ni nini???
ReplyDeleteKuna kitu kimoja jamani kuhusu hawa wamarekani weusi.Usifikiri kwa kuwa wewe ni mwafrika mweusi basi ukija huku watakukubali kama mwenzao. Hapana. Hawa wamegawanyika. Kuna ambao wanawaona waafrika kuwa ni watu wa nyuma, wasiojua lolote, na kwamba waliwauza utumwani, kwa hiyo wana kinyongo. Pia wengine wana wivu kwa kuwa waafrika wakija U.S. wanajiendeleza katika muda mfupi na kuwa mbali kimaendeleo kuliko wao waliozaliwa hapa U.S. Pia kuna kundi lengine linalowakubali waafrika, kwa mtazamo kuwa waafrika ndio asili ya mamarekani weusi. Kwa hiyo usishangae ukiwa U.S. wamarekani weusi wanaweza kuku treat vibaya kuliko ambavyo mzungu ata ku treat wewe mwafrika. It is a very complicated issue. Hiyo picha ya huyo lecturer isidanganye watu.
ReplyDeletesasa jamani ndiyo sikukuu za KWANZA zimeanza mablacks hua wanapenda sana kujifanya ni Waafrika hata kuliko sisi ila mablack wenyewe ni wale wenye shule kidogo au walio lelewa kwenye maadili mazuri the rest hua hawana hata habari what the fu......ck is KWANZA.
ReplyDeleteMAYOR,
ReplyDeleteSasa umetoa maelezo ya kwanini hicho chuo kina wanafunzi wengi weusi, halafu unaniuliza tena ninashangaa nini??? Unafikiri ningeuliza au kushangaa kama nina data zote ulizotoa hapo juu. Au wewe ukishaijua USA unahisi wote tunaijua kama ulivyoielezea wewe? Maarifa au ufahamu haufanani baina ya mtu mmoja na mwingine (knowledge is not universal, I believe). Ila tu ukweli ndio utakuwa ni wa aina moja (truth is universal). Na uliyoyaelezea wewe hapo juu sio vitu universal vya kueleweka na kila mwanadamu. Ukijua wewe si lazima nami nijue. Ingekuwa nashangaa kuzama kwa jua, au Afrika kuwa na weusi wengi, hapo ungeniona wa ajabu. Sasa hiki ni chuo Kikuu ambacho darasa nimeona halina mweusi na ni nchi yenye weupe wengi kuliko weusi. Lazima nisome kwanza, au nitembelee ndiyo ningejua hilo. Unafanana na baadhi ya wazungu wanaodhani kila mtu duniani anaijua Ulaya au USA.
Halafu, "ANONYMOUS" hapo juu kaeleza kuwa ukiishi nje Kiswahili hakina nafasi kabisa. Huo ni uwongo uliokithiri. Kwanza twambie ni sehemu ipi ya USA au UK unayoielewa hakina nafasi kabisa. Pili, una fikra fupi sana juu ya umuhimu wa lugha. Kwako, lugha ina umuhimu maofisini na dukani au katika biashara tu? Pole, hata Wenyeji wa nchi ulizotaja wanaojifunza Kiswahili watakushangaa. Kwani wengi wanaishi nchi hizo ulizotaja kwa kufundisha Kiswahili, na wanasaidia wenzao Tanzania. Unafikiri kuishi nje lazima iwe ni kwa kilichokupeleka wewe??? Nyie ndio mlikimbia Tanzania baada ya kujifunza Kiingereza kwa lengo la kupata kibarua au kutarajia utaongea Kiingereza na kila mtu unayemkuta USA au UK. Kwa taarifa USA ina maeneo yanayokaliwa na watu wasiojua Kiingereza na wameishi huku zaidi yako. Nenda California (San Fransisco) na New York city, mfano, kuna CHINA TOWN kote huku na wachina wengi hawaongei English, ukiongea English wanakuangalia tu. Haya, majimbo kama California nk, kuna Wamexico nk. wanaongea lugha yao tu na hawajui Kiingereza. Kwanini hufikirii na Kiswahili kitajijenga na kuwa na wazungumzaji wengi?
Ushahidi wa kukua Kiswahili USA: Mosi, vyuo(colleges and universities) kati ya 50 na 70) wanafundisha Kiswahili USA. Pili, vitabu vingi vya Kisw. vinatumika
dunia nzima na vimeandikwa na watu waliojifunza Kiswahili nje ya Afrika. Mfano, wengi wamesoma Ujerumani, USA, UK, Finland,nk. Tatu, BBC, Voice of America haisikilizwi na waafrika tu, bali na wazungu wengi waliojifunza tu Kiswahili. Nne, kuna wataalam wageni wengi wa lugha waliofanya na wanaendelea na utafiti juu ya Kiswahili, na matokeo yanatumika hata na wakufunzi hata Afrika. Tano, ukikutana na wageni wanaojua Kiswahili nje, wakikujua tu wanataka kujionesha kwa kuzungumza lugha yako ya Kiswahili. Na mengine mengi.
Kwa hiyo, maneno uliyotamka "anonymous" yanakuaibisha kama wewe ni Mtanzania. Maana watakushangaa hata wageni. Mwulize huyo 'lecturer' ni kiasi gani kiswahili kinapanuka siku hadi siku atakueleza. Najua wewe uko "BUSY" na kilichokupeleka ughaibuni, kutafuta hela. Ndiyo maana unaangalia ukuaji wake kwa namna finyu.
MLALAHOI.
Wewe anony wa 8.34 na ulimbukeni wako wa lugha na nchi za nje,unafahamu kwamba sio kila mweupe anajua kingereza??nenda Canada sehemu kama quebec unafahamu kwamba kuna weupe ukiongea kingereza kwao ni msamiati tupu??Fungua macho yako ndugu yangu na acha ulimbukeni na lugha za kigeni acha wanaothamini lugha zao wafanye kazi yao.lugha ni lugha muhimu mawasiliano na nyumbani ni nyumbani sasa kilikoni tusienzi lugha yetu??
ReplyDeleteWe anonymous wa 8.34 ni limbukeni sana tu,kama wewe mswahili huoni umuhimu wa kiswahili inakuwaje movies kibao za hao hao wa US zinatia kiswahili ndani?na nyimbo kibao katika movies zina kiswahili na hata michael jackson kuna wimbo wake moja una kiswahili inakuwaje wewe mswahili toka huku usione umuhimu wa lugha yako?sio utumwa wa lugha kweli huo?
ReplyDeleteWewe mlala hoi unasema tu. Pamoja na kuwa marekani ina wageni wengi toka nchi mbali mbali, lugha ambayo kidogo hapa U.S. tunaweza kuiita second language ni spanish. Lakini hiyo lugha yako kiswahili pamoja na kufundishwa kwenye vyuo vichache hapa U.S., bado haina nafasi KABISA. Kama huamini, njoo U.S. alafu kila mtu utakaye come accross with, iwe ni mitaani ukitembea, au dukani unifanya shopping, au ukibahatisha kibarua mahali, au uki enroll madarasa shuleni, alafu ongea nao kiswahili uone kama wata respond. Lakini ukiongea spanish, kati ya watu 20, unaweza ukapata mmoja ambaye atakupatia tafsiri. Nina sema haya kutokana na personal experience. Nimekuwa naishi U.S. kwa zaidi ya miaka 6 sasa, na kiswahili huwa nakizungumza ONLY ninapokutana na watanzania wenzangu. Na sio siri, English bado ni muhimu sana, kwani tunawajua watanzania waliocha kazi, au walionyimwa kazi kwa kuwa tu English yao ni MBOVU. Na hakuna sababu ya maana kwa mtanzania kuongea English mbovu wakati english tulianza kufundishwa toka darasa la tatu. Kwa maneno mengine, kiswahili inapokuja kwa watanzania kuishi kwenye English speaking country, bado kwetu ni tatizo kwa sababu watanzania wengi hawatilii umuhimu englsi toka wakiwa shuleni. Utasikia mtu anasema "mimi english itanipeleka wapi". Sasa wakija huku nje wanabaki wanajiuma uma midomo kwa sababu hawawezi kuongea. Matokeo yake mtanzania akienda kuomba kazi na mkenya, mkenya ana chance kubwa ya kupata kazi kwa sababu anaongea fluent english. Kiswahili ni lugha kubwa, lakini English is more important, trust me on this one. Or fly to the U.S. bila kuwa na mwenyeji atakaye kupokea airport alafu kila kitu uulize watu in english, ndio utakapoona umuhimu wa ENGLISH.
ReplyDeleteMichuzi mtu huyu ambaye unasema ni mhadhiri wa Fisk university hayumo kwenye orodha ya wahadhiri wa Chuo hicho.Sijui amekuwa classfied kama nani....you can just check for yourself.Facts check....inasema mhusika hatambuliki!!!So.....I don't know.Nafikiri kuna umuhimu wa facts checks badala ya kudandia na ku-post kila habari unayotumiwa.Tafadhali usiokote habari,kama huna nafasi ya kusaka na kuhakiki unachoandika ama kuweka hewani.
ReplyDeleteAnonymous hapo juu, unachoongelea ni point tupu. Lakini ingekuwa ni mtihani ningesma unajibu swali au mada nje kidogo ya swali la msingi. Tatizo lako na yule aliyekandia Kiswahili ni kwamba mmekwenda kwenye kitu kinaitwa 'falacy of generalization'. Hivi unaposema, Kiswahili "HAKINA NAFASI KABISA", what is the implication? Tena, mwenzio wa awali, kwa taarifa yako hakutaja kabisa ni mtu gani Kiswahili hakimsaidii (Mtanzania au mgeni anayekisoma). Huwezi kuni-convince kwa ujumuisho au 'generalization' unayoiendeleza. Unless kama watu mnatoa tu mawazo kama 'lay people'. Lazima uwe na ground unapotoa urgument ili iwe solid. Ulichofanya wewe ni kulinganisha 'status' ya Kiswahili na Kiingereza, of which hakuna atakayesema Kiingereza kina nafasi sawa na Kiswahili nje. Ila kukataa asilimia 100 ndio mnaonesha bado tafsiri finyu juu ya umuhimu wa lugha yoyote duniani. Kwako wewe umuhimu wa lugha ni kuisikia ikiongelewa kila mahali. What about other functions it fulfills in those countries? Lakini anyway, siwakatazi kuwa na mawazo mliyonayo, maana mnaongea 'from a very personal perspective'. Uliza wabongo wanaoona kinawasaidia. Mie pia nawajua wengi wanaofaidi kwa hicho hicho Kiswahili, ukiacha wewe na aliyekikandia mwanzo. Kamwe sidharau Kiswahili kwa kiasi hicho, hata kama hakilinganishwi na English.
ReplyDeleteMLALAHOI.
December, 2006
ReplyDeletefront page
Tanzanian Ambassador Andrew Daraja Visits Fisk University
Ambassador Andrew Daraja visited Fisk during his stay in Nashville during Tanzanian Independence Weekend at the request of the Middle Tennessee Tanzanian Association.
Fisk University welcomed The Honorable Andrew Daraja, Tanzanian Ambassador to the United States during a reception on December 8 in the Board Room of Cravath Hall. Daraja met with Fisk’s 2006 Fulbright Scholar and Tanzania native Zablon Mgonja in addition to Fisk’s faculty, staff and students.
“Fisk University was tremendously pleased to have Ambassador Daraja visit our campus,” said Fisk Provost Dr. Kofi Lomotey. “The relationship between the U.S. and Tanzania has been strong and we were glad to exchange ideas with the Ambassador about possible links between institutions in the East African country and Fisk University.”
“Having Zablon Mgonja here as our Fulbright Scholar for this entire academic year has been rewarding,” Dr. Lomotey continued. “We were glad to have provided the opportunity for these two countrymen to meet and interact on our historic campus.”
Ambassador Daraja was first appointed as the Tanzanian Representative to the United States of America in July 2002. Since his first appointment as an ambassador in 1991, Daraja has also served as Tanzanian representative to Germany, Poland, Austria, Switzerland and Holland. Daraja has visited 73 countries since he was first named to the Tanzanian Foreign Service Office in 1970.
As a Fulbright Scholar, Zablon Mgonja teaches Swahili at Fisk in the modern foreign languages department. The Fulbright Scholar Program enables scholars from abroad to teach in America in an effort to promote global engagement. After careful consideration of several qualified candidates, Fisk selected Mgonja based on his academic excellence and extensive command of five languages (English, Chasu, Masai, Shambala and Sukuma) in addition to Swahili. He is also enrolled in French courses at Fisk.
“The more languages a person speaks, the more opportunities they’ll have,” Mgonja says. His native Kilimanjaro is home to more than 125 ethnic groups and more than 100 languages.
Daraja’s visit to Fisk followed the recent secession of global and community leaders that visited the university in 2006 as a part of the Global and Community Lecture Series and University Convocations. Speakers have included Attorney Vernon Jordon, The Honorable Melvin Watt, The Honorable Mickey Kantor, educator and author Dr. Dennis Kimbro, acclaimed poet, essayist, educator and Fisk Alumna Nikki Giovanni and Fisk Visiting Distinguished Professor Dr. Preston King. Daraja was invited to Nashville by the Middle Tennessee Tanzanian Association in celebration of Tanzanian Independence Day on December 9.
Copyright 2006 Fisk University